Serikali haitakiwi Kubembelezwa bali kulazimishwa

Serikali haitakiwi Kubembelezwa bali kulazimishwa

Bams

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2010
Posts
19,768
Reaction score
49,949
Hakuna mwajiriwa anayempa masharti Mwajiri.

Katiba yetu hii mbaya iliyopo inatamka wazi kuwa mamlaka ya Serikali yatatoka kwa wananchi. Hii inamaanisha wazi kuwa mamlaka ya Rais yanatoka kwa wananchi.

Ujinga wetu wa kutotambua mamlaka yetu, umewafanya watawala dhalimu kuigeuza Katiba. Yaani yale mamlaka ya kikatiba waliyostahili kuwa nayo wananchi, wameyapora watawala, na kuwafanya wananchi kuwa waajiriwa wa Rais na Serikali yake. Yaani badala ya wananchi kumwelekeza Rais na Serikali namna ya kuwaongoza, Rais na Serikali yake ndio wamegeuka na kuwaamrisha wananchi namna watakavyowatawala.

Huo ni uhuni, huo ni unyang'anyi wa mamlaka ya wananchi. Ni uhuni ambao wananchi wamekubali kufanyiwa kwa sababu ya uzembe wao. Ni uhuni ambao watawala wanaufanya dhidi ya wananchi baada ya kuwaona wananchi ni watu wasiojitambua.

Wananchi wamekuwa kama mwajiri ambaye mfanyakazi wake kwanza anaiba pen, anamwacha; baadaye anaiba laptop anamwacha, baadaye anaiba milioni 10 anamwacha, mwishowe mwajiriwa anawafukuza hata walinzi wanaolinda hazina ili wakati wowote akitaka kuiba kusiwe na walinzi viherehere watakaotoa taarifa kwa mwajiri. Bahati mbaya, mwajiri huyu aliyeupata utajiri kwa kudra za Mwenyezi Mungu, amelala fofofo, wakati mwajiriwa asiyemwaminifu anauza mali za mwajiri kama atakavyo.

Rais na Serikali yake hawana mamlaka yoyote ya kuwaamlia wananchi namna ya kuiandalia Serikali mkataba wa ajira. Serikali inatakiwa kupewa amri ya kuandaa ukumbi, viti, vinywaji na lunch, kwaajili wakurugenzi (wananchi) siku ambapo wanataka kukutana kuandaa mkataba wa kuendesha nchi yao (katiba), ukiwemo mkataba wa ajira kwa Rais na Serikali yake.

Zile habari za kijinga za Ndumbaro eti Serikali (mwajiriwa wa wananchi) itaendesha elimu ya katiba kwa mwajiri ( wananchi) kwa miaka mitatu, ni upumbavu, uhayawani mkubwa toka kwa mwajiriwa aliyejisahau, na ni matusi kwa wananchi. Yaani mwajiriwa anasema anataka amfundishe mwajiri namna ya kumwandalia yeye mwajiriwa mkataba!! Kama siyo ukichaa wa huyu mwajiriwa aliyejaa kiburi ni nini?? Huu ujinga abakie nao Ndumbaro na wenzake.

Wananchi kupitia majukwaa yetu mbalimbali, tuanze kuandaa utaratibu wa namna tutakavyoielekeza Serikali ya Rais Samia, maandalizi inayotakiwa kuyafanya kwaajiki ya kuwezesha sisi waajiri wake kukutana na kupanga utaratibu wa kufikia hatima ya upatikanaji wa katiba mpya.

Kwenye hili Serikali haitakiwi kuombwa, kubembelezwa wala kupigiwa magoti. Inatakiwa kuelekezwa na kulazimishwa. Mwajiriwa ameonekana ana dhamira chafu ya kuzuia katiba mpya kwa sababu makosa aliyoyafanya mwajiri kwenye mkataba wa awali yamempa nafasi kubwa mwajiriwa ya kujifanyia chochote anachotaka, ikiwemo hata kumwua mwajiri wake. Kama mwajiriwa huyu anaonesha kiburi na dharau kwa mwajiri wake (wananchi), hastahili kuonewa aibu au huruma, anastahili kufukuzwa kwa aibu.

Wananchi tuungane, tuilazimishe Serikali kuandaa mazingira yatakayotumika wananchi kupata katiba yao mpya. Kuibembeleza Serikali katika upatikanaji wa katiba mpya, ni wananchi kukosa kufahamu mamlaka yao makubwa waliyo nayo juu ya Serikali walioiajiri.
 
Kabisa!!

 
Hakuna mwajiriwa anayempa masharti Mwajiri.

Katiba yetu hii mbaya iliyopo inatamka wazi kuwa mamlaka ya Serikali yatatoka kwa wananchi. Hii inamaanisha wazi kuwa wa katiba mpya, ni wananchi kukosa kufahamu mamlaka yao makubwa waliyo nayo juu ya Serikali walioiajiri.
Kinyago kilichochongwa na wananchi wenyewe pale kinapogeuka kuwa kitisho kikubwa sana kwao kwa mamlaka makubwa waliyokipa wao wenyewe.
 
Mkurugenzi wa kampuni anawavimbia wana hisa ni jambo la kushangaza sana
 
Hakuna mwajiriwa anayempa masharti Mwajiri.

Katiba yetu hii mbaya iliyopo inatamka wazi kuwa mamlaka ya Serikali yatatoka kwa wananchi. Hii inamaanisha wazi kuwa mamlaka ya Rais yanatoka kwa wananchi.
Umesema, ila kama kuna taasisi ya kulaumiwa kwenye hili ni bunge. Bunge ndo linawakilisha wananchi. Bunge ndo hutunga katiba na sheria nyingine; kwenye hili bunge ndo lililotunga katiba na likatunga sheria likampa rais mamlaka ya kuendesha serikali ama moja kwa moja au kupitia wawakilishi (mawaziri, makatibu wakuu, makamshna na wengine). Ingependeza ungeligusia hili.

Hili la kuilazimisha serikali ni sawa ila tungeona akina Bams wanaanza, lakini hawafanyi kwani ni waoga. Ni vema maneno yakafuatiwa na vitendo.

Kuhusu bunge la katiba na madai ya kwamba kwanza elimu itolewe ni kweli inaudhi na kuwafanya wananchi ni mbumbulkn je, akina Bams mbona wamejifungia ndani na wamebaki kuwa waandishi wa riwaya tu?.

Ushauri: Jitokezeni mufanye, muonekane na wananchi wakufuateni/tukufuateni ila tujitayarishe na matokeo ya matendo yetu. Ikiwa hamuelewi waulizeni wale mnaowaita wala urojo, kwani wao si haba wamehitimu ktk hili.

Kukosa kufanya hivyo, nikwambie tu utaendelea hivyohivyo kwani Waswahili husema " kelele za mlangoni hazimzuii mwenye nyumba kulala.
 
Mapambano ni Serikali ya SAMIA au mkakati wa kudumu dhidi ya kiongozi yeyote atakayeshika madaraka/utawala?
 
Hakuna mwajiriwa anayempa masharti Mwajiri.

Katiba yetu hii mbaya iliyopo inatamka wazi kuwa mamlaka ya Serikali yatatoka kwa wananchi. Hii inamaanisha wazi kuwa mamlaka ya Rais yanatoka kwa wananchi.

Ujinga wetu wa kutotambua mamlaka yetu, umewafanya watawala dhalimu kuigeuza Katiba. Yaani yale mamlaka ya kikatiba waliyostahili kuwa nayo wananchi, wameyapora watawala, na kuwafanya wananchi kuwa waajiriwa wa Rais na
Serikali ni ya kunyenyekewa, kubembelezwa na kuabudiwa" in uvccm's voice!!!
 
Mapambano ni Serikali ya SAMIA au mkakati wa kudumu dhidi ya kiongozi yeyote atakayeshika madaraka/utawala?
Haya si mapambano ila ndivyo nchi za wanaojitambua zinavyoendeshwa, mfano Kenya serikali haibembelezwi na kwa ujinga wetu tunasema eti Kenya kuna vurugu!
 
Haya si mapambano ila ndivyo nchi za wanaojitambua zinavyoendeshwa, mfano Kenya serikali haibembelezwi na kwa ujinga wetu tunasema eti Kenya kuna vurugu!
Vurugu na mapambano ni vitu viwili tofauti.

Au nimekosea?
 
Mimi niondoe kwenye hilo kundi la wananchi unaotaka waasi dhidi ya serikali
 
Tumemwacha mwajiriwa afanye anachotaka! Hili ni kosa kubwa sisi waajiri tumelifanya. Lazima tuweke mkakati wa kufuta ajira yake mara Moja! Mkakati namba 1 ni kuandaa mkataba na mwajiriwa mwingine, no way!
 
Back
Top Bottom