Serikali imeshindwa kutekeleza bajeti ya trilioni 29 inayokwisha

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
"SERIKALI IMESHINDWA KUTEKELEZA BAJETI YA TRILIONI 29 INAYOKWISHA, INAWEZAJE KUTEKELEZA BAJETI YA TRILIONI 31.6 IJAYO? MHE. MBOWE

Serikali imeshindwa kukusanya pesa ilizotegemea kutoka vyanzo vya ndani kutoka kwa wafadhili, leo kama vile haitoshi, serikali hiyo hiyo iliyoshindwa kutekeleza bajeti ya Trilioni 29 kwa sababu haina fedha inaleta tena mpango wa bajeti wa kutumia shilingi trilioni 31.6 huku ni kuwadanganya wananchi, hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Mbunge wa Hai, Mhe. Freeman Mbowe wakati akihutubia Baraza la Viongozi wa Kanda ya Kaskazini mkoani Tanga leo Jumatano 29/03/2017 katika ukumbi wa Ringo Naivera mjini Tanga.

Ameongeza mpaka sasa Serikali inakopa fedha kwa ajili ya kujuendesha, sio tu Serikali inakopa fedha kwa miradi ya Maendeleo bali inakopa fedha kuendesha operesheni za kawaida za Serikali kwa hiyo deni la Taifa linazidi kuongezeka.

Ulipaji wa kodi wa deni la Taifa kwa hiyo fedha nyingi zinakwenda nje ya nchi ndo maana kuna ukata mkubwa katika Taifa.Kupitia Rais, Serikali inafanya maamuzi mengine ambayo yanawatisha wawekezaji, na ukiwatisha wawekezaji wanaingia hofu ya kufanya uwekezaji mkubwa katika nchi yetu na ajira zinapotea.

Akizungumzia kuhusu sakata linalomkabili Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam amesema hamna mtu mwenye chuki binafsi lakini Watanzania wanahitaji viongozi wanaoweza kujenga mshikamano katika taifa na sio viongozi wanaoleta migogoro baina ya Serikali na wale inao waongoza, matendo ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam hayahashirii utawala bora.

Akizungumzia Uhuru wa habari na kutoa maoni amemtaka Rais awaache wananchi wazungumze, waobteshe hisia zao, hakuna mtu mwenye lengo la kumjaribu Rais, yeye ndiye Kiongozi Mkuu wa nchi anao ulazima wa kutusikiliza, tunachompa Rais ni free consultance , ushauri wa bure anastahili kupokea anastahili kupokea malalamiko na vilio vya wananchi wake.

*UCHAGUZI*

Kuhusu Uchaguzi wa kumchagua Mwenyekiti wa Kanda ya Kaskazini, Makamu Mwenyekiti na Katibu umehairishwa baada ya uongozi wa Chama Tanga uliokuwepo kuondolewa, Uchaguzi utafanyika baada ya Uongozi mwingine kupatikana na kutangazwa tarahe nyingine ya uchaguzi.
 
Ndio maana hata kuongeza mishahara ya watumishi wameshindwa.

Watadanganya lakini muda utawaambua.
 
Pesa yote imepelekwa Chato kujenga eti Chato International Airport !!

Nyerere aliwahi kuonya huko nyuma kuwa mkimchagua Rais toka kabila hili....... hakika atajenga na kupitisha barabara za lami na flyovers juu ya Ziwa victoria !!

Aaah bhana, unatoa bastola ya nini tena ? ??
 
  • Thanks
Reactions: MC7
Bajeti ya trilioni 29 imewashinda. Pesa walizotoa kwa mwaka mzima wa bajeti hazifikii hata 60% ya bajeti yote, sasa wanaudanganya umma wa Watanzania kwamba bajeti ya 2017/2018 itakuwa 31 trillion! Kweli hii Serikali imeamua uongo ni mbele kwa mbele.
 
Back
Top Bottom