Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,529

Serikiali inapoteza dola za Kimarekani Milioni 30 kila mwaka kutibu wagonjwa wa saratani iliyotokana na matumizi ya Tumbaku ambao ni asilimia 32 ya wagonjwa wanaopata huduma katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na Ocean Road huku zao hilo likiingizia serikali dola za Marekani Milioni 15 tu.
Taarifa hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam na Katibu mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Dk Mpoki Ulisubisya wakati wa mkutano wa kimataifa ulioshirikisha nchi mbalimbali duniani kujadili athari za matumizi ya tumbaku na namna ya kukabiliana nazo.
Aidha amesema serikali imekuwa ikipata hasara kubwa ya kuwahudumia waathirika wa tumbaku ikilinganishwa na kiasi cha fedha zinazotokana na zao hilo fedha ambazo zingeweza kutumika kwenye jambo lingine ikiwemo ununuzi wa dawa.
Amesema kwa sasa serikali iko kwenye mchakato wa kuwatafutia wakulima wa zao la tumbaju zao mbadala ili waweze kuondokana na kilimo cha zao hilo na kuongeza kuwa katika kukabiliana na tatizo hilo wamepiga marufuku matangazo ya sigara na kutokudhamini jambo lolote.
chanzo; ITV