Series (same time same place tomorrow)

Series (same time same place tomorrow)

Herymiller

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2018
Posts
613
Reaction score
861
STORY: MANOEUVRE (MANUVA)

MTUNZI: HERY_MILLER

SEASON 01E01

Baada ya purukushani na hekaheka za mapumziko ya mwisho wa wiki ndani ya jiji la Dar es salaam hatimaye majogoo yaliwika kuashiria ni siku mpya, ambayo haipendwi kiivyo na asilimia kubwa ya watu inaitwa jumatatu, tukiacha na utani jamani jumatatu inaboa haijalishi we ni nani, una cheo gani, jumapili ulikua kanisani,nyumbani na familia au maeneo ya starehe kama watoto wa mjini wenyewe wanavyosema "kula bata".

Alarm ilisikika masikioni mwa kijana mmoja mtanashati,bila kupoteza muda aliamka kitandani nakuelekea kwenye chumba chake maalumu cha mazoezi,kama kawaida ya vijana wa kileo alichukua simu yake na kupitia maeneo muhimu ku like,comment na kujibu ujumbe wa maandishi katika mitandao ya kijamii facebook,twitter na Instagram.

Mguu wa kiume uliingia ndani ya airmax na kupendeza kiroho mbaya, wakati ule upaja uliojikatakata ulivaliwa na bukta fupi kidogo na kumfanya aonekane shupavu kwa jinsi misuli yake ilivyo inyanyasa bukta ile, kile kifua kilicho jigawa katikati na kujaaliwa misuli iliyo nyumbulika na kutengeneza matuta madogo madogo juu ya tumbo (six packs) ukijumlisha na mbavu nene zilizo beba kifua hicho zilikaa kwenye vest moja maridadi iliyokua na maandishi haya "Chicago bull's "na kuifanya mikono ya yake iweze kuwa huru kufanya shughuli zake kikamilifu.

Aliwasha redio na kucheza mtiririko wa nyimbo zake tano(playlist) ambazo hupenda kazisikiliza akiwa anafanya mazoezi( Lituation-fabulous,Many men-50,like a boy-ciara,Dirty off ur shoulder -jay z,Topback- T.I)

Mashine ya kukimbilia ilisoma kilomita 1.5 ndipo alipohamia kwenye pushup 150 akamalizia na squash 70 kabla ya ya kunyanyua chuma mara 100 kwa mikupuo 10.
Kijasho chembamba kilimchurizika mtoto wakiume taaratibu alielekea bafuni kuoga, kutokana na uzito wa siku ile katika maisha yake ya kazi ilibidi awe nadhifu kuliko kawida, ilikuwa hamna namna ndipo alipoamua chukua suti(black label) iliyotengenezwa na mbunifu nguli wa mitindo ya mavazi hapa mjini kwa sasa @ mtani_ be _spoken, chini alivalia travota ya kisigino kifupi inayofungwa kwa zipu pembeni aliyo inunua pale@born 2 shine, Pete yenye mng'aro hatari wa dhahabu kidoleni ,kidani cha madini ya tanzanite(bleclet) mkono wa kulia wakati mkono wa kushoto uling'arshwa na saa yenye rangi ya dhahabu(g-shok), laiti kama kile kioo kingeweza kusema basi kingeomba msamaha maana taswira ya mtu aliyekua anakitumai alikua amependeza kupita jinsi ambayo naweza kukusimulia.

Alipomaliza kujiandaa aliingia kwenye gari lake tayari kwa kuelekea kazini huku moyo ukimdunda dunda kwa sababu alikua anakwenda kwenye kikao ambacho mawazo yake yeye binafsi yanaweza kuja kuathiri maisha ya watu wanao mzunguka na shirika kwa ujumla.
"Deutsche mark" ni jina la shirika la kimataifa lililo anzishwa nchini ujerumani na kufungua matawi katika nchi mbalimbali ulimwenguni,shirika linajishughulisha na kuhifadhi nyara za kihistoria za utawala wa kijerumani kipindi cha ukoloni na kufanya utafiti wambo ya kale,hayo yote yanafanyika chini ya mwamvuli wa sheria ushirikiano wa kimataifa ya umoja wa mataifa.
Majira ya saa mbili asubuhi ndani ukumbi wa mikutano ya ofisi,watu walianza kuingia na kuchua nafasi zao wakisubiri kinacho endelea, nyuso za sitofahamu na bashasha ziliendelea kukinzana mbele ya mapaji ya nyuso zao hatimaye muda uliwadia mkurugenzi aliingia na kuchukua nafasi yake na kikao kikaanza rasmi.
Baada ya salamu na kila mtu kujitambulisha mkurugenzi alitakiwa kuwasilisha mada ili ijadiliwe na kutafutiwa ufumbuzi
"Kwa majina naitwa Herman muller mkurugenzi wa shirika hili hapa nchini Tanzania, nawaombeni mtege masikio yenu vizuri na mnisikilize sio muishie kunitumbulia macho tu (hahahahahahaha) alicheka kidogo, najua leo nimependeza sana ninawashukuru kwa kunisifia pia asante sana naomba niwasilishe mada kama ifuatavyo……
Baada ya mkutano wa berlin (1884-85) Africa mashariki ilikua chini ya utawala wa wajerumani ilitawaliwa kwa mfumo wa majimbo, kuimarisha mfumo wa utawala kila gavana alipewa jimbo lake la kuliongoza, tukirudi nyuma zaidi kabla ya mkutano wa berln ulifanyika utafiti(survey)kwa ajili ya kukagua na kupima maeneo yenye rasilimali ndani ya afrika ili itengenezwe ramani ambayo ingeonyesha maeneo yote, mipaka na rasilimali zake ndani ya africa. Ramani hyo ilipewa jina la skelett,kila nchi tawala ilipewa skelett yake. Baada ya wajerumani kupewa skelett yao waliamua kupunguza hatari ya kuweka mayai yote katika kapu moja(risk) kwa kutengeneza ramani nyingine ambazo zinaonyesha kila jimbo pekeyake na gavana wa jimbo ndiye aliyepewa mamlaka ya kuilinda na kuhifadhi, ili kuhakikisha siri inaendelea kuwepo wote waliousika kutengeneza ramani za majimbo waliuwa na ramani zikabaki mikononi mwa magavana, ziliandaliwa karatasi maalum za kuchorea ramani kwa ustadi wa hali ya juu waliweza kutengeneza picha ambayo inayesha sura ya gavana wa jimbo husika lakini picha ikielekezwa kwenye mwanga inaonyesha ramani ya jimbo.

Baada ya ujerumani na washirika wake kushindwa katika vita ya kwanza ya dunia makoloni yake yalichukuliwa na waingereza, kila gavana wa kijerumani ambaye hakufanikiwa kuirudisha ramani berln aliificha alipoona panafaa.………
Herman baada ya kumaliza kusoma alichokiandaa alikunywa glasi moja ya maji huku akiwaangalia wafanyakazi wake waliokuwa wanamsikiliza kwa makini, kabla haja endelea mlango ulifunguliwa na aliingia binti mbichiiiiii aliyekuwa amependeza na kuvalia viwalo vya hatari guu la shampeni ndani ya mchuchumio wa rangi nyekundu(high hills),mini sketi nyeusi ilionyesha sentimita kiduchu za upaja mtamu unao anza kuichora figa iliyo unganishwa na nyonga iliyoifanya sketi ivimbe kama mimba ya panya, zigoo sasa kajaaliwaa mashalaaaah lakini sio sana maana sana inaboa,juu alivaa kikoti cha suti za kiofisi ambacho kwa mbele ilivaliwa na skafu kuziba uwazi uliokua unasababisha sehemu kubwa ya utamu wa vifuu vya nazi kuonekana na kuzidisha gharika na kuwatoa udenda vidude, hatua kadhaa za madaha hatimaye mtoto mzuri alikaa kwenye kiti ………
"binti jitambulishe na utueleze kwanini umechelewa kwenye kikao muhimu cha kampuni "Herman akiongea maneno hayo kwa sauti ya ukali kidogo
"kwa majina naitwa gwantwa nyakababi ni mwajiliwa mpya wa shirika hili pia mtaalam wa lugha na alama zinazotumika katika mawasilano ya lugha,naongea kiswahili,kiingereza, kifaransa kijerumani,kirusi na kiitaliano kwa ufasaha, kichina na lugha zingine za mashariki ya mbali nazifahamu lakini sio vizuri sana bado nazifanyia kazi na kuhusu kuchelewa hapa ni katikati ya mji kunafoleni sana naomba msamaha naombeni mnisamehe"
"binti unaitwa gwantwa sio kila sehemu kuna sheria zake hivyo basi tuache tumalizie kikao chetu siku nyingine kukiwa hakuna foleni ukiwahi kufika mapema tutajumuika pamoja"

Kinyonge kabisa binti wa watu alitoka nje ya ukumbi wa mkutano akiwa hana raha hata chembe huku akieleke ofisini kwake kuendele na shughuli zake za kila siku.
"kama tulivyo kubaliana kuwa shirika letu litaendeshwa kwa misingi ya sheria tulizo jiwekea,
Haya tuachana na hayo turudi kwenye mada yetu, kwa gharama yoyote ile inabidi tuzipate hizo ramani(skelett) ilituweze kutimiza malengo tulio jiwekea kila mtu atumie uwezo na nafasi aliyonayo ilituweze kupata taarifa sahihi kabla ya kuanzisha oparesheni(field mission) kutona na unyeti wa suala tunalolifanya kwa sasa wafanyakazi wote ambao wanahusika katika mpango huu hatatumia tena mfumo wa mawasiliano ya kawaida badala yake watatumia mfumo mpya unaoitwa enigma toleo la teknolojia mpya ukiachana na ule ulichakachuliwa na Alan Turing wakati ya vita kuu ya pili ya dunia, hiyo yote ni kwa sababu ya kulinda usalama wetu na sifa ya shirika kwa ujumla naamini kila mtu amenielewa leo sihitaji maswali natoa siku tano tuu natakila mtu awe na majibu yanayo eleweka na ushahidi wa kile anacho kieleza"

Aliongena kiingereza ili kuonyesha msisitizo kidogo kabla hajawarusuhu waende
"our primary target is to secure the skelett and I don't think if we have other alternative than to put all our assets on play..."
asanteni sana kwa kunisikiliza mnaweza kwenda sasa.
………Itaendelea usikose......
 
STORY:MANOEUVRE (MANUVA)
MTUNZI:HERY_MILLER
SEHEMU YA 2

Kikao kilimalizika na watu walianza kusambaratika kuelekea maeneo ya kazi,kila mfanyakazi alipewa namba ambazo atazitumia katika kufanya mawasilano kwa kutumia mfumo wa enigma.

Tangazo la kutafuta ramani (skelett) ndio jambo lililopewa kipaumbele na kila mfanyakazi hivyo basi kila mfanyakazi alitumia ujuzi na maarifa aliyokuwanayo kuhakikisha zoezi linakamilika katika muda mfupi.
Big tunchii mtaalamu wa mambo ya upekuzi wa mitandao (hucker) baada ya kama masaa mawili kasoro hivi aliweza kugundua baadhi ya nyaraka za siri kwenye mitandao mbalimbali zilizonyesha mfano wa ramani(skelett) wanazo zitafuta lakini kwa bahati mbaya hakuweza kuelewa lugha iliyoandikwa ila tu aliweza kujua nyaraka hizo zilipatikana makumbusho ya taifa.

