Serikali iokoe jahazi Shule ya Sekondari MWAMALA-Nzega,70% ya wahitmu Form 4 wametumia majina yawatu

Civilian Coin

JF-Expert Member
Dec 2, 2012
2,305
4,380
cc. Waziri wa Elimu
cc.Katibu Mkuu Wizara ya Elimu
cc.TAMISEMI
cc.Mkuu wa Mkoa Tabora, RAS Tabora, R.E.O Taboara
cc. Mkuu wa Wilaya Nzega, DAS Nzega, Mkurugenzi wa halmashauri Nzega, D.E.O Nzega
cc. PCCB-Nzega, Usalama wa Taifa Nzega.

Salaam zangu ziwafikie wote, leo ikiwa ni jumapili mwanana na tukufu mbeleza Mungu kwangu na wewe msomaji wa makala hii inayokwenda kuzungumza ukweli halisi wa mambo. Mlio makanisani nawatakia ibada njema na mkitoka tuendelee na mjadala hapa jamvini.

Mimi nimekuwa Mwalimu mwajiriwa pale Mwamala sekondari, halmashauri ya Nzenga, Tabora na nimekaa kwenye shule hiyo tangu mwaka juni 2007 mpaka juni 2012 kama mwalimu wa Leseni (Induction Course) iliyokuwa inatolewa kwa kuajiriwa kwa miaka 5 tu.

Shule hii ya Mwamala ilianza rasmi mwaka 2006 na kidato cha kwanza na Form 4 ya kwanza kumaliza ilkuwa ni mwaka 2009, Form 4 ya pili ni mwaka 2010, Form 4 ya tatu ni mwaka 2011 na Form 4 ya nne ni mwaka 2012. Hapa nitazungumzia haya madarasa manne yaliyohitimu mwaka 2009, 2010, 2011 na 2012.

Mkuu wa Shule wa kwanza alikuwa Mwalimu Mtalai ambaye alichukuliwa kutoka shule ya msingi na baada ya hapo alifata Mkuu mpya ambaye ni Mwalim Buswelu ambaye sasa amehamishwa.

Shule ilianza mwezi Juni 2006 kwa wanafunzi wa chaguo la pili, hivyo shule ilipata takribani wanafunzi 90 wakuanza nao kutoka shule za msingi ndani ya kata hiyo, kilichotokea ni kuwa waliochaguliwa wengi hawakupata taarifa na hivyo wananchi wakawaida waliomaliza shule miaka mingi (watu wazima) waliomba nafasi hizo kwa kutumia majina ya wanafunzi ambao hawakuripoti na walikubaliwa.

Mwaka Novemba 2006 shule ilivuma kuwa imeshafunguliwa na wanafunzi ambao hawakuripoti wazazi wao wakashituka kuwa majina ya watoto wao yanatumiwa na watu wengine, na hivyo ikawa shida kubwa sana, mwaka 2007 tulipofika sisi kutoka chuo cha ualimu Tabora tulikuta mjadala umezidi kuwa mkubwa huku wananchi wakitaka kufanya fujo juu ya majina ya watoto wao, nguvu kubwa ya vitisho ilitumika kuwatuliza na wengine kuwaomba wawalete watoto wao waendelee na majina yao, lakini watoto wenye majina walipofika walirudishwa kutokana na nguvu kubwa kutoka inje iliyoshinikiza kuwazuia.

Kimsingi darasa la wanafunzi takribani 90 wanafunzi 50 walikuwa wamechukuwa majina ya watu wengine, ilkuwa ni kero sana, na darasa jipya la 2007 nalo lilipochaguliwa kuja kuanza form 1 hali ilikuwa ni ileile yaani TSM 9 ya mtoto ni tofauti na aliyekuja kuripoti, rushwa ilitembea sana serikali ya kata na Tarafa, tulikuwa tunashangaa aina ya huu mchezo. Tulijaribu kuwasihi waliokuwa juu yetu waache hiyo tabia.

Cha kushangaza darasa jipya tena la mwaka 2008 form1 nalo likaja na mamluki wengi hasa mpaka naenda masomoni mwaka 2009 darasa hilo nalo lilikuwa ni majanga matupu.

Nilijaribu kujitoa mhanga binafsi kuongea na walimu wakuu wa shule za msingi za kata hiyo hasa shule ya msingi Mwamala, kishiri, mahene, relini na chaming'wa lakini wakuu wa shule hizi waliniambia mjini shule huku bushi ndio sehemu ya kula pesa kwani wengi bado wamelala na hawajui umhimu wa elimu acha tu watu watumie majina yao, nilichokiona mabinti walirazimishwa kuolewa na majina yao yakatumiwa na watu wengine, wavulana wao walikatishwa tamaa lakini walishangaa kuna watu wanatumia majina yao.

Wengi walifika na kuomba, basi wasitumie majina yao maana wana athiri watoto wao watako wazaa na pia wanaathiri majina ya koo zao, na wengine walifika mbali na kusema wana mpango wakujiendeleza mbeleni sasa kama majina yao yanatumika wao watatumia majina gani?

