Serikali inawatengenezea vipato Wachina, huu ni wizi!

Waziri kivuli

JF-Expert Member
Nov 30, 2016
2,987
3,450
Nimechukua muda kufuatilia hizi mashine za bonanza,kwakweli ni wizi mtupu!

Serikali imebariki machine hizi kuingizwa na wachina na kuzipeleka mitaani kwa sh 100,000 kwa mwezi kila mashine!

Nimechunguza,mashine hizi ziko programmed "kula kingi" na "kutoa kidogo"! Randomly,kama wakicheza watu 20,kila mmoja akacheza 1000,itakuwa imechezwa 20,000!Katika hiyo elfu 20,itatoa labda 4000 kwa mtu mmoja kati ya hao 20!MTU huyo anaondoka akiwa na furaha kuwa amekula faida ya sh 3000 kwa buku aliloweka!Mchina anaondoka na 16000!

Kuna kijiji kimoja huko Kigoma,mchina alianza kwa kuweka mashine 1,ameona zinalipa,kwa sasa ziko mashine 6!

Wamenunua Harrier nyingi kwa ajili ya kuzunguka vijijini kukusanya pesa ambazo mashine hizo zinawapa!

Kiufupi watz wanatoka jasho kupata fedha na kupeleka kucheza kamari kwa mchina!

Serikali inaridhika na hiyo 100000 kwa mashine,hawajui kuwa wachina wanachukua zaidi ya Mara 10 ya kiwango hicho kutoka kwa watz wasiokuwa na uelewa ambao ni wengi!

Kama pesa ambayo inapotea kwenda kwa mchina ingewekezwa na hawa wananchi pengine return yake ingekuwa kubwa na baadaye wangechangia kodi indirectly kwa serikali!

Naiomba serikali ipige marufuku machine hizi,wachina wengi wamepata ajira kupitia mashine hizo!!Halafu wanatuona wajinga!
Sidhani kama China ingekubali nchi nyingine ipeleke mabonanza haya nchini kwao na kuwaingiza mkenge raia wake!
 
Una point lakini malalamikon yako hayana msingi. Nitaelezea: Msingi wa mchezo wowote wa kubahatisha ni kusanya kwa wingi lipa kidogo huku ukibakiwa na faida kubwa. Duniani popote kamari ndivyo ilivyo! Ila sasa Tanzania kuna tatizo moja. Sehemu nyingi duniani mchezo wa bahati nasibu unaendeshwa na serikali tena kwa uwazi. Bahati nasibu ni njia nzuri sana ya kuingiza mapato makubwa kwa nchi nyingi. Hapa kwetu kuna tatizo. Nadhani viongozi wa bahati nasibu ya Taifa huwa wanakatiwa kitu kidogo ili waachie hii michezo kwa watu binafsi. Tatizo kama fedha za kugharamia elimu ya juu lingeweza kupunguzwa kwa kiasi kikubwa kama shirika letu la bahati nasibu lingekuwa linajitangaza na kuchezesha ile michezo mikubwa inayoingiza fedha huku ikiachia kamari ndogo ndogo kwa watu binafsi.
 
Kwan umelazimishwa kucheza asee?................
Mtu yeyote mwenye busara anapoona tatizo hujaribu kulitatua, na kama hana uwezo hutoa taarifa ili tatizo liondolewe. Utakuwa ni ujinga kukaa kimya eti kwa sababu eti kwa sababu hathiriki moja kwa moja au hujalazimishwa kucheza.
 
tatizo watanzania wengi uelewa mdogo sana, watu wanataka "shortcuts" na faida ya haraka haraka na hawana matumaini, kwa kulijua hilo wachezesha kamari, wagaga wa kienyeji, wanasiasa, manabii n.k wanakula tu kirahisi kile kidogo ambacho masikini na mbumbumbu wa tanzania wanakitolea jasho kwa kuwauzia "hope", kuna wakati hua nafikiria kuwahurumia na kuwapigania watanzania ni "lost cause" lakini hua nakumbuka kuwa wengi wao hawakuchagua kuwa mbumbumbu bali ni mfumo duni uliopo katika jamii chini ya mkoloni mweusi CCM ambaye anatumia ujinga wa watanzania kama mtaji wake kisiasa
 
Analipa kodi,ameleta machine(aliinunua) kama anapata faida na kununua magari,kwa nini huko amjiungi kikundi ata watu watano mfungue kampuni mfanye competition mpate fedha?
 
Mteja ni mjinga katika bidhaa anayoipenda..
 
Hakuna mtu aliyelazimishwa kucheza, hii michezo ndio lengo lake kuchukua sana na kutoa kidogo, kwani hizo mizuka na biko zina tofauti? cha maana labda serikali iwabane zaidi wenye mashine walipe kodi stahiki! halafu tuendelee na usemi wa "wajinga ndio waliwao"
 
Naiomba serikali ipige marufuku machine hizi,wachina wengi wamepata ajira kupitia mashine hizo!!Halafu wanatuona wajinga!
Sidhani kama China ingekubali nchi nyingine ipeleke mabonanza haya nchini kwao na kuwaingiza mkenge raia wake!
kwani umelazimishwa kucheza?
kazi kulalamika tu,mapori hayana mwenyewe huko nenda ukalime upate pesa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…