Moja ya mapungufu makubwa kwenye utawala wa JK ni kushindwa kwake kuwawajibisha wale wanaotuhumiwa kwenye vitendo vya kifisadi kama hao waliotajwa na Dr Slaa. Tatizo kubwa hapa naamini ni kitendo chake cha kuhusisha urafiki kwenye kuteua viongozi jambo ambalo limekuwa ni kikwazo kikubwa kwenye utendaji wa kila siku. Asipojitahidi kutenganisha uswahiba na uongozi tusitarajie mabadiliko yoyote hata akipewa miongo miwili au zaidi.
Ndiyo maana hatufai kama Kiongozi hivyo hafai kugombea tena 2010. Rais muoga ni hatari sana kwa nchi yoyote ile ikiwemo Tanzania.
Mwenzetu tupo wote sayari hii hii?Hosea atachukuliwa barua kwa mujibu wa taratibu, kwa sasa ngoja kwanza atekeleze wajibu aliopewa kwa na Rais Kikwete wa kuwashughulikia mafisadi. Ile ripoti ya kusafisha Richmond ilitoka kwa shinikizo. Sheria ya kudhibiti rushwa ili badilishwa baada ya hapo kumpa mamlaka zaidi na kumlinda dhidi ya mashinikizo. Sasa Hosea anachukua hatua
.............ndiyohiyo
Mimi nina wasi na uongozi wote wa JK...na uoga wake,kuingia kwafedha kifisadi,hana ubavu kusema na kutenda....akiweza kumkamata RA na EL ataweza kumkamata na kumfukuza yeyote yule...ila kama hawezi kwa hao 2 Hosea atakaa pale hadi 2010.heri tumpe Magufuli maana ameonyesha angalau cheche kidogo tangu awe waziri...wengine wotemizigo tu...