Tulipokaribia kuanza mitihani ya kidato cha pili mwaka 2007 ililazimu kuanza kufojisha majina kwa wanafunzi kwa maagizo kutoka juu, mfano usio rasmi Jina lililpo ni John Magoli na anayetumia jina hilo anaitwa Musa Kiboko, hivyo jina lililofojiwa na kuwa John Musa Kiboko au John Magoli kiboko n.k, lakini wengine iliwiwa ugumu kubadilisha na kulazimika kuendelea na majina ya watu kama yalivyo, walimu wenzangu nilijaribu sana kushauri ilikuachana na jambo hilo lakini nilidharauliwa sana na kuwekewa vikwazo vingi sana vya kimaisha ikiwemo kuzushiwa mambo ya hovyo ili nisiseme ukweli, maana wengine waliotumia majina hayo walikuwemo pia wadogo zao na walimu.

Nilichomewa utambi mji mzima wa mwamala na kuonekana ni mubabaishaji kwa kuwa natetea ukweli,mpaka nikazushiwa kuwa mimi sio mwajiriwa, nilishuhudia form3 ya kwanza wenye majina wakija kutaka kuendelea na majina yao kwa kuwa yameshafanyiwa mtihani wa kidato cha pili, lakini pesa ilitembea kwa siri, wanafunzi wenye majina ya watu niliwashauri sana na kuwaambia madhara yake mbeleni, kiukweli waliniona kama fala tu, maana wao walitegemea serikali ya kata na tarafa kuwatetea kwa kuwa ndio walikuwa wasimamizi wa uhalifu huo.

Form 4 ya mwaka 2009, 2010, 2011 na 2012 wote waliohitimu 70% wametumia majina ya watu, na wengine walirudia shule za msingi wakachukua majina ya watu walioacha shule na wakaja nayo sekondari japo hao ni wachache ila wengi waliochukulia sekondari majina hayo.

Msingi wa uanzishwaji wa shule hizi za kata umebeba majina ya watu hasa shule zilizoko vijijini maana wengine walitoka mijini na kuwahi kuchuka nafasi vijijini. kwa hiyo tusiseme tumeboresha elimu wakati watu wametumia majina ya watu na wenye majina WAMEWEKWA VIZUIZINI na kutishiwa maisha kama watainuka na kusema majina yao. Nipo Mwanza hapa wapo vijana kila nikikutana nao wanalalamika majina yao yametumika halafu wale waliotumia majina hayo wanawalazimisha waitwe kwa majina yao yaani kama kubadilishana majina hivi.
Wengine kila mwezi wanalipwa ili wasiropoke.

Wengine wameshaingia kwenye ajira mpaka sasa wakitamba kwa majina ya watu na kuongeza majina ya koo zao mwishoni ili wasijulikane.

Mimi Deogratius Kisandu, nimekuwa chukizo kwa wengi na ndio maana nimefilisiwa na wengi iliniwe kapuku ili nisiweze kusema ukweli wa mambo, nina mambo mengi sana maovu nchini hapa lakini tuanze na hili. Nasema hili huku wengine wamejipanga kunipakazia kesi eti nimezaa na mwanafunzi ili ninyamaze ili hali sijawahi kuzaa na mwanafunzi bali niliwahi kuzaa na Mfanyabiashara wa chakula(mamantilie) pale nzega mjini. Hata wanizushie vipi, ukweli taendelea kuuanika tu.

Tunatakiwa kujenga jamii mpya yenye ukweli na sio uongo, hata kama mkinifanyia ASASSINATION lakini ujumbe nimeshafikisha. Unajua wengi walifikiri mimi nimefoji majina na wakajua nitakaa kimyaa,mficha uchi hazai hivyo nauanika uchi ili tuzae Taifa jiya. Yaani nausema ukweli ili tujenge taifa jipya.

Najua mtakaa kimya kwa kuwa pia kuna Viongozi waandamizi serikali wanatumia majina ya watu na hawataki kuyaachia wala kuapa, Serikali ya Arena for Correcting Africa Tanzaia-ACA itawaweka sawa wakati ukifika, tuombeeni kwa Mungu tupate usajili.

USHAURI: Waliotumia majina ya watu kuyasomea waachie vyeti vya watu maana wamewasomea wengine kwa kuwasaidia maana hawakulazimishwa. AU utaratibu wa kisheria ufuatwe ili wakamtwe, AU waapishwe kuachia majianya ya wenzao maana sasa wanaadhirika watumie majina gani.

Kwa leo naishia hapa:

Deogratius Nalimi Kisandu
Mtemi Kiongozi wa Chama tarajiwa cah ACA
 
Acha umbeya. Mbona Bashite memuacha? Kweli nyan haoni kundule lake.
Achane watoto wa watu wasome. Wanafuata nyao ya kaka yao kibaka Bashite
*ccm shiwaladu*
 
Si huko tu. Wakuu was shule wengi wanafanya hivyo.
Hii inahatarisha usalaama wa nchi yetu maana mamluki wengi wanatoka nnje ya nchi.
Binafsi Nina mfano hai na nimefikisha sehemu husika lakini ufuatiliaji ni was kusuasua.
Ninampango wa kulipuka bila haya.
Tutakuja tawaliwa na watu wa nnje wenye majina yetu
 
oh it's this weirdo again . You've made a good point mwanzoni lakini huku mwisho umejaza utumbo.
 
Deo pole. Ushauri tu. Unaweza kuandika kero zako zote kwa siku moja. Maana kila leo mada zako ni kulalamika umeonewa, umewekewa vikwazo. Huna lingine la kuandika?
 
Back
Top Bottom