The seer
JF-Expert Member
- Jul 31, 2015
- 407
- 690
Tangu serikali mpya iingie madarakani imekuwa ikisisitiza ukusanyaji mapato kupitia kodi mbalimbali.na imekuwa ikijisifu kwa kukusanya mapato makubwa na kuvunja record kwa mda mfupi lakini imekuwa haiangalii na kwa upande wa wafanyabiashara.ukusanyaji wa kodi ni jambo jema ni wajibu wa mfanyabiashara kulipa kodi lakini je serikali inaangalia mazingira ya wafanyabiashara.si jambo jema serikali kujisifu kukusanya mapato makubwa bila kuboresha mazingira ya wafanyabiashara ni sawa na kumkamua ng'ombe bila kumlisha majani.ni ukweli usiopingika mifumo ya kodi (tax system and tax structure) ya Tanzania ni mibovu inatakiwa iboreshwe na kurekebishwa ili ilete mazingira Mazuri kwa serikali kupata kodi na wafanyabiashara kupata faida.
SABABU KUBWA YA WAFANYABIASHARA KUKWEPA KODI NI KUTOKANA NA MIFUMO MIBOVU YA KODI.kwa mifumo iliyopo mfanyabiashara akisema alipe kodi kihalali basi faida atakayopata ni ndogo sana kutokana na mazingira mabovu ya biashara na ushindani wa bidhaa za nje ambazo zinazalishwa kwa gharama.ndogo
N.B serikali inapaswa kuwaangalia wafanyabiashara kwa kuboresha mazingira yao na mifumo ya kodi na ndipo ikusanye kodi.na si kujisifu kukusanya mapato makubwa bila kuangalia upande wa wafanyabiashara.