Bila ya kupoteza muda Big tunchii alimpigia simu Gwantwa aje kumsaidia kusoma ile lugha ili wajue inamanisha nini, simu ilipokekelewa
"hallow naongea nani tafadhali"
"big tunchii hapa wa cyber command unit nakuomba uje haraka iwezekavyo kuna jambo la muhimu kupita maelezo"
"mhhhhh mbona unanitisha? haya nakuja"
"uje sasa hivi"
"ok am coming "
Kijasho chembamba kilianza kumtoka mtoto wa kike moja haikai mbili haikai kutokana na boko alilolito asubuhi alihisi ni barua ya kufukuzwa kazi au anaenda kupewa adhabu huku akitetemeka kidogo alianza kwenda kusikiliza wito.
"ohhhhh gwantwa mambo vipi mtoto mzuri "
"poa tu za kwako"
"niko poa ……Umependeza "
"asante"
"sasaa kuna kazi hapa naomba unisaidie kutafsiri haya maandishi ilitukamilishe kazi mapema " big tuchii aliongea maneno hayo akimshika mkono Gwantwa huku akimuonesha maandishi hayo yaliyokuwa yanaoneka kwenye kompyuta.
"jamani hicho ni kijerumani maneno hayo yanasema kwamba ni bandari kuu ya mashariki, halafu kuna maneno siyaelewi ila nahisi yanaleta neno bagamoyo" kabla jahamaliza big tunchii alidakia
"bagamoyo ndio ilikuwa bandari kubwa Tanzania kwa kipindi hicho basi ngoja tuwajulishe na wenzetu tulipofikia ilitujue tunafanyaje au unasemaje mchumba"
"mchumba tena!!! ila poa tuu naomba uniachie hizo data nikazifanyie kazi" gwanta aliongea maneno hayo huku akielekea mlangoni alipogeuka nyuma alimuona big tunchiii katumbua macho mithili ya mjusi aliyebanwa na mlango
"weee tuchii vp unaumwaa"big alishtuka na kukijibu haraka haraka
"hapana"
"vp sasa mbona umeduwaa haya npe hyo flash basi niende" big tunchii ilibidi ampe tu gwantwa flash aende zake.
Kwa jinsi gwantwa alivyofungashia hakuna ambaye angemlaumu big tunchii namna alivyokua anajitukana kimoyo moyo.

Bila kupoteza muda Big tunchiii alielekea ofisini kwa bosi kupeleka taarifa alizozipata katika upekuzi wake,alipofika walisalimiana na alianza kumuelezea alichokipata hadi alipoishia na anchofikira kwa kutumia uzoefu alikuanao
"umejitahidi sana kama sio kumaliza kila kitu kabisa umesema ulikua na gwantwa wakati unafanya kazi hii sio" Herman alimuuliza big tunchiii.
"ndio mkuu ilibidi nimshirikishe kwa sababu sikua naelewa kijerumani"
"basi sawa unaweza kwenda "
"nashukuru mkuu" big tunchiii alitoka ofisini kwa bosi na kuelekea ofisini kwake....

Alipopata taarifa hizo Herman alifikria kwa dakika kadhaa kabla hajachukua maamuzii,alipoona amejiridhisha alinyanyua simu na kupiga
" rogers mambo vp? kimya sana "
"poa tu… mbona nipo bosii ! "
"baby amekuficha nini au ushaopoa mshangaziii"
"hamna si unajua tena bata mzee……nipe michakato"
"una dakika 20 tukutane makumbusho ya taifa kuna safari nataka twende leo ……mnyama si yupo sawa usisahau na vifaa vya kazi,zana zote ujenazo"
"natokea hapo sasa hivi"
"usichelewe " Herman alimsisitizia rogers ili kila kitu kiende vizuri.
Alipokata simu ya rogers alitoka nje ya ofisi yake na kuacha maagizo kwa karani wake ampigie simu CANDICE MILLINGA na amwambie anahitajika ofisini kesho mapema sana asubuhi.
Roger Paul kijana wa mjini anayesifika ka kuendesha magari kwa spidi lakini yupo makini sana japukua anaonekana legelege wenenye wanamuita traspota ama Powoka,alikua ameshafika makumbusho ya taifa akimsubiri bosi wake ……Herman alifika katika muda muafaka na akaingia ndani na kuanza kutafuta mfano wa ramani (skelett) aliyoiona kwenye mtandao, alipoipata hakupoteza muda akamfuata muhisika na kumuomba maelezo ya ile ramani
"hii ramani ni mfano wa ramani zilizo tengenezwa na wajerumani zikionyesha maeneo na vitu mbalimbali "alisema huyo jamaa baada kuulizwa na Herman
"ipo hii tu au kuna na nyingine "
"kwa hapa ipo hii moja tu ila inavyosemekana ramani nyingi za wajerumani zilifichawa kaole bagamoyo kwenye makaburi matupu bila miili sina uhakika sana labda ukaulize mwenyewe "
"asante sana ushauri wako ntaufanyia kazi....sisi wamoja bwana hizi ndio kazi zinazo tuweka mjini"alisema hivyo huku akitoka mbiombio kuelekea nje alipo muacha roger ili waanze safari ya bagamoyo.

Ndani ya gari ndogo ya rangi nyeusi aina ya AUDI Herman na rogers walianza safari ya kuutafuta mji wa bagamoyo iliwaweze kuhakikisha taarifa walizozipata
"kitambo ndugu yangu usalama upo "
"mungu anasaidia ila leo nakutegemea wewe nataka tufawaihi kufika ikiwezekana iwe chini ya saa saba mchana sii inawezekana!!"
" wewe tu mimi nanyoosha mguu si unaona chombo kinateleza tu kwanye lami bossi"
" huo ndio uanaume usisahau tunakufa mara moja tuu kuwa makini barabarani "
"usiwaze mkuu"
" nipe flash nisilize mziki kidogo"
Herman alichukua flash na kupiga nyimbo anazozipenda akiwa safarini , zilizoanza kumpa mizuka dereva wake na kumfanya aanze kuongeza mwendo kidogo kidogo.
Mitikisiko ya simu ya mkononi (vibration) ilimshitua kutoka usingizini alipofumbua macho aligundua wapo maeneo ya bunju, ndipo alipopokea simu
"hallooo"
"hallooo…… bosi nimeonge na candice millinga amesema hawezi kuja kazini kesho kwa sababu likizo yake haijaisha"
"mwambie kama hataki kazi na asije"
"sawa ntamwabia kama ulivyoniagiza bosi"
"mwambie sina utani na mtoto wa mtu katika hili"alikata simu na kuangalia mbele hakuamini alichokua anakiona gari ilkua inakimbia kwa spidi ya kilomita 150 kwa saa hakutaka kumshitua dereva Wake alichokifanya aliongeza sauti ya mziki tu na kuendelea na usingizi wake.

Majira ya saa saba kasoro mchana aliposhtuka walikua wanaingia kaole bagamoyo sehemu walio elekezwa kuwa kuna uwezekano wa kuzipata ramani(skelett), walishuka kwenye gari na kuafuta mwenyeji kama wanavyofanya watu wote wanaoenda kutalii katika eneo hilo.
"dada unaweza ukatuonyesha makaburi ya wajerumani katika maeneo haya na kutupa historia yake kidogo" aliuliza Herman
"haaa poleni jamani makaburi hayapo hapa yapo karibu na mjini nyuma ya jumba la dhahabu karibu na mti waliokua wananyongewa wahalifu"
" ni mbali sana "
"hapana msiogope hamja potea sana"
" ilitusipotee unaweza kutupeleka"
"haina tatizo mteja ni mfalme kwetu" baada ya kusikia maneno hayo waleelekea walipo egesha gari la na kuondoka kuelekea walipoelekezwa
Walipokua ndani ya gari Herman alianza kumuuliza maswali yule dada
"samahani dada unaitwa nani kama hutojali"
"Naitwa Nuru"
"Nuru ya mwanga sio(huku akitabasamu kidogo) mimi naitwa Herman muwakilishi ya shirika la mambo ya kale la ujerumani linaitwa Deutsche mark "
"nashukuru kukufahamu"
"nasikia kuna makaburi yalitengezwa na kufukiwa vitu vingine badala ya miili. "
" Ndio inavyosemekana "
"wewe kwa mtazamo na uzoefu wako unaonaje"
"ni kweli nimeshawahi kushuhudia wakifukua aina fulani ya picha za kuchora na kwa jinsi walivyokuwa makini zinaoneka zilikua zamuhimu kwao"
" pichaaa?ilikua picha ya nini na ilikua kwenye kaburi la nani"
"wanasema lilikua kaburi la askari mtiifu"Nuru alisema hayo akionyesha wazi alikua haamini anachokizungumza…walikua wameshafika eneo la tukio walishuka kwenye gari na kuelekea bondeni ambako kwa mbaliii bahari ya hindi ilikua inaonekana.

Baada ya Nuru kuwazungusha hapa na pale na kuwapa historia ya yale makaburi Herman aligundua kwamba kuna kaburi moja halija fukuliwa wala kufanyiwa matengenezo
"Nuru mbona hililiko tofauti na mengine"
"sijui nikuelezee vipi ila ni kwamba wanavyosema hilo halichimbiki kwani linalindwa kwa nguvu za giza"
"heee nguvu za giza kivipi na kwanini kaburi hili tu" rogers aliuliza kwa mshangao?
" walio uliza swali kama lako ni wengi ila wachache wadadisi zaidi na waliotaka kujua ndani kuna nini walikutwa wamekufa na maiti zao zilikutwa zikielea baharini"
" mhhhhh mbona unatutisha Nuru"
"hapana siwatishi ila huo ndio ukweli wenyewe "
"kwa hiyo hizo ramani zilipelekwa wapi"aliuliza rogers
"zipo kwenye kanisa la wa mishenari wa kanisa katoliki jimboni hapa" baada ya kusikia jibu hilo bila kupoteza muda Herman alimwambia Nuru awapeleke,basi walingia ndani ya gari lao na kuanza kuelekea kanisani.

Ilikua saa nane mchana kipindi cha xxl ya clauzi fm na( b kumi na mbili) ngoma za town(na dj ziiro) ndio kilikua kinatesa spika za gari aina ya AUDI likichapa mwendo kuelekea kanisani. Kwa vile Nuru alikua mwenyeji walikenda moja kwa moja hadi zilipkuwa zimebandikwa zile ramani
"ni hizi hapa"
" ni kweli zinastahili kulindwa na kutunzwaa"huku ajitikisa kichwa Herman alimjibu Nuru
"naruhusiwa kupiga picha"
"unaruhusiwa"baada yakusikia hivyo Herman alimwabia rogers apige picha zile ramani
Kabla hajamaliza kupiga picha ramani zote alikuja mzee mmoja amabeye yeye ndiye muhusika wa zile ramani,Nuru aliwatambulisha jina la mzee huyo kuwa anaitwa Ngindo baada yakupiga nae stori mbili tatu yule mzee akawa anondoka
"mzee Ngindo nisubiri kidogo "
Herman alimfuata wakaanza kuteta kidogo
"samahani mzee ukiacha ramani hizi kuna ramani zingine za utawala wa kijerumani unazozifahamu"
"ndio lakini ni mambo ya siri kidogo"
"wanasema penye udhia unapenenyeza rupia"
"hahahahahahaha unamaanisha upo tayari kuacha mbachao kwa msala upitao kijana"
"kama natakiwa nifate nyuki nile asali nadhani sina cha kupoteza"
Ndipo Herman alimpomweleza mzee Ngindo mpamgo wake nakumuuliza kiasi cha pesa anayotaka
"hapo sasa shuzi limepata mjambaji nnataarifa unazotaka lakini tutaaminianaje sasa"
"pesa ndio kila kitu nadhani hakuna kitakacho shindikana" basi alienda nae kwenye gari kumalizana nae, alimlipa hela aliyotaka na kusikiliza atakacho ongea
"asante sana ila tu mambo yakibuma tusijuane… ni hivi ramani unazozitaja imebaki moja ya tuu na ipo tosamaganga kanisani Iringa ila hajulikani iko sehemu gani? wengine wanasema ipo kwenye kaburi la askofu wa kwanza aliyezikwa ndani ya kanisa na wengine wanasema ipo chini ya meza ya altare madhabauni." mzee Ngindo aliongea maneno hayo huku wakitoka nje ya gari na Herman.

