Naanto Mushi
JF-Expert Member
- Oct 16, 2015
- 6,236
- 15,673
Habarini wana jukwaa,
Ni siku moja imepita na ya majonzi makubwa, taifa limepoteza vijana takribani nane waliokuwa wanahudumu katika jeshi la polisi. Hakika nimeguswa moja kwa moja kwa vijana tuliowapoteza;
1) Kwa sababu ni vijana wenzangu na
2) Kwa kuwa ni watu katika jamii, wana familia zao zilizokuwa znawategemea. Kwa namna moja tukio hili huenda lika athiri moja kwa moja uchumi wa familia takribani nane. Nimeongea hili kwa kuwa nafaham hali halisi ya familia zetu. Vijana wengi walioenda upolisi wametoka familia duni na wengi wanategemewa na familia zao.
Kwisha kusema hayo nataka niingie kwenye issue ya msingi kama kichwa cha habari kinavosema. Baada ya tukio hili kutokea habari nilizozisoma na reaction niliyoipata ni kwamba "Magaidi" "Majambazi" "watu wasiojulikana" ndio inasadikika walitekeleza tukio hilo la majonzi.
Tukio kama hili sio mara ya kwanza kutokea, kwa kipindi cha kama miaka 3 iliyopita matukio kama haya yamejitokeza kwa wingi. Lakini kinachoshangaza ni kwamba mpaka leo serikali imeshindwa kutoka hadharani na kueleza source ya haya mambo yanayojitokeza.
Miaka 10 mpaka 15 iliyopita matukio ya ujambazi na ya "watu wasiojulikana" walikuwa wakivamia mabenki na sehemu zenye fedha. Miaka mitatu iliyopita hadi sasa mbali na mataukio ya ujambazi, limeongezeka hili la askari kuvamiwa na kuuawa.
Hii changing behavior of crimes, kutoka kuvamia mabenki na kupora pesa mpaka kuvamia vituo vya polisi, kuua askari na kupora silaha ni jambo ambalo linapaswa kuangaliwa kwa mapana na kufanyiwa utafiti wa kina.
Kitendo cha kutuhumu Majambazi, Magaidi, na watu wasiojulikana, nakichukulia kama kitendo cha dharau kwa serikali kukwepa majukumu ya kutafuta chanzo na kutokujali thamani ya maisha ya watu waliofariki.
MAWAZO BINAFSI NA OMBI KWA SERIKALI
Namshauri waziri mwenye dhamana, RAIS MAGUFULI, IGP wafanye yafuatayo.
1) Kiundwe chombo ndani ya wizara ya mambo ya ndani ambacho kitafanya kazi kwa karibu na taasisi za utafiti wa mambo ya kijamii. Chombo hiki kazi yake itakuwa ni more of Intelligence, ku monitor changing behavior of society towards vyombo vya usalama. Na pia kutafuta na kufanya estimation ya causation ya matukio ya crimes.
Mfano kwa situation ya Tanzania kwa sasa, unashindwa kuelewa the real reason ya mauaji yaliyotokea. Unaweza kusema majambazi, unaweza kusema magaidi. Lakini je tukisema ni wananchi wenye hasira, unaweza kutoa hoja zipi za kupinga?
Je mahusiano ya polisi na wananchi yana afya? Kwa mara nyingi kiasi gani polisi wameonekana kuumiza hisia za wananchi? Je kuna anayeweza kupima reaction ya mtu aliyeumizwa hisia?
Serikali iache kujificha kwa kufunika macho angali i uchi... Itafute chanzo, haya mambo yana chanzo, suala la kusingizia watu wasiojulikana hakitusaidii sisi wananchi.
Busara za Naantombe