Serikali imepata ugonjwa mbaya

usishangae kumsikia Makonda naye akitoa tamko la kuhamia Dodoma!
Makonda atanunua kiwanja ajenge nyumba Guest House , mbona wakuu wa mikoa yote Tanzania wanaishi Dsm ? Kila Mkuu wa mkoa ana nyumba Dsm wakimaliza kazi hurejea Dsm hata waliwa na nafasi hujichimbia Dsm , sasa wajenge Dodoma ili wasambaze maendeleo nchini kote.
 
Miundombinu Dodoma haijawa rafiki kwa lundo la wafanyakazi watakao hamia huko. Wewe angalia tu kipindi cha bunge Dodoma huwa haitoshi sembuse tuhamishe Ikulu msururu wa vigogo ma mawizara na wafanyakazi wa kada mbalimbali. Mhhhh ngoja tuone hiii movie itakapo ishia.
 
Mkuu watahamia slow slow kadri miundombinu inavyoimaarishwa , lakini serikali kuhamia Dodoma italipa unafuu mkubwa jiji la Dsm na maendeleo yatakuja Kwa kasi maana foleni na misafara itakuwa imepungua sana hivyo kuharakisha utoaji huduma.
 
Hivi utabiri wa kila siku wa UKAWA ni kufeli kwa serikali, ni kweli haitafanikiwa!?
Ni bora mkawa neutralistics kuliko kutabiri upumbafu na kujidai eti... Time will tell..
Ombeeni taifa lenu nyumbu nyie
 
Hivi utabiri wa kila siku wa UKAWA ni kufeli kwa serikali, ni kweli haitafanikiwa!?
Ni bora mkawa neutralistics kuliko kutabiri upumbafu na kujidai eti... Time will tell..
Ombeeni taifa lenu nyumbu nyie
Umesoma kwa makini nilichoandika lakini? Au umekurupuka tuu?
 
Ni yupi uliyemsikia akipinga serikali kuhamia Dodoma??..yani MTU atekeleze ahadi za CHADEMA alafu wanachadema wampinge??
 
Subiri utasikia mwingine anasema atahamia kesho...
Ni kushindania matamko tu
 
Jiji la Dsm ndilo litapata faida na unafuu mkubwa pindi serikali ikihamia Dodoma kwani moja ya kero kubwa ni misafara na foleni huku idadi ya wahamiaji ikiongezeka Kwa kasi na miundombinu ikiwa bado ni ile ile , Kila kiongozi anataka awe mkazi wa Dsm hawataki kupeleka maendeleo mikoani , huu ni mda wa kusambaza maendeleo Nchi nzima.
 
Reactions: BDN
Nachoona mimi hapa , tunahamisha matatizo sugu ya Dar na kuyapeleka Dodoma.Hakuna maandalizi makubwa hasa ya upande wa Infrastructure ya mji kwanza.Pili kuna vision ya future huko say miaka mia mbele kwa kuangalia unavyopanga mji na reserves za future expansion za barabara , reli mijini ,makazi n.k.Suala la kuhamia DOM lilisimama kitambo tu na sidhani ni busara kwa kitu kilicho dormant mnakurupuka na kwenda na spidi ya jet
 
Tanzania,na watanzania ni wapevu kimakwelikweli...! Serikali iliyochaguliwa na watanzania, inaakisi upevu wao...sasa tofauti ni kujiliwaza kwa "wafuasi", wa walioshindwa 25/12/2015!
...hakuna kukurupuka!
...serikali inahamia Idodomya kabla ya 2020, na asiefurahishwa na hilo, akale malimao!
 
Ni yupi uliyemsikia akipinga serikali kuhamia Dodoma??..yani MTU atekeleze ahadi za CHADEMA alafu wanachadema wampinge??
Ni kweli Mkuu chadema hawana kipingamizi juu ya kuhamia Dodoma kwani hata kule South Africa makao makuu ya ANC yapo Johannesburg licha ya serikali kuishi Pretoria
 
Loooooh! WaTanzania lipi jema kwetu? miaka yote tunalalamika kuwa serikali haina utashi wa kisiasa kuhamia Dodoma leo JPM amepata huo utashi badala ya kumpongeza tunalalamika wamekurupuka. Black people got problems, big problems.
 
Hebu tumia akili kidogo aisee! Hivi unaelewa maana halisi ya HARAKA IWEZEKANAVYO?

Hivi unaweza kulinganisha hiyo kauli na kinachofanywa na hawa mawaziri? Eti "MIMI WIZARA YANGU INAHAMIA DODOMA WIKI IJAYO" seriously!?
 
Wanakurupuka.ndio tatizo la kufanya kazi kwa woga.

 
Umetumia kiungo gani kufikiri? MBOWE ni Kiongozu wa CHADEMA akiongea anaongea kwa niaba ya chama chake huyu mleta amekwambia anaongea kwa niaba ya Chadema? Mijitu mingine
 
Hii awamu ya 5 ina drama nyingi bala....maamuzi ya kukurupuka....sipati picha mambo yangekuwaje kama zile chokochoko za yule manzi wa malawi zingetokea leo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…