Aliwakuta rogers na Nuru wanapiga stori akajumuika nao, akawaambia kuwa amemalizana na mzee Ngindo hivyo inabidi waanze safarii ya kurudi mjini alifugua pochi yake na kumlipa ujira wake Nuru na kumuliza rogers kama amemaliza kupiga picha.

Walimrudisha Nuru kaole na walianza safari yao ya kurudi mjini Dar es salaam Herman alichukua camera na kuamishia picha kwenye simu yake na kumtumia bi tuchii kisha akampigia simu
"sema tunchii fungua enigma kwenye akaunti yako nimekutumia picha ziweke kwenye database yetu huonekama kuna picha kama hizo zinafanana nazo unijulishe kabla ya nusu saa"
"sawa mkuu" big tunchiii alijibu
Alipomaliza kuongea na tunchii alimpigia candice millinga
"hallooo bosii "
"habari za siku nyingi"
"salama tu sijui wewe"
" huku sio salama kila kitu kipo kwenye akaunti yako ila kesho asubuhi tukutane uwanja wa ndege tunaenda kwenye misheni Iringa "
"sawa saa ngapi sasa"
"kila kitu kita kuwepo kwenye akaunti yako enigma baada ya nusu saa"
Alikata simu na kushusha pumzi kisha akatulia akimuangalia rogers akiwa afanya shughuli zake barabarani
"bosii vp mbona umetulia ghafla " aliuliza rogers
"naifikiria misheni ya kesho"alijibu kinyongeee
Simu ya mkononi ilianza kuita akaipokea
"hallooo "
"big tunchii hapa… picha ulizonitumia zinafana na picha fulani nimejaribu kutafuta eneo lake wakasema ni Iringa sijaweza kugundua eneo moja kwa moja"
"kazi nzuri…… nimekutumia utaratibu wa shughuli za kesho andaa ratiba na ticket za safari tukutane kesho asubuhi uwanja wa ndege"
"sawa mkuu tukutane kesho " alikata simu na kumuambia rogers.
"kaka kunjua goti tuwahi maana kesho ni siku ndefu"

Baaada ya kusikia hivyo roger akawa anafanya yake tuu laiti ungeliona gari lao lilivyokua linakimbia ungesema labda wanawahi ndege au mamilioni ya pesa.
Mapena asubuhi siku iliyofuata watu wanne walikutana uwanja wa ndege tayari kwa kuelekea Iringa, candice millinga mwanadada mwenye umbo la kimisi mrefu na sura ya kuvutia lakini yupo tofauti kabisa na uzuri wake kwani yeye ni muuaji wa kukodiwa(recruited assassin) na ndiyo kazi inayomuweka mjini amesha watoa roho watu maarufu wengi sana ndani na nje ya nchii,alipitia mafunzo ya kijeshi nchini Korea alipokuwa masomoni na baadaye alipata uzoefu baada ya kufanya michezo michafu maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi.
Big tunchii,rogers, candice na Hermani walipanda ndege saa mbili asubuhi kuelekea Iringa, wakiwa angani kila mtu aliwaza lake ndipo candice alipomuuliza Herman
"hivi we ni raia wa nchi gani maana baba yako ni mjerumani na mama mswahili na umekulia nchi zote mbili"
"sasa candy siumesha jijibu mwenyewe mimi raia wa nchi zote mbili "
"wacha wee chotara uyoo"
"Acha utoto fikiria misheni wewe"Herman aliongea hivyo ilikukatisha maongezi

Baada ya masaa mawili walikua wamesha ingia Iringa na tayari rogers alikua kwenye uskani tayari kuelekea tosamaganga kanisani, big alikua sio mtu wa operasheni(field agent) kwaiyo walikua wanampa maelekezo iliasije akatoa boko,mwendo wa saa moja uliwatosha kufika eneo la tukio bila kuchelewa walianza kusoma mazingira kila mtu alikua na kazi yake, big tuchii alikua na kompyuta yake ya mkononi(tablet) aliyo iunganisha na camera inayo weza kugundua vitu vya zamani ikisetiwa katika mfumo wa X rays.Herman yeye alikua anawapanga walinzi wa kanisa na watu wilio na zamu ya kufanya usafi wafanye haraka kwani wao ni mafundi wanataka kujaribu mfumo mpya wa taa za kumulikia wakati wa ibada za usiku.Candice alikua na begi lake la Luis vuiton aliloweka bunduki aina ya AK-47 na vifaa vyake vingine kwa ajili ya kutumia nguvu kama itahitajika akiwa amevalia miwani nyeusi na mzula kuficha sura yake kiaina flani.wakati roger akichora ramani ya kutorokea mambo yakienda kombo,baada ya usafi na shughuli za kawida kuisha big tunchii na Herman waliingia na kuaanza kukagua sehemu yenye ramani wanayoitafuta, walinza na mbele ya altare Mashine haikusoma kitu wakawa wanaelekea kwenye kaburi la askofu lililo mlemle ndani ya kanisa ndipo mashine ilipoonyesha ramani waliyokuwa wanaitafuta walipo jaribu kufungua kufuli likagoma,wakamuita rogers aje na gesi ili walikate lakini ilishindikana wakawa wamebakiwa na njia moja tu ambayo ni kutafuta funguo ikiwa wamebakiwa na saa moja na nusu tu lakuendelea kubaki pale,
"jiongeze basi bossii muda unaenda "alisema big tunchii
"poa ngoja nimshitue candice afanye yake"alisema Herman huku kijasho Kikimtoka…… akampigia simu candy na kumuamuru aje na funguo kwa njia yeyote ile
Bila kupoteza muda candice aliingia kwenye chumba cha padre mkuu nakujifanya anataka kuungama padri alipoamaliaza kusali kabla hajaanza kumskiliza alichomwa sindano
"nimekuchoma sindano ya sumu baada ya dikaka tano hautakuwepo dunia nataka funguo ya kaburi kama unataka dawa ya kuondoa sumu(antidote) "

Bila kupoteza muda padrii alitoa funguo na kumpaa candy akazipeleka kwa Herman wakafungua wakachukua ramani zao na kuaanza kujiandaa kuondoka, candy alienda kumpa dawa(antidote) pandri gafla walinzi wa kanisa waliingia na kumuamuru anyooshe mikono juu kabla hawajipanga walipigwa visu vya shingo vilivyorusha gafla na candy na kuwafanya wakae chini papohapo
Alipofika nje aliwaona akina rogers wakiwa na mizigo yao wakielekea kwenye gari lakini alipotazama kushoto aliwaona walinzi waliokua na bunduki wakita kuwafuata ndipo alipofungua begi na kutoa ak-47 iliyokatwa kidigo kwa mbele na kuanza kuwamiminia risasi zilizo wajeruhi na kuwafanya wajifiche,muda wao ulionyesha wamebakiza saa noja tu ili waweza kuwahi ndege ya kurudi Dar es salaam kuona hivyo roger aliwasha gari na kilikimbiza kwa kasi hadi alipokuwa candy akapanda wakiwaacha watu wote midomo wazi. Walirudisha vifaa na gari waliloazima kwa watu wao wa wanguvu na kubaki na mizigo yao tu pamoja na (skelett),safari yakuelekea uwanja wa ndege ilianza wakiwa barabarani walisikia taarifa ya habari mpasuko kuwa majambaz yamevamia na kupora kanisani baaada ya kuwadhuru watu kadhaa wakitumia silaha za moto,baada ya kuskia hivyo walianza kuwa na mashaka hususani big tunchiii ambaye alikua siyo mtu wa michezo ya uwanjani (field agent). Walifika uwanja wa ndege na kupanda ndege tayari kwa kurudi Dar es salaam. Big tunchii alikua amshapiga picha na alikua anazichambua kugundua zikua na siri gani baada ya takribani dakika ishirini aliweza kugundua eneo lenye madini ya dhahabu yaliyofichwa katika kipindi cha utawala wa wajerumani maeneo ya Sekenkenke mkoani Singida.kabla kushuka kwenye ndege walishajua kwa mba mgodi wa Sekenkenke ulifungwa mwaka 1959 wakidai madini yame kwisha lakini kumbe sikweli ila madini yaliyobaki yalikuwa hayawezi kuchibwa kwa teknolojia iliyo kuwepo muda ule.
"jamani tumerudi salama ila kazi nduo kwanza imeanza kila mtu aifikirie Sekenkenke kwa marefu na mapana na tujianda kwa misheni ya kwenda kuchukua madini zaidi ya tani elfu tatu"
"mkuu ila bado hatujajua kwamba yapo kweli au la"aliuliza big tunchiii
"Acha uoga mtoto wa kiume mzigo utakuwepe tu"
"hii ni mesheni kubwa tutahitaji watu wa kila aina na vifaa vingi kwa maana hiyo pesa nyingi itatumika umejipangaje bosii "aliuza candy aliyekuwa kachoka mbaya utadhani mbwa aliyekimbia siku nzima
"natoa wiki moja ya kila mtu kupumzika ilimniachie mimi kazi ya kupata pesa na vifaa kabla hatujaanza misheni ya Sekenkenke " walishuka kwenye ndege mishale ya saa kumi na mbili za jioni kwa masaa ya afrika mashariki na kila mtu alielekea nyumbani kwake. Kupumzika.

Herman mawazo ya kupata pesa yalimtawala kichwani mwake na kijiuliza atazitoa wapi pesa hizo ili wakamilishe misheni ya Sekenkenke
……………Itaendelea …………
 
STORI:MANOEUVRE (MANUVA)
MTUNZI:HERY_MILLER
Sehemu ya 3

Alipoingia ndani kwake alianza kuhisi hali ya tofauti iliyomfanya atembee kwa kunyata, ilikua majira ya saa tano za usiku huku akiwa na wasiwasi kutokana na shughuli za kimafia alizozifanya siku ya hiyo Herman hakutumia mlango wa mbele badala yake alipitia dirishani alipongia ndani alichomoa bastola nakuificha kwa nyuma akiwa bado anatafakari alisikia sauti ya mziki uliokua unatokea chumbani kwake na kumfanya ausogelee mlango na kuchungulia kwenye kitundu cha kitasa, moyo wake ulilia paaaaaaa!!! Ilikua inaimba nyimbo ya wizikid (show you de money) mtoto mzuri aliyejaaliwa umbo na kiuno kama nyigu mzee alikua akiinyanyasa nyonga aliyopewa na muumba wetu bila kunchangia hata senti tano,alijitikisa kuanzia kichwa hadi kisigino heee kweli raha jipe mwenyewe unaweza ukadhani ni feni kwa jinsi mauno yalivyo kua yakimiminwa bila huruma na binti huyo wa kizaramo tokea hapo mjini mwanalumango msanga chole.

