Serikali ili kuwasaidia watanzania wataalam wangerejea tena vipaumbele vyao

Ndikwega

JF-Expert Member
Feb 1, 2012
5,841
2,000
Salam!
Nianze kwa kusema, hii Nchi ya Tanzania ni Mali ya Watanzania na si Serikali iliyoko Madarakani. Kuna Kasumba ya Kuona CCM wanahaki Zaidi ya Wengine kitu ambacho ni Makosa, hivyo nitatoa maoni kama Mtanzania Mzaliwa na mwenye asili na si Mkimbizi.

Moja ya Vitu vinavyochangia Utawala wa awamu ya 5 Uchukiwe pamoja na mambo mengineyo Ila Kubwa ni hali za Wananchi wake. Hali imekuwa Mbaya kiuchumi kuliko awamu mbili zilizopita (Nimerejea awamu mbili tu).

Ni kwamba Ajira hamna, ukijaribu kufanya biashara ndogo ndogo pesa hamna, pia Ukitaka Kulima mazao tunaambiwa tuuze ndani ya nchi inamaana kwa bei Mbovu! Mbaya Zaidi, Serikali imekomaa na vitu ambavyo hata mchango wake kwa wengi hautaonekana Mara Moja. Mf Ujenzi wa Barbara za Juu Dsm, Reli ya Kisasa (SGR). Siyo mbaya, ila mchango wake utachelewa Kuonekana (Long term plan).

Sasa basi, kwavile Kuna kundi kubwa la Wasomi wamemaliza na Ajira hakuna pia swala la Tanzania ya Viwanda ni Ngojera tu maana huwezi pigia bajeti pesa ya Mfukoni kwa jirani, Serikali ilipaswa ifanye mipango mifupi na ya kati kwaajili ya Kunusuru Janga hili.

Moja: Weka Ruzuku ya Kutosha katka Pembejeo za Kilimo. Mathalani Mbolea sasa hivi ipo juu saana, bei ya Chini kilo 50 unakuta ni Kuanzia TZS.60,000/- na Kuendelea, hiyo ndiyo yeneye ruzuku kitu ambacho ni kama kichekesho fulani hivi. Ningeshauri, Serikali Ishushe angalau Kilogram 50 isizidi bei ya TZS.20,000/-, Vijana watapata morali wa kulima.

Pili: Achia Masoko ya Nje. Bidhaa zitakazozalishwa na vijana kwa jasho lao ziweze kuuzwa nje nchi (Hususani nchi jirani) ambako kutakuwa na Soko zuri. Mfano sasa hivi Wakenya wamevamia Soko la Tanzania kwa kuleta Viazi Ulaya hivi ama Mviringo ambapo vimekuja kuuwa Soko la Viazi vya Mbeya, Njombe na kwingineko maana wamefanya timing.

Tatu; Kuondoa Kodi kwa Wakulima Wadogo wadogo. Natambua kuwa Rais alitoa tamko juu ya hili ila ikumbukwe bado kuna maeneo Wakulima wadogo wadogo wanasumbuliwa.

NNE; Kuwezesha Miundombinu ya Umwagiliaji. Hili litasaidia kufanya kilimo kiwe endelevu na si Kusubiria Mvua za Misimu! Peleka Wataalam huko Vijijini wakafanye hizo kazi!

Tano; Kuwakopesha hawa Vijana Mitaji midogo midogo ya Kilimo Kupitia Bank ya Kilimo. Wajikusanye Kikundi, halafu wanapewa Mkopo wa Masharti nafuu. NB; Kuweka hii Bank Dar es Salama wakati Wakulima wapo Songea napo ni kukosa Weledi.

Kwa machache hayo naamini unaweza kusaidia kundi kubwa la Vijana wanaoranda randa mtaani na huku ni graduate. Hili la Tanzania ya Viwanda litawezekana pia kama kumezalishwa Mali ghafi za Kutosha, japo naamini Viwanda havija kwa Matamko. Hivyo ningeomba tufanye lililondani ya Uwezo wetu Kwanza! Hali mtaani inatisha!

Nawasilisha.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom