Serikali ifanye hili kuhusu manabii matapeli

Paul Mchumi

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2013
Posts
1,051
Reaction score
1,284
Nimeona clip ya aliekua anajiita nabii 'kiboko ya wachawi' akitoa kejeli juu ya watanzania waliokua wanalipia kingilio cha laki tano.

Naishauri serikali kabla ya kutoa kibali cha mtu anayejiita nabii anaeponya watu,ifanye hivi:
πŸ‘‡πŸ‘‡
Imwambie nabii husika aende kuwaponya wagonjwa mahututi hospitali na ikibainika kuna wagonjwa kadhaa wamepona basi nabii husika apewe kibali.

Haiwezekani mtu anachukua pesa za watu kwa gia ya imani kumbe ni tapeli wa kutupwa.

Kuna namna Serikali ifanye kuwadhibiti hawa manabii.
I stand to be corrected
 
Serikali ipi ss hiiya CCM ambayo n matapelii tu km kiboko ya wachawii....


N watu tu kujitambuaaa wenyewe tu km ww ulivyojitambua na kukaa nao mbalii na kutokuwapa hata sekunde yakuwasikiliza au kufungamana nao Kwa chcht ,tuone watamtapeli nani tenaa tukiwatengaa
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ tena hao wagonjwa wawe wanaofahamika vizuri, Coz hawachelewi kutuletea wagonjwa fake wa mchongoπŸ˜‚ kama wale waliokua wanashuhudia ndugu zao kufufuliwa na lile tapeli. Zile familia zilizoshuhudia wakamatwe wazima wazima watumbukizwe kwenye mapipa ya Acid 😏😏😏
 
Asilimia kubwa ya madhehebu ya kikristo hawana tofauti na TRA katika kukusanya fedha za waumini.
Kuna baadhi ya michango mnachangishwa kwa kushinikizwa. Mtu ukitaka kubatiza mwanao au kufunga ndoa unaulizwa kama umeshalipa michango fulani na Dhaka. Kama hujalipa hupewi huduma.
Kuna dhehebu fulani kongwe ukitaka maombi yako yasomwe Jumapili fulani kanisani inabidi ulipie. Sasa kuna tofauti gani na hawa manabii feki. Wengine wanatishia hata kutoendesha ibada ya maziko kwa watu ambayo hawatoi michango kanisani. Kiufupi viongozi wa makanisa ya kikristo wamekuwa watu wa kupenda fedha kuliko kueneza na kufundisha Imani.
 
Acha watu wafanye biashara.

Biashara za watu ziheshimiwe.
 
Ushawahi ona nabii mtume amijipeleka sehemu kama muhimbili, mwananyamala,bugaboo,dodoma general hospital akawaponye wagonjwa au kufufua maiti πŸ˜„

Ova
 
Kuwe na board maalum kuregulate haya mambo.
Hivi Kuna bodi gani hadi sasa imefanikiwa kwa chochote Tanzania hii,?sana sana inageuka kuwa kikundi cha ulaji na upigaji tu.
 
Namba moja wako alipeleka sadaka kwa miongoni mwa hao manabii pale kawe, I was there na ilitangazwa! sijui serikali gani unayoishauri
 
Acha wapigwe tu mpaka pale akili zao zilizoenda likizo zitakaporudi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…