Herman baada ya kujua kuwa alipata mgeni wa kushitukiza alirudisha bastola mahali pake huku akionuesha kufurahishwa na kile alichokiaona na kujisemea kimoyomoyo
"mhhhhh kwa huu ukame nilio kuanao leo huyu mtoto zai atanikomaje"alitoka mlangoni na kuingia kwenye chumba chake cha siri kwaajili ya kutoa ripoti kwa bosi wake,aliwasha laptop na kufungua mtandao wa Skype ilikufanya mazungumzo kwa njia ya simu ya video,alimueleza kinacho endelea ndipo alipoambiwa
"sikia mwanangu hatuna muda wakupoteza nataka uandae mpango wa maandishi na gharama zote kwa ujumla halafu kesho jioni uje nyumabani ujerumani"
"sawa baba ntajitahidi nikamilshe huo mpango mapema kesho"alimjibu mzee muller na kukata simu

Alitoka taratibu na kuelekea kwanye jokofu na kuchua mvinyo na kupiga glasi mbili tatu alipogeuka alikutana uso kwa macho na Zai mtoto wa kizaramo aliyeiitawala nyumba kwa wakati huo akiwa na kinguo cha kulalia kilicho onyesha kila kitu kilicho kua kwenye mwili wake,
Zainab Habib mwana sheria wa kujitegeme wa sheria za kimataifa za biashara,baada ya kupagawishwa na michezo hatari ya Herman aliamua kuchonga mzinga kama wafanyavyo watu wote waliowahi kulamba asali
" jamani hery I miss u"kwa sauti ya kumtoa nyoka pangoni zai alimwambia Herman kabla hajajibu chochote tayari alikua amesharukiwa na kukumbatiwa na Zai na kumfanya akose cha kujibu
Kifua chake kilihisi kuchomwa na michongoma baada ya vifuu vya nazi vya Zai kumgusa mashetani yake yalimpanda ndipo alimpokamata kiuno na kuanza kumpapasa taratibu juu ya kijungu matata laini kama nyanya masalo huku juu wakibadilisha mate kwa ndimi zao mithili ya mtu anakoroga uji jikoni

"I miss u too baby "
maneno hayo yalitoka kwa tabu sana kutokana na mdomo wake kubanwa na lips za zai jogoo lake lilianza kutanua mabawa kuashiria linataka kuwika, alianza kwa kumlamba mwili mzima kuanzia kilimbero hadi uvinza na kumfanya zai atumbue macho utazani mtoa roho alikua karibu yake,bibie nae hakua nyuma alipitia azam kwa bakhresa akachukua koni na kuanza kuonyesha ufundi wake wa kuchezea kipaza sauti,alimbeba na kumewaka kwenye sofa na kumtega kwa staili ya popo kanyea mbingu kwa vile alikua kashamnyong'oshea vya kutosha alianza kuingia mgodoni na kutoka huku akichimba na sululu yake na kumfanya zai apige kelele za utamu utadhani amekabwa na jinamizi baada ya kuona mashambulzi yamekua makali mtoto wa kizaramo alichukua uskani huku akikata mauno ya taratibu kabisa na kumfanya Herman aongeee lugha asizozifahamu ghafla alianza kuiona kilimanjaro kabla hajafika kilele cha kibo au mawenzi zai alisimana na kubadilisha staili sasa alishika meza na kuinama wenyewe wanaiita mbuzi kagoma kwenda, bila kuchelewa dushelele lilitumbukia ukumbini na kuendelea kutumbuiza huku waki chekecha cheketua chekecheke mtanange ulienda kumaliziwa chumbani ambamo laiti kitanda kingeweza kusema basi kingeongea siku ile.

Asubuhi na mapema Herman aliwahi kuamka na kuanza kuandaa mpango mkakati wa kwenda kuchukua hazina ya dhahabu iliyofichwa maene ya Sekenkenke Singida, big tunchii alikua ameshakamilisha taarifa zote na kuziweka kwenye mtandao wa enigma na kuzidi kuifanya kazi kuwa rahisi, yalihitajika magari,pesa na mitambo mbalimabali ya kuchunguzia eneo wanalolitafuta pamoja n rasilimali watu wanye taaluma mbalimbali na walinzi wa kuhakikisha usalama unakuwepo alipomaliza kuandaa ripoti alirudi chumbani na kumkuta zai ndio kwanza ana amka toka usingizini

"baby umeakaje"
"nimechoka halafu mbona uko mbali "
"kuna kazi nilikua namalizia jioni nina safari ya kwenda ujerumani ndio nilikua naanda vitu vyangu vya safari"
"mhhhhh jamani hata kuniambia au ndio michepuko tena"
"hamna naenda kikazi kuna kikao naenda kuhudhuria"
"na mimi ntakua munich wikend hii naiwkilisha kampuni ya bavaria nchini kuna mambo ya kusaini mikataba"
"mikataba wapi wewe sio unaenda kwa jamaa yako unayelalamika ana kibamia"
"jamani usinifanyie hivyo naenda kikazi tuu ila anapesa kweli mungu hakupi vyote"
"achana na hao wazembe hebu nipe cha asubuhi sii unajua kilivyo kitamu(morning glory) "
"vyote vipo kwa ajili yako wala usiwe na pupa njoo ujilie utamu umejaa tele unakusubiri wewe tu"baada ya kuwashiwa taa ya kijani hakujifunga alingia uwanjani na kutembeza bakora utadhani mwalimu wa zamu shule ya msingi au sekondari.

Baada ya shoo walioga na kupata kifungua kinywa na kila mtu aluendelea na mishe mishe zake,ofisini walikuwepo rogers, candice,tunchii na gwantwa wakimsubiri Herman aje ili wajue wanafanyaje hazikupita dakika 20 alikua ameshafika na wakaanza kujadili
"ramani inaonyesha hazina ilifichwa katikati ya mgodi wa Sekenkenke na Kirondatal "alisema big tunchiii
"ruti ya ndege inachukua saa maja kutoka Dar es salaam "alisema rogers
"kwa sababu za kiusalama inabidi tulichunguze eneo na watu wake kwa miezi kadhaa kabla ya kuingia ilitusije tukajiingiza kwenye midomo ya mamba,pia tujue kama kuba timu nyingine ambayo ina mipango kama yetu na mwisho tunitaji watu wa kufanyanao kazi"alisema candice
"jioni ya leo naelekea ujerumani ambako naenda kufatilia masuala ya pesa kwa ajili ya misheni hii najua tunahitaji vitu vya teknolojia iliyoendelea kidigo hivyo naomba kila mtu aniandakie mahitaji yake na ayaweke kwenye enigma "alisema Herman,aliendelea
"naondoka leo ila kila kitu kiendelee na mawasilano yote yafanyike kwa enigma " alianza kutoka kuelekea nje
"gwantwa "Herman aliita kwa sauti ya mamlaka
"abbeeee bosi "alitika kwa woga huku amkifata bosi wake koridoni
"saa yako inasema ni saa ngapi"
"saa mbili na dakika hamsini"
"kajiandae tunaenga ujerumani leo saa tatu usiku"
"haaaa jamani bosi me ntajiandaaje muda mchache hivyo"
"kwa hiyo hutaki kwenda au!"
"hapana bosi "
"niletee passport yako sasa hivi pesa na maandalizi yako imeingizwa kwenye akaunti tiketi yako utachukua ofisi za KLM mjini"
"sawa haina shida bosi" gwantwa alitikia huku akiwa na mshituko lakini alijitahidi kuendana na mazingira.
*************************************

Munich -ujerumani
Mzee muller aliwapokea uwanja wa ndege na kuwapeleka hotelini badala ya nyumbani kwake kwa sababu za kiusalama hali ilikua sio salama ndani ya mji huo wa bavaria kutokana na uchovu wa safari walipumzika masaa kadhaa kabla hawajaanza kazi rasmi.
Ndani ya ukumbi wa mikutano walikuwepo wawekezaji mbalimbali waliokua tayari kuweka pesa zao katika mradi huo, vijana wawili yani gwantwa na Herman walijitambulisha na waliwaelezea mpango wao na changamoto zinazo wakabili, kwa vile kikao kiliuzuliwqa na watu toka mataifa mbalimbali gwantwa ilibidi awatafasirie wale waliokua hawaelewi kijerumani sana sana watu wa mataifa ya mashariki ya mbali kama wa China, Taiwan na Thailand, kwa vile ilikua ni usiku wao walitoka nje na kuwaacha wamiliki wa hisa za shirika wakijadiliana wakapanda juu kabisa ya jengo la ghorofa 40 na kutokana na hali ya hewa ya baridi wakati huo iliwabidi wasogeleane ilikupunguza baridi
"ivi unaachaje kukaa sehemu nzuri kama hii na kuamua kuishi Tanzania "gwantwa alimuuliza Herman
"mama yangu ni mtanzania unadhani sistahili kukaa Tanzania "
"sijasema hustahiili ila tu kwanini Tanzania "alisema gwantwa huku akifikicha mikono kupunguza baridi
"hujazoe baridi!!! maskini pole sana haya njoo kifuani kwangu nikupe joto" alisema Herman huku akimpapasa mgongoni na mabegani gwantwa
"haaaa mhhhh jamani bosi me naogopa "
"unaigopa nini sasa kwani una miaka mingapi'"
"25"
"haaaaaa kumbe bado mtoto mbichiiiiii kabisa wewe"

Simu iliita na walikua wanatakiwa kwenye chumba cha mkutano wakasikie majibu ya maombi yao
"naona wameamua kunipeperushia ndege wangu tunaitwa ndani mrembo" huku akitukana kimoyomoyo Herman alianzakuekea walikoitwa
Shirika lilikubali kutoa bilion mbili za kitanzania kwa ajili ya misheni hiyo na kutoa wataalamu kwa ajili ya kufanikisha mpango huo,waliambiwa wajiandae kwa safari ya kuelekea africa ya kusini kuonana na wataalamu wa mambo ya madini na operasheni yote kwa ujumla
"anaitwa van meer anakaa capetown south Africa ndio mtu aliyependekezwa na shirika kukuelekeza shughulu za madini na oparesheni zake "aliwaambia mzee muller
"ntawasiliana nae vipi sasa"
"leo twende ukapumzike na kumsalimia mama yako kidogo alafu kesho ndio utajua hayo mengine"baada ya kusikia hivyo basi akajua amesha mkosa gwantwa kwani hatoweza kumtafunia kwao.

Kesho yake walikutana standi ya treni za umeme itakayowapeleka mpaka amstredam uholanzi ambapo walipanda ndege kuelekea capetown afrika ya kusini. Walipofika walipokelewa na bwana van meer na kuwapeleka kwenye nyumba walioyo andaliwa,gwantwa alikua sio mtu wa safari ndefu za mara kwa mara hivyo alipatwa na kahoma uchwara kaliko mchosha chosha kidogo, baada y kupumzi kwa takribani siku mbili waliamza kutafuta vifaa walivyokua wanavihitaji kwa mgongo wa jina la kampuni ya kidachi inayimilikiwa na van meer kuanzia drone (ndege ndogo zisizo na rubani zinazotumika kupiga picha na kurekodi matukio mbalimbali ilikuyafanyia uchunguzi) vifaa vya kugundua kama eneo lina madini na kuangalia shughuli za uchimbaji zinavyo endeshwa huko nchini afrika kisini ndipo walipo tembelea mgodi wa kimberley na kujifunza baadhi ya mambo.Mawasilano na timu iliyopo Dar es salaam yaliendele ilikujua mipango inaindeleaje,candice alikua ameshawatafuta walinzi watakao kuwepo kwenye misheni na kuwapa mwongozo wakati big tunchii alishatafuta taarifa na vibali vyaa kufanya kazi kama kampuni ya utafiti wa madini huku rogers akiwa kasha tungeneza mpango wa kutorokea (escape plan).
Baada ya wiki nne kila kitu kilikamilika na wakianza kufanya taratibu za kurudi Tanzania katika timu mbili tofauti Herman na gwantwa walipitia Johannesburg na kupanda ndege tayari kwa kurudi Dar es salaama wakati vifaa na wataalamu wengine wakiongozwa na Mr van meer walitumia usafiri wa meli itakayoenda kutia mjini Tanga.

Wakiwa Johannesburg Herman alimuomba gwantwa wamalizie walipoishia siku ile walipokua munich ujerumani kutokana na kaukame bila hiyana gwantwa aliingia kingi lakini kwa sharti moja tu kwamba ni kwa siku hiyo tu (mechi ya kirafiki),Herman hakutaka kumpoteza mtoto wa kihaya alianza kumtembezea katelelo kwa ufundi wa hali ya juu ulio amsha ngale za gwantwa na kumfanya aanze kupiga kelele za utamu zilizomfanya azidi kusulubiwa bila huruma, Herman alimtafuna kisawasawa laiti kama yale mashuka na kitanda vingekua vinaongea tusingeamini ambayo yangesemwa navyo, wakati mchezo unaenda ukingoni alma nusura jamaa aruke ukuta kutokana na jinsi ule mkia ulivyokua unatamanisha ila tu kwa vile alikua anataka kuiona pepo basi aliachana na mawazo hayo ya kifirauni ili aende jannhatusi filidausi.

