gstar
JF-Expert Member
- Jun 19, 2011
- 786
- 1,367
Habari zenu wakuu.
Ni majuzi tu iliripotiwa kuwa mheshimiwa Mkuu wa mkoa wa DSM ndugu Paul Makonda kuwa amesafiri kwenda Afrika ya kusini kwa likizo ya miezi miwili taarifa hiyo ilitoa uthibitisho wa clip ya video aliyo pigwa akiwa uwanja wa ndege wa OR Tambo huko south.
Kabla ya hapo mheshimiwa Makonda alisafiri kwenda ulaya na kuzunguka kwa zaidi ya mwezi mmoja, haikufahamika kwamba ziara ile ya ulaya ilikuwa ni ya kiserikali au ya kibinafsi na ni nani alikuwa anagharamia ziara ile.
Mheshimiwa Makonda ni muajiriwa wa serikali na sidhani kama kuna sheria inayo mpa malaka ya kujipangia likizo ndefu kila baada ya miezi kadhaa.
Kuna mdau alitupenyezea hapa kuwa mheshimiwa Makonda jana alikuwa kwenye ndege kurudi Dar es Salaam na leo ni kweli ameonekana kwenye uzinduzi wa barabara maeneo ya Kurasini. Swali hapa ni je amesha maliza likizo au bado inaendelea? nakama likizo yake inaendelea ni kipi kilicho mtoa huko sauzi kuja kuzindua barabara kama sio ufujaji wa fedha ni nini?
Swali jingine ni kuwa je baada ya huu uzinduzi ataendelea na likizo yake au atarudi ofisini. Kuna kitu kinajificha hapa nyuma ya pazia ambacho tusipo kipigia kelele kitatuumiza sana na inaonekana kama mheshimiwa raisi amepigwa ganzi kabisa!
Maswali ya kujiuliza;

- Raisi alipiga marufuku safari za nje lakini RC wa dsm anasafiri nje kila mara na hachukuliwi hatua
- Uhakiki wa vyeti ulifanyika kwa wafanyakazi wa serikalini lakini kwa Mheshimiwa Makonda serikali imepigwa ganzi (no one is talking)
- TAKUKURU wamepigwa ganzi hawamchunguzi mkuu wa mkoa pamoja kuwa na kashfa za matumizi mabaya ya fedha na mengine yalisemwa Bungeni
- Amekataa wito wa bunge na hakuna anaye mshurutisha