cchrispian
Member
- May 9, 2013
- 16
- 5
Benki za simu kama M-Pesa zilianzishwa ili kiwasaidia wananchi ambao hawana uwezo wa kufungua akaunti benki au hawaishi karibu na benki kuwawezesha kuweza kutunza pesa kwa usalama na toka zianzishwe zimeongeza sana mzunguko wa fedha hasa kutoka mijini kwenda vijijini.
Kuna vijiji ambavyo hakuna benki, barabara mbovu, na inawezekana hakukuwa na umeme kwa muda mrefu. Wananchi hawa wanaitegemea teknolojia hii kwenye kupokea pesa kidogo kutoka kwa ndugu zao waliopo mijini ili iweze kuwasaidia matumizi ya kila siku. Hawa ni watu ambao wanapata shida ya kuingiza kipato.
Serikali kuongeza tozo za miamala ya simu inawaumiza watu hawa zaidi kwani mtu wa mjini anaweza kuamua kupunguza au kuacha kutumia M-Pesa na badala yake akarudi kutumia benki. Watu hawa hawawezi. Hata serikali ikitumia fedha hizo kuleta maendeleo vijijini itakuwa imeleta kwa kiwaumiza wananchi wasio na uwezo kifedha na 2025 wataona ni bora wapigie kura watu tofauti watakaoenda kuwaokoa kwenye jambo hili.
Ukizingatia wengi wanaona Serikali itaendelea kuchukua mikopo mikubwa, kuongeza posho za wanasiasa na hakutakuwa project yoyote mpya kubwa itakayosogeza maendeleo.
Maoni yangu ni kwamba serikali iongeze uwajibikaji na uwazi wa matumizi ya fedha. Ianzishe mfumo utakaowawezesha kila mwananchi kuona fedha zinatumikaje serikalini na ikiwezekana ibandike ripoti ya matumizi ya fedha (flash report) kila mwezi kwenye bao za matangazo za vijiji na halmashauri. Hii itasaidia kuongeza uaminifu wa wananchi kwa viongozi wao.