Mchana majira ya saa sita hivi walikua ndani ya ndege ya shirika la afrika kusini(south African airline) tayari kwa kurudi nyumbani Dar es salaam Tanzania
"mhhhhh sijutiii kukufahamu bosi"alisema gwantwa
"kwa nini"
"kwa ulichinifanya jana kweli wanaume mpo wachache "
"haaaa achaa utani wewe kwanini unasema hivyo"
"nilianza kuhisi nnamkosi wa kikutana na vibamia ila jana nilipolona dushelele lako haki ya nani tena nilihisi nimepigwa na shoti ya umeme'"
Kabla hajajibu uiingia ujumbe kupitia akaunti yake ya enigma ukimuuliza
"what asset do we have on play"
"van meer" alijibu Herman
"operation "
"clean sweep and self destruct"alijibu Herman
"status"
"on progress "alijibu Herman
"GOOD LUCK"

Baada ya kupata ujumbe huo alimuonesha gwantwa na kumuambia kuwa kazi imeshanza rasmi hivyo ajiandae kimwili na kiakili pia aliwatumia taaarifa watu wote wanao hisika na kuwaambia misheni inaanza rasmi pale yeye atakapo kanyaga ardhi ya Tanzania kwa kutumia akaunti zao za enigma, kila aliye pata ujumbe roho ilianza kumuenda mbio na kumfanya azidishe juhudi kukamilisha majukumu yake kwani yalikua yamebaki masaa mchache tu mchezo hatari wa kufa na kupona uanze, mungu sio Athumani muda ulifika Herman na gwentwa walitua Dar es salaam na akaunti zikaonyesha rangi nyekundu chini ilionyesha maandishi haya "Show time" yaani muda wa kazi…………

***********itaendelea***************
 
STORY :MANOEUVRE (MANUVA)
MTUNZI: HERY_MILLER
SEHEMU YA 4

Mr van meer na timu yake waliwasili pembezoni mwa fukwe za bahari ya hindi wakiwa na vifaa vyote vinavyo hitajika kukamilisha misheni yao,ilibidi watie nanga mbali kidogo ili kukamilisha taratibu za utoaji mizigo bandarini zikamilike.

Candy na rogers walikua njiani kuelekea Tanga wakiwa na nyaraka muhimu zinazo hitajika kukamilisha zoezi lao la kutoa mizigo bandarini,baada ya kuwasili maeneo ya club lakasachika walikutana na vigogo wa bandari walio waelekeza jinsi ya kufanya na kupewa mabaharia kadhaa ili kuhakikisha zoezi linakamilika kama walivyo kubaliana.

Kama ilivyo kawaida ya mwanaume rijali vibinti vikikatisha ndio macho ya rogers yalivyokua yakipata wakati mgumu ndani ya Tanga raha,macho mazuri, miguu ya shampeni,figa matata zilizotiwa ndani ya madera na baibui vikamfanya achanganyikiwe kabisa. Mapema siku iliyo fatia meli ilianza kuingia bandarini na mizigo ilianza kupakuliwa na kuwekwa tayari kwa ajili ya kuelekea sekenke kukamilisha kazi, mr van me'er alikutana na rogers kujua watafikaje sekenke kwa muda muafaka na bila matatizo yeyote baada ya mazunguzo ya muda mfupi walimalizana lakini swala la usalama lilikua ni kikwazo ndipo van meer alipowashtua walinzi wake wakapate maelekezo toka kwa mtoto mzuri candy

"from now on, we will be under command of our new team leader miss candice,she is highly trained assassin and much experience in field combat more than anyone in our group "alisema mr van meer akiwaambia walinzi wake aliokuja nao
"she's simple in appearance but complex in nature please boys play safe"alimalizia mr van meer
Waliingia kwenye chumba wakazungumza na kupanga jinsi ya kuhakikisha usalama unakuwepo wakati wote wakati huo mizigo ikitayarisha kwa ajili ya kuelekea sekenke mkoani singida '

"any question
opinion
or suggestions ........ Silence means we are together but every one has to remember that the only communication channel is through enigma streaming line on your account and is live twenyfour seven"alisema candy
" it's show time let's move"aliwaamuru candy

Kila mtu alichukua nafasi yake na safari ya kuelekea sekenke mkoani singida ilianza chini ya ulinzi mkali malori makubwa mawili aina ya scania yaliyobeba vifaa na min bus mbili zilizowabeba wafanyakazi huku pikipiki nne aina ya honda xl250 mbili nyuma na mbili mbele zikisafisha njia na magari sita aina ya jeep yakiwa na walinzi sita kila gari wakiwa na silaha za kutosha huku candy na rogers wakiwa ndani ya gari aina ya AUDI Q5 HYBRID nyeusi wakiongoza msafara huku camera iliyo nyuma ya gari hilo ikirekodi safari nzima na kuirusha live kwenye mtandao wa enigma kwa njia ya setilaiti na kuwaonyesha njia ilivyo wanakoelekea.

Dar es salaam team ya Herman na wenzake walikua wanangalia kinacho endelea live kutokea Tanga huku nao wakikusanya vitu vyao tayari kuelekea sekenke mkoani singida kwa ndege maalumu ya kukodi kwa kibali cha kampuni ya utafiti wa madini kwa hisani ya watu wa ujerumani kwa muda wa mwezi mmoja na nusu,kitu cha muhimu kilikua ni ramani(skelett) inayoonesha mahali ilipo hazina ya madini ya dhahabu iliyofichwa kabla ya mgodi kufungwa waloitunza vema iliwasije wakatafutana baadae.

Big tunchiii alipewa jukumu la kuangalia maeneo yao ya muhimu kwenye mtandao na kuona kama kuna mtu anafuatilia mpango wao kwa namna yeyote ile baada ya kujiridisha alitoa taarifa na wakaannza safari yao ya kuelekea uwanja wa ndege wa julius nyerere.walingia kwenye kambi yao sekenke mapema na kuanza kukagua maandalizi kabla kufunga mitambo iliyokua njiani.

Baada ya kusafiri kwa siku mbili hivi candice na rogers pamoja na team nzima ya mr van meer walipumzika dodoma ilikupata chochote kabla ya kuelekea sekenke ndipo mmoja wa walinzi wa mr van meer alipoamua kuchukua nafasi hiyo kujaribu kukimbia na min bus iliyokua na nyara muhimu pamoja na drone(ndege ndogo inayo endeshwa kwa remote control) kabla hajaanza kuondoka candy alimuona na kumuomba asifanye utoto huo maana atajutia lakini jamaa hakuelewa na alianza kuondoka kwa mwendo mkali candice hakuwa na jinsi ilibidi achukue bunduki yake aina ya smg rifle na kuwaambia waliobaki wasiogope akapanda kwenye pikipiki xl250 na kuanza kumfukuzia na kama kawaida mawasiliano yalikua yanaonekana live kwenye mtandao wa enigma kwa njia ya setilaiti na kuwafanya waliokua wanatazama wahisi wanaangalia muvi lakini kumbe ni kweli,huku akijiamini kupita maelezo candy mkono mmoja akiwa anavuta spidi iliyofikikia mwandokasi wa kilomita 170 kwa saa na mkono wa kulia akiwa ameshika mashine aina ya smg
"yurii stop the car "
"watch me bitch"alisema yuri ambeye naye alikua vizuri kuendesha gari
"last time yurii stop the dem car!!, you give no choice "alibembeleza candy
Jamaa alizidi kuongeza mwendo huku akichora barabara nzima kuzuia candice asimpite ghafla ikasikika sauti kwenye mtandao ikisema
"do what you do best.. Baby, shut him down now"alisema Herman
"roger dat boss"alijibu mtoto mzuri candy huku macho yake yakiwa yamebadika tayari kutoa roho ya yurii aliyekuwa anazingua.

Kwakuwa walikua wanaona kilichokua kinaendelea kila aliyekua anamfahamu candy alinuonea huruma yurii kwani alikua amekwisha kuitaoa bunduki yake begani nakuishika mkononi akiwa ana muangalia yurii kwa pembeni kwenye kioo huku kamuonyeshea mashine kabla hajafyatua risasi
"i was testing your skills love, sorry am responsible for everything ……yurii stop the dem car" ilikua sauti ya mr van meer huku akitweta kidogo
Kweli yurii alimsikiliza boss wake huku kijasho kikimtoka maana alikua anatazamana na mashine nzito mbele ya macho yake ambayo ipo mikononi mwa mtoto mzuri muuaji aliyekwisha toa roho za watu wengi katika maisha yake.

Aliposimama na kutoka kabla hajaongea jambo lolote yurii alimiminiwa mvua ua risasi na candice na kumfanya adondoke chini kama zigo la mahindi huku wangine wakishuhudia macho yaliwatoka na kufanya wapigwe na butwaa utadhani wameona mlango wa kuzimu unafunguka na wao wanaitwa waingie motoni
"we have to move now,come pick me up don't worry he will be fine,it was just a plastic bullet " alisema candice na kuwafanya wote wavute pumzi na kumshukuru mungu kwa yote yaliyotokea

Safari iliendelea kila mtu akiongea lake huku akiitilia mashaka misheni wanayoenda kuifanya kama ni kweli ya utafiti au ugaidi kama sio uharamia baada masaa kama nane wakawa wameingia sekenke mkoani singida ndani ya kambi yao na kupokelewa na akina Herman, tunchii na gwantwa na kuanza kupewa maelekezo kwa sababu ilikua ni usiku walipumzika lakini kwa sharti la kutokujaribu kufanya utoto kama waliufanya van meer na yurii na kwa atayethubutu atapigwa risasi ya kichwa papohapo.

Kwenye hema alilokua amelala Herman alisikia mtu ananyemelea alihama alipokua amelala nakuificha kwa pembeni alipotazama kwa makini aligundua alikua ni gwantwa na alishajua shida yake ilikua ni mpepe basi bila hiyana alifata kwa nyuma na kumshika kiuno na kuanza kumnong'oneza sikioni
"tupo kazini mama na tulikubaliana ni shoo moja ya kibabe vipi tena"
."kwahiyo vipi sasa acha uzembe mtoto wa kiume "
"hupati kitu hapa,huku kazi tu mapenzi mjini"
"me siondoki hapa hadi kieleweke hivi unadhani nawezaje kuondoka "
"nakuitia walinzi kama huondoki kwa hiari yako "
Huku akisonya na kumuangalia kwa hasira herman gwantwa aliondoka na kuelekea kwenye hema lake.

Jua lichomoza na shughuli za kukagua eneo zilianza bigi tuchii alihakikisha drone ina chaji ya kuiwezesha kusafiri angani kwa masaa matatu na kupiga picha maeneo yote wanayo yataka kwani ndio alikua anamalizia kuifungia kamera aina ya canon 7D iliyowekewa progamu ya magic ranten kwa ajili ya kutoa picha hd za still na video. Huko van meer na watu wake wa nguvu wakiongozwa na yurii wakifanya yao na kuanza kufunga mitambo mbalimbali kabla ya kujua eneo halisi yalipo madini ili kuanza kuyachimba na kuondoka nayo

Drone ilitumwa angani na wote walikaa kusubiri itue ili wajue eneo na kazi ianze rasmi kila mtu alikua na hamu ya kujua kiasi cha madini kilichopo iliwajue kazi itachukua muda gani kumalizika na njia zitakazo tumika.....mungu sio athumani drone ilitua ikiwa na majibu yote na wakaambiwa wasubiri saa moja wajue kinacho endelea ……………………

**********ITAENDELEA **************
 
STORY :MANOEUVRE (MANUVA)
MTUNZI :HERY_MILLER
SEHEMU YA 5
Mitambo maalumu iliyo fungwa katika eneo lililokua linasadikika kuwa na madini yaliyofichwa tungu enzi za utawala wa kijerumani ilikua tayari kuanza kazi ya kuchimba ardhi hiyo lakini walikua ni lazima wasubiri maelezo ya kitaalamu kutoka kwenye kifaa mbacho taarifa zake zinamaliziwa kuhakikiwa na team nzima ya mr van meer pamoja na big tunchii, huku wanyeji na wakazi wa maeneo jirani wakiendelea kujiuliza nini kinaendelea na kujengea hisia tofauti mbona watu wengi wa mataifa mbalimbali! Na je wanafanya shughuli gani hapo tena chini ya ulinzi mkali?.
Ripoti ilikamilika majira ya saa tano asubuhi na wahusika walikusanyika kusikiliza, herman alikua anatoa maelezo kwa kiswahili huku gwantwa akiyatafsiri kwa kiingereza
"majibu yamefanana kwa asilimia zote na tulichokua tunategemea, tupo eneo sahihi kilichobaki ni kuanza zoezi la uchimbaji na kuyasafirisha yanapotakiwa kwenda"ilikua sauti ya herman akiwa na sura ya kazi kwelikweli
"kutokana na unyeti wa swala hili usalama ndio kitu cha kwanza kwa sasa kuvuja kwa taarifa hii kunaweza kutuletea majanga makubwa sana kila mtu achunge mdomo wake"huku akiwa amekunja ndita kama mtoto aliyefinywa herman alisisitiza
"I think we all heard the man, if so let's go do the dam business "ilikua sauti ya kibabe ya van meer akionyesha mwani wa kutaka kupiga kazi
"kila mtu afanye kazi aliyopangiwa na aulize anapoona hajaelewa ilitumalize zoezi mapema tuna masaa 48 kuanzia sasa tuwe tumeshapotea maeneo haya la sivyo tutaharibu misheni nzima,kila mtu ajitahidi kucheza na muda, juu tuanze kufanya yetu sasa"alisema huku na yeye akielekea kwenye eneo lake la kazi
Umati ulitawanyika rogers alipewa kazi ya kwenda manyoni kuchukua spare moja muhimu iliyokosekana alipokua anataka kuondoka mtoto gwantwa alimwambia naye anataka kwenda nae town, waliingia kwenye gari na kuanza safari yao wakiwa njia kutokana na ukame aliokua nao gwantwa alianza kuleta mitego na usumbufu mara akijifunue mara ajilembe rogers aliopoona hivyo ilibidi amuulize
"vipi wewe mbona utulii"
"nitulize "
"weee mtoto mbona unanitaka ubaya mchana wote huu"
"mhhhhh kweli siku hizi wanaume wameisha yaani kusikia hamsii hata kuona hamuoni"huku akimshika paja na macho akiwa kayalegeze utadhani amekula kungu gwantwa alijishobokesha
"jamani jamani chondechonde kwa huu ugwadu niliokua nao naona unanichanganyia habari tu "
"mwenzio nashindwa kuvumilia yamenifika hapaaaaa"huku akionesha kwenye paji la uso na kupitisha vidole kwenye lips zake tamu zilizojaa utamu mtupu
Rogers alihisi kama shetani anamnyemelea alichokifanya ni kusali kimoyomoyo huku akiongeza mwendokasi ili wawahi wanapokwenda kabla maji hayaja zidi unga, walipokarobia kufika kwa hasira gwantwa alisonya msonyo mkalii na kutoa maneno ya dharau ambayo kama huna moyo mgumu huwazi kuvumilia
"jogoo la kuchora huwiki wala hudonoi nakuone huruma hupandi mtungi kazi kuendesha magari ya wanaume wenzako tu"
"maneno ya mkosaji tu hayo una chuma cha moto nini! Embu niache wewe ata panya rrrr kila shimo sembuse mimi?"
Walishuka kila mtu akachukua njia yake na walikubaliana wakutane baada ya masaa mawili ili warudi kambini na mizigo walio agizwa.
Mtandao wa enigma uliweza kugundua sauti za majasusi wakiuongelea misheni yao, watu wote wanao hisika pamoja na ramani ya eneo walipo na kinacho endelea mpaka hivi sasa, sauti zilikua kwa lugha ya kirusi na kichina hali hiyo iliwachanganya akili kwa sababu walijua lazima watavamiwa katika hatua yeyote ya misheni yao.Sauti zilitumwa kwenye akaunti ya gwantwa ili atafsiri wapate kujua vizuri kinacho endelea na kila mtu aliambiwa akae tayari kwa lolote
Masaa mawili yaipopita rogers alikua tayari kwenye usukani kuelekea sekenke na spea alizoagizwa huku akimkata jicho la wiziwizi gwantwa
"kama namiona vile uko ndembendembe kitu kimeloa chapachapa"
"Muda wa kazi huu wewe joka la kibisa usijifanye huelewi mambo yamesha haribika huko"huku akiwa bize na simu yake gwantwa alimwambia rogers
"kivipi tena "
"kuna watu wamegundua mchongo wetu na wanampango wa kutuvamia na kutupora mzigo na wako vizuri wana kila aina ya vifaa"
"daah basi ngoja niongeze mwendokasi tuwahi kufika kabla hakija nuka"
Bila kupoteza muda rogers alianza kufanya yake huku akisali wafike salama kwani alishaanza kutetemeka na kijasho kilianza kumtoka,baada ya mwendo wa dakika kumi gari aina ya subaru mbili za rangi nyeusi na zikifatiwa na landcruser mkonge mbili nyuma zili wapita utafikiri wamesimama na kumfanya rogers azidi kupata kiwewe na mchecheto, alimshitua gwantwa ambeye alikua bize na simu yake kujaribu kugundua maana ya mazunguzo ya majasusi hao
"baby leo disco linaweza kuingia mmasai tumia enigma setilaiti uone haya magari yametoka wapi na yanaelekea wapi maana yana nipa wasiwasi "
"mhhhhh leo kweli majanga maana naona huyu mrusi ametoa amri ya kuua yeyote atakaye taka kizuia kazi yao na kupoteza ushahidi"
"washitue wadau kwamba kitumbua kinataka kuingia mchanga hivyo wajiandae na wazidishe ulinzi"
G aliwasiliana na candy kuhusiana na masuala ya ulinzi huku herman na mr van meer wakisimamia shughuli nzima ya uchimbaji punde si punde rogers aliwasili na spea iliyokua inahitajika na shughuli ilikua inakaribia kumalizika.
Kazi ilibidi ifanyike usiku kucha na ilipofika saa tisa na nusu usiku big tunchii alikua amesha wafahamu majasusi wanaowafatilia na kuandaa taarifa za majasusi hao na historia pamoja na sifa zao ile ampelekee bosi wake
"bosi inaonesha tumesalitiwa na watu wakubwa katika mpango huu, kwa hawamajasusi walipokea simu toka Moscow urusi ikiwataka waje kutuvamia na wahakikishe wamepoteza ushahidi huku wakipewa ushirkiano na wachina toka Beijing wenye kampuni fulani ya madini hapa nchini "
"basi lazima watakua wale wazee tuliokutana nao kule munich Germany ndio walio tuzunguka"huku akipata mshangao na mfadhaiko herman alizidi kuumiza kichwa kufikiria
"na kiongozi aliepewa misheni ya kutupoteza anaitwa Vladimir kochenco, mwanajeshi wa kikodiwa wa kirusi aliyepigana na kuongoza vita huko Afghanistan miaka ya hivi karibuni kabla ya kustaafu"
"hili sasa limeshakua tatiza kubwa ahhhh"aliacha kuongea baada ya kuona ujumbe wa maandishi uliosema mzigo umeshapatikana bado kutoa tu hivyo basi anatakiwa aende wakapange jinsi ya kuusafirisha
Jumla ya tani hamsini za zahabu iliyokwisha kuoshwa na kuficha ardhi kwa zaidi ya miaka 80 ilishaonekana na kilichobakia ni kuitoa na kuisafirisha kuipeleka ujerumani.Ilitumia takribani masaa masaa sita kutoa tani zote hamsini na kuzipanga kwenye makonte tayari kwa kusafirisha kwa njia ya meli iliyopo Tanga, watu wote wakiwa hawaamini kinachoendelea kila mtu alipewa jiwe la dhahabu lenye uzito wa kilo tano kama zawadi kwa kazi walioifanya na pia kuwapunguzia mawazo potofu na woga
Masaa 48 yalipoisha helkopta mbili zilitua zikiwa na askari wa kikodiwa tayari kuimarisha ulinzi wa mali na wataalamu walio husika na mpango huo,wengine walishtuka kidogo kuona ulinzi ukiongezwa tena kwa helkopta sio jambo la kawaida candy na herman peke yao ndio waliokua wakifahamu nini kina endelea
"what hell is going on young man"van meer aliuza kwa shangao
"preparation to take off"
"any change of protocols"
"everything is on my command from now on,piece of advice do not trust anyone "
"i don't understand "
"the whole mission is compromised "
"how did you know that!"
"I've my sources, stop asking questions get ready we have to move right now"alisema hivyo huku akihakikisha kila mtu yupo tayari kuondoka.
Bila kupoteza muda Herman alivaa jaket maalumu la kuzia risasi (bulletproof) na kuchua mashine aina ya smg na zingine kuziweka kwenye kombati,ubosi pembeni kweli mwanaume hasifiwi kula alibadilika kabisa na kuanza kuwatia wasiwasi waliokua wanamchukulia brazameni bila kupoteza muda aliingia kwenye helkopta huku chini akiwaacha rogers na candy wakisimamia shoo kiroho mbaya, walipojiridhisha kila kitu kipo sawa safari ya kuitafuta Tanga ilianza chini ya ulinzi mkali,awamu hii spidi ilikua kubwa kidogo kwa sababu walikua hawana cha kupoteza, lory aina ya scania lililokua limebeba dhahabu lilikua katikati wakati la mbele na nyuma yalikua na vifaa walivyo vitumia kuchimba madini hayo.
Walipovuka morogoro kabla ya kuingia chalinze walikutana gari zilezile walizoziona rogers na gwantwa walipokua manyoni singida,subaru mbili na landcruser mkonge mbili zikiwa katika spidi isiyo ya kawaida mara ya kwaza walikutana nazo uso kwa uso zika wapita mara ya pili zikawa zinarudi wakagoma kuzipisha kitendo kilicho wafanya wapunguze spidi,walipo ziachia zipite pikipiki aina ya xl250 zilianza kuzifukuzia gari zile ilikujua lengo lao.yurii alikua na pikipiki moja aliongeza mwendo na kuyapita yale magari huku begani akiwa na kombora aina ya RPG akiwabado anajifikilia alsikia milio ya risasi alipogeuka nyuma alimuona mwenzake akiwa huku pikipiki kule na watu wenye asili ya kichina wakiwa wametokeza kwenye madirisha ya magari yale aliyokuwa anayafatilia na bunduki mikononi,nae hakupoteza muda alishika kombora na kulifyatua na kuyasambaratisha magari matatu papohapo na moja kuanguka pembeni,akina candice walipofika eneo la tukio walimkuta yurii akijaribu kumumpa huduma ya kwanza majeruhi mwenye asili y ki asia lakini alisema neno moja tu kabla hajakata roho "Vladimir kochenco "

Vladimir kochenco alikua tayari kashaingia ndani ya msitu mnene chini kidogo kabla ya mto wami eneo walilopanga na majasusi wenzake kwa ajili kufanya shambulio lao na kutoroka na shehena ya dhahabu, waliandaa magogo na senyenge za kuzuia magari ya sipite huku msituni wakiwa na silaha nzito za kivita tayari kutoa roho ya yeyote atakaye leta ubishi..................
Unataka kujua nini kilitokea?
Nani alishinda!
Nani aliwasaliti wenzake?
Na nani atashinda!
Je mchezo wote unafanywa na nani?
USIKOSE
**********itaendelea ****************
 
STORY :MANOEUVRE (MANUVA)
MTUNZI :HERY_MILLER
SEHEMU YA #6
Ndani msitu na mapori ya wami mkoani pwani jasusi wa kimataifa Vladimir kochenco na team yake wakua wanajiandaa kufanya shambulio la kutisha na kupora shehena ya dhahabu huku wakipewa msaada wa silaha nzito kutoka kampuni moja ya kichina kuhakikisha wanafanikiwa na lao, team ilikua na mamafia wa kichina waliotoroshwa gerezani na kua wanatumika katika misheni za kijasusi kama hizi na kulipwa pesa mingi sana wanazogawana na mabosi wao na kuendelea kula raha za dunia katika sehemu mbalimbali za kifahari ulimwengu, genge hilo linaongozwa na lee kan taa mchawise wa shughuli za utekaji na uuaji watu wenye nafasi kubwa katika nchi na makampuni mbalimbali.
Msafara ulikua unakaribia kufika eneo la tukio ambalo walishajua lina walakini kwani lilikua hatio picha za (moja kwa moja) yaani live kupitia mawimbi ya setilaiti kwenye mtandao wa enigma.
Herman alipoona maelezo na sifa za majasusi hao alizidi kuchanganyikiwa, kama kamanda wa msafara ilibidi afanye maamuzi magumu
"PLAN B " ndio neno lililokua linaonekana kwenye vioo vya vifaa vya mawasiliano wanavyo tumia,kila mtu alijia uwezekano wa kufika salama ulikua mdogo kwa hiyo kila mtu atajua atakachofanya kujiokoa mwenyewe, mapigo ya moto yalianza kuwaenda mbio hofu na mshituko vilitawala vichwani mwao.
Gari mbili aina ya jeep zilizo tangulia mbele zilipita na hali ilikua shwari ukimya wa eneo lile ulowatia wasiwasi mkubwa kwani kwa takribani dakika ishirini na tano hakuna gari walilopishana nalo au kulipita na hivyo kuwafanya wazidi kuamini wameingia katika mtego,ghafla sauti iliyo sababishwa maumivu makali ya bega lililopigwa na risasi ambayo haikujulikana imetokea wapi.
Msafara ulisima na ilibidi wajipange kwa kujibu mapigo walianza kumimina risasi maporini bila kijua wanapigana na nani!,walipotulia kidogo hawakumuona mtu yeyote aliyejibu mapigo sanasana zilisikika sauti za ndege angani na wadudu wa mwituni,candy aligundua kua risasi zinatokea milimani
"kuna sniper's (watunguaji) juu ya miti na milima kila mtu ajifiche vizuri"candice aliwaambia wenzake.
Lilipigwa kombora lililolipua kontena moja lililokua na vifaa walivyotumia kuchimba madini,kabla hawaja tahamaki yaliaanza kipigwa mabomu ya machozi na watunguaji(snipers) sasa walikua wanapiga walinzi risasi za vichwani tuu iwe jichoni,sikioni au kosogoni kwa mbaliii huku wikiwa wamevalia mask usoni kuzuia moshi wa mabomu ya machozi na makombora moshi kipunguza uwezo wa kuona mbele , candice na wenzake wijitahidi kupambana nao lakini maji yalianza kuzidi unga na ndio muda Vladimir kochenco na LEE KAN TAA walikua wanaingia kazini rasmi, walianza kuwamiminia riasasi walinzi waliokua wanajifanya wanajua kupigana na kuwa sambaratisha mmoja baada ya mwingine na wakawa wamemaliza kazi , wakaanza kusogele kontena lililokua na madini na baada ya kujiridisha wakaingia kwenye basi lililokua na wataalamu wa uchimbaji wa madini waliotokea afrika ya kusini chini ya uongozi wa mr van meer
"Who is in charge"aliuliza Vladimir kochenco kwa rafudhi ya kirusi
"me"
"who are you "
"van meer c.e.o south African mining co.ltd responsible for extraction of package"
"kill em all except him"
Wataalamu wote walipigwa rsasi za vichwa na mamafia wa kichina walipotaka kuamia minbusi nyingine majasusi wale walipigwa risasi nyingi zilizotokea angani kwenye helkopta alipokuwamo mtu mbaya , mchawise herman ambeye alikua amechanganyikiwa na kuvurugwa utadhani chizi baada ya kuona watu wake walivyo uwawa kikatili na kundi la majasusi linaloongozwa na Vladimir kochenco, wakiwa wanaendele kushangaa risasi zilizokua zinatokea upende wa pili wa mlima hakua mwingine alikua candy aliye waua watunguaji na kuchua silaha zao na kuanza kumimina vyombo kuwalenga wapinzani wake walioko chini huku akipewa msaada n yuriii aliyeshuhidia team nzima ikiuwawa kutokana na uchungu alikua nao alikua anapiga risasi kichwani kwa yeyote atakaye jaa kwenye kumi na nane zake. Helkopta ilishuka chini na heman alishuka wakati inajiandaa kuondoka chopa ilitunguliwa palepale na kumfanya aone mlango wa kuzimu ulikua umefunguliwa kwani aneo lile lote lilikua linanuka damu ya binadamu walio uwawa kinyama kwa kupigwa risasi vichwani. Lilipigwa bomu zito upande wa juu wa mlima lika sambaratisha eneo la kama mita ishirini pamoja na pale walipokua candy na yurii na kumfanya herman anyooshe mikono juu akionyesha amesalimu amri mbele ya majasusi hao walio shindikana kwa kufanya mashambulzi ya kutisha
Baada ya kumkamata herman walimfunga pingu na kumuweka kwenye gari ambomo humo ndani alimkuta mr van meer anavuja damu maeneo tofauti ya mwili,walipojaribu kufungua kontena maalumu lililokua lime hifadhiwa madini walishindwa ndipo walipo mfata herman akafungue mlango,aliwatajia namba ya siri walipoingiza mlango ulifunguka na shehena ya dhahabu ilonekana kabla hajaingia ndani ya kontena mlio wa kifaa kama fyuzi ulisikika na saa iliyokua juu ilionyesha dakika themanini na zilianza kupungua, walipotazama kwa makini lilikua ni bomu ambalo likilipuka eneo la kama kilomita moja litageuka kua majivu ndipo LEE KAN TAA na Vladimir walipo mtazama kwa hasira na kuanza kupiga Hermann kwa kutumia vitako vya bunduki
"trust me you will regret this"Vladimir kochenco alimwambia Herman kwa hasira huku akiwa hajui nini cha kufanya
"did you real think I've no plan b"aliongea kwa dharau huku akijiamini
"what you want kid"
"am not negotiate with terrorist "
"You have to choose either to disarm the bomb and let you live or you die"
"either way am dead man but at least takecare of my wounded friends, let them live and take me hostage instead "
"your demand are granted as you wish kid"
Baada ya kukubaliana msafara wa kueleke Tanga ulianza kwa ajili ya kusafirisha madini kuelekea kusiko julikana mateka wote walivalishwa vitambaa vyeusi machoni kuzuia wasijue wanapelekwa wapi,gwantwa alipoteza misha palepale kabla ya kupelekwa hospitali lakini candice na yurii walikua na roho za paka licha ya majeraha waliyo yapata walikua bado wapo hai, walipofika bandarini Tanga baada ya kupandisha mizigo kwenye meli tayari kwa kutokomea kusiko julikana Herman aligoma kutegua bomu na kuwambia hadi awaone ndugu zake wapo salama
Tayari rogers alikua amesha kabidhiwa candice na yurii kama watu pekee waliopona kwenye shambulio lile na kupewa simu na kuambiwa baada ya dakika kumi na tano atapugiwa simu
"oyo roja mishe zimefeli hawajamaa sio watu ni wadudu tupo Tanga hapa sijui tunaelekea wapi sema cheza n mimi magetoni kwangu si ukikimbuka kile kichupa babu"
"kichupa kipya sio lakini inabidi niwapeleke hawa hospitali wakazie wasechu hao mpaka mwisho"
Baada ya ombi lake kukamilika Vladimir kochenco na LEE KAN TAA walimfata wakimtaka akategue lile bomu kwani zilikua zimebaki dakika kama tano tu, Herman alikataa kutegua na meli tayari ilikua imesha toa nanga bandarini kila mtu alianza kuogopa zipobakia sekunde 30 herman alijifanya kama anataka kutegua alafua akasita waoga wote walishaanza kusali sala zao za mwisho huku wengine wakijitosa baharini, muda uliisha na bomu halikulipuka wote walijikuta wanacheka kama wame changanyikiwa na kuona jinsi walivyo fanywa watoto na herman.
Alipelekwa kwenye chumba cha nahodha wa meli ambeye alikua mr van meer na wasidizi wake kadhaa alipofika pale alijua kua walikua wameuzwa kwani meli ilikua inaelekea cape town afrika kusini
Kilicho mshangaza zaidi ni pale alipoletewa simu aongee na mtu alikua anamuhitaji, aliposikia ile sauti miguu yote ilimuisha nguvu na kumfanya akae chini hakuamini maskio yake kwa alichokisikia
Je unajua alikua anaongea na nani?
Aliambiwa nin!
Je unadhani atachukua uamuzi gani
************ITAENDELEA ***********
USIKOSE
 
STORY:MANOEUVRE (MANUVA)
MTUNZI :HERY_MILLER
Sehemu ya #7
Mawazo yalimzonga na kumfanya anyong'onyee utadhani mtu aliye ugua maradhi makali kwa muda mrefu,hii ilitokana na kujua kuwa waliuzwa kama chumvi inavyo uzwa sokoni na mtu aliyemwamini kuliko watu wote duniani si mwingine bali ni baba yake mzazi ambaye kwa tamaa ya mali aliwatuma Vladimir kochenco na team yake kuja kupora mali na ku ua watu wote walio husika na misheni ili kupoteza ushahidi wa mchakato mzima.

Akiwa ndani ya meli kuelekea africa ya kusini herman alihisi kama dunia yote inamuelemea kwani sura za watu waliokufa chini ya uongozi wake alikua anaziona zinamuita huko kuzimu, ndipo alipoanza kuwaza na kupanga mikakati ya yeye kuwahamasisha akina Vladimir kochenco na LEE KAN TAA waungane nae kwa sababu yeye ndiye anayejua maeneo yaliyo baki na madini na rasilimali nchini Tanzania maana kama baba yake ameweza kumgeuka kwa hichi kodogo je wakipata ramani yenye utajiri mkubwa itakuwaje?,kama mbwai iwe mbwai tu alianza kueleke ndani ya meli na kuwaita wote aliowataka na kukutana kwa nahodha mr van meer na kuanza kujadiliana nao huku akionyesha msimamo wake wa kumpinga baba yake mzee muller aliyemsaliti kwa kumletea majasusi hatari wanaousumbua ulimwengu.
Aliwapa muda wa kuamua na kuchagua upande watakao shirikiana nao katika michakato yake ya kutafuta ramani(skelett) na kugundua maeneo yenye utajiri pamoja
"you have till dawn, make wise choice because i will no longer be the man you use to know "
"give us sometime "

Alitoka na kukaa nje ya meli akiangalia mawimbi ya bahari yanavyo panda na kushuka huku akilinganisha na maisha yake kitu alicho kipigania muda wote kina chukuliwa na watu aliowaamini wangemsaidia kufika mbali ila badala yake wao ndio wamemgeuka, kwa vile aliye anzisha vita hiyo ni mzee muller basi alipanga atakapofika afrika ya kusini apande ndege kuelekea munich Germany kuonana na baba yake mzazi na kujua hatma ya maisha yake.
*************************************
Rogers alihakikisha candy na yurii wanapata matibabu ya mahera waliyo yapata kwenye mapigano makali kule wami lakini kikwazo kikubwa ni majeraha na vipande vya risasi vilivyo ndani ya miili ya wagonjwa wake. Alimtafuta daktari wa hospitali kubwa moja hapa mjini na kumuhonga kiasi kikubwa cha pesa kwa ajili ya kuwafanyia upasuaji kuondoa vipande vya risasi vilivyo nasa katika miili yao,ilichukua muda wa wiki moja kuanza kupata nafuu kampuni yao ilokua imesimamisha shughuli zote za kiutendaji kwa sababu za kiusalama, alikumbuka maneno ya mwisho aloyoambiwa na Hermann hakumuelewa lakini alijua lazima yana maanisha kitu fulani,alipomuaga candy anaenda kutafuta nyaraka zilizo salia nyumbani kwa Hermann na wafanyakazi wengine waliopoteza maisha pia alimwabia kuwa gwantwa alipoteza maisha na mwili wake ulikabidhiwa kwa familia kwa ajili ya mazishi.
"kuna kitu kinaitwa black box kipo nyumbani kwa Hermann kwenye chumba maalumu cha mawasilano kikatunza kumbukumbu zote za mtandao wa enigma "
"kumbe ndio maana jamaa alijitolea kufa ili wewe upone kwa sababu unajua siri hii kubwa ya misheni"rogers alimuambia mwenzake
"vipi big yuko wapi ila uipata black box tutajua kama yupo hai au la maana yeye ndiye mwenye pini za kuwashia mtandao "
"tunchii sijaonana nae wala hatuja wasiliana ila inasemekana ile meli iliyotokomea na dhahabu inaelekea afrika kusini naamini herman watakua nae na atakua bado yupo hai"
Roger aliwasha gari kueleke alipokua anaishi Herman ilikua mida ya jioni jioni hivi kwa vile alikua na funguo alingia ndani na kuanza kutafuta kile chumba alichoelekezwa, alingia na kuwasha taa akaliona lile sanduku jeusi aliloelekezwa na candy alichomoa nyaya na kulichukua akatoka ndani ya kile chumba alipokua anamalizia korido alisikia sauti ya kike ikimwambia
"black box chini mikono juu fasta"
Rogers hakuogopa akageuka nyuma akakutana na zainab Habib aliyekua anamfahamu kama demu wa boss lakini cha kushangaza alikua ameshika bastola iliyovalishwa kifaa maalumu cha kunguva mlio na akiwa amishika kwa kijiamini
"shemeji bora nimekukuta maana ni majanga juu ya majanga "
Risasi zilipigwa chini ya sakafu pembeni kidogo ya mguu wa rogers na kumfanya ajue kua hata Zai naye ni tishio kwao akanza kupiga hesabu za kutoroka na black box
"unashindwa kunielewa tu mimi na wewe tupo pamoja"
"me nipo kazini wewe acha ilo box unajiingiza kwenye matatizo maubwa mno"
Kwa vile zainab alikua amevaa viatu virefu (high hills) rogers alijua akipata nafasi ya kukimbia mwanamke yule asingeweza kumkamata hivyo akajifanya kama anaweka chini vile kitendo cha kushangaa sekunde kadhaa alikua ameshatoweka na kutokomea nje kabisa aliko paki gari lake na kuanza kiendesha kwa kasi ya ajabu kuelekea anakokujua mwenyewe.
Simu iliita kuangalia alikua big tunchii
"kaka vipi uko wapi"
"niko njiani kuna watu wananifukuza nimechukua black box nyumbani kwa Herman "
"Sasa izime au kama uwezi nisomee code zilizo andikwa juu hapo"
"1477554AKKL"
"poa nimeshaizima nitajie namba za gps ya simu yako itakuekeze ilipo safe house uje utulie"
Baada ya kusikia maneno hayo aligeuza gari na kwenda kuwachukua akina candy na yurii akanza kuelekea pembezoni mwa mji ramani ilopokua ina muonyesha kuna safehouse alikua amejificha big tunchii, walipofika big aliwapokea na kuwapeleka waginjwa ndani kwani majeraha yalikua yameanza kupona lakini bado walikua wagonjwa. Jumba lilikua lina kila kitu ndani kwa ndani kabla hawajatulia big tunchii alichukua simu zote na kuzitoa line na kuziwekea kifaa maalumu cha kuzuia kuona mtumiaji wa simu hiyo yuko wapi
"jamani sikieni kama mpaka zainab ni jasusi inawezekana wakawepo majasusi wengi kushinda tinavyo fikiria hivyo tatizo ni kubwa mno"alisema candy
"cha kufanya inabidi tujifiche huku tukiendelea kuchunguza kwa makini wote wanaohusika na tujue nini hatma yetu"alijibu big tunchii
Baada ya kukaa katika nyumba ile kwa siku mbili walianza kupata taarifa za kuwatisha kwamba warudishe black box au watamuua Herman kwani yupo mokononi mwao hivyo maisha yake yanategemea maamuzi watakayo yafanya wao. Heman alipigwa picha bila ya yeye kufahamu na zilitumika kuwalazimisha wenzake walioko Dar es salaam warudishe kile kisanduku cha siri chenye taarifa zote za misheni
"jamani tunafanyaje sasa maana wametuambia tusipo wajibu ndani ya masaa matatu wanamuua boss"aliuliza rogers huku akionekana kuwa na wasiwasi
"cha msingi hapa ni kuwarudishia box lao lakini lazima tuwe na plan b"big tunchii aliwaambia wenzake
"na hiyo plan b ni ipi"
"ntatoa sehemu ya chip hivyo watashindwa kutoa data wakiona hivyo watatusikiliza na ndivyo tutakavyo muokoa boss "
Kila mtu alikubalia na mpago huo na walikaa sasa kusubiri simu ili wawape maelezo ya jinsi ya kubadilishana black box na heman.
*************************************
Meli ilitia nanga capetown afrika kusini laikini hakuna mtu hata mmoja aliekubaliana na kujiunga na Herman badala yake kila kitu kilikua kinaendelea kama kilivyo pangwa, utaratibu ulikua Herman anapandishwa ndege itakayo mpeleka Johannesburg atakapopewa hati mpya za kusafira na chini ya ulinzi mkali atapelekwa munich Germany kwa mzee muller.
Madini yalipelekwa kwa mr van meer ambako watatumia mitambo yake kuyatengeneza yawe yanaweza kuuzika kwa matumizi mbalimbali, huo ndio ulikua mwisho wa heman kuonana na van meer. Masaa mawili yalipita chini ya ulinzi mkali wa Vladimir kochenco na warusi wenzake walikua kwenye ndege kuelekea munich Germany ila kundi moja likiongozwa na lee kan taa lilibakia afrika kusini kusimamia zoezi la kutayarisha madini. Wote walikua sura meee sura ya mbuzi hakuna aliyemchekea mwenzie ndege ilitua munich wakaingia kwenye gari lililokuja kuwapokea na kutokomea mafichoni kwao herman alichomwa sindano ya usingizi naalipokuja kishtuka alkikuta amefungwa kwenye kiti na mbele yake kuna kamera na vifaa vya kutesea vya umeme na vingine.
Meee muller alingia na kimtazama mwanae bila huruma kweli wajerumani wana roho mbaya na kuamrisha kamera ziwashwe na nyaya za umeme zilochomekwa na yeye alichukua kisu na kumkata pajani alopopitisha waya wa umeme na kumfanya Herman aanze kulia kama mbwa na kwa uchungu kwani alikua ana sulubiwa bila makosa yoyote
Upande wa pili simu ya video ilipigwa Dar es salaam walipokua rogers na wenziea waliokua wakishihudia unyama aliokia anafanyiwa herman na baba yake mzazi na kuwafanya wapote woga mara dufu zaidi ya mwanzo
"you have hard decision to make now, either him or the box"
"father he is your so......"hata kabla hajamaliza kusema mzee muller alimtia bisu la paja mgumuu ambao ulikua haujakatwa mwanzo
"we will deliver the box but in our term "
"am listening "
Rogers alimuelezea mzee muller kama alivyopanga na wenzake lakini tatizo ni kwamba mabadilishano yanabidi yafanyike Tanzania.
Mzee muller ilibidi akubali na aliwamuru walinzi wamtoe kitambaa mdomoni ili aweze kuongea na mwanae kidogo, lakini alipoinama kutatazama usoni alitemewa mate usoni alipata hasira na kupiga makofi mawili herman ambeye alikua amefura kama mbogo au chui aliye jeruhiwa.Hakutaka kusikia chochote kutoka kwa baba yake sanasana alimuapia labda amuue muda huo ila akimuachia nafasi ya kuishi tena atajuta maisha yake yote.
Mzee aliona ni kelele za chura tuu aliwamuru walinzi wamfunge vidonda na safari ya kurudi Dar es salaam ianze, bila kupoteza muda walipanda ndege na upande wa pili rogers ilibidi yeye ndiye asimamie misheni ya kurudisha box kwa sababu yurii na candy walikua hawajawa sawa kiafya kuweza kuhimili mikimiki ya mapigano.
Majira ya saa nane za usiku Vladimir kochenco na wenzie wanne walitua uwanja wa ndege wakiwa na mateka wao tayari kwa kwenda kuchukua black box kwa njia yeyote ile,walipofika walipokelewa na zainab Habib na kumfanya herman apate maumivu makali ya moyo kumbe hadi mpenzi wake alikua amepandikizwa na majasusi. Zai alimkumbatia herman huku akimbusu kimahaba
"jamani beib i mis you"
"umefanya kosa kubwa sana kunisaliti lakini utanikumbuka mama"
Zai aliposikia maneno hayo alisonya kwa dharau na wakaingia kwenye gari kueleke escape1 walipokubaliana kukutana na rogers.
Simu iliita alikua rogers akiwataka akina Vladimir kochenco na team yake wapande boat kuelekea kisiwa cha mbuji watakapo badilishana black box na herman.
Walingia kwenye boti na safari ikaanza kuelekea mbuji,walipofika walimkuta rogers akiwa yupo peke yake na machozi yalianza kumtoka kwa jinsi Herman alivyokua kachakaa utadhani anaumwa sana
"nipeni mtu wangu mzigo wenu huu apa"
"anajifanya mjanja sio unazani tunaweza kuamini unatoa black box kizembe kiasi hiki"
"imani zenu hazinihusu mzigo wenu huo"
Zainab alichikua mzigo na kumpa Vladimir kochenco aujaribu kama upo sawa, baada ya kuukagua akamwabia kuna chip haipo na ni ya muhimu kwani box lote hilo bila chip ni kazi bure, zainab baada ya kujua wamezidiwa akili alimshika herman mikono na kumfungua pingu na kumruhusu aende kwa Herman alipo fika katikati alimpiga risasi ya mguu na kushitua kila mtuu
"hatu jaja kucheza hapa tupo kazini itakayo fata ni ya kichwa na nakumalizia na wewe"zainab aliongea kwa suti ya juu iliyijaa hasira na gadhabu
Rogers alinnyosha mkono juu ndipo walinzi watatu aliokuja nao Vladimir kochenco walipigwa risasi vichwani na kufa papo hapo bila kujua zilipo tokea
"nadhani umeelewa sasa kua sitanii mchumba, mlete herman mpeleke kenye ile pikipiki ya majini pale alafu ntawaambia chipi iko wapi"
Wakawa hawana ubishi tena wakafanya kama walivyo ambiwa naye akapenda ile pikipiki akaiwasha na wakaanza kuondoka
"nani anafunguo za boti "
"dereva aliangalia akasema mimi apa"
"chip ipo ndani ya holder hiyo "huku akiweka spidi kali na kuanza kufutika mbele ya macho yao
"the kid got skills,i like him"alisema kochenco
"mwanangu jikaze unishikilie vizuri we are going home "rogerz alimuambia herman huku akiwa katika mwendo mkali ndani ya mawimbi ya bahari ya hindi
"nashukuru sana hapa nime changamyikiwa sielewi lolote"
Rogers alizidi kutokomea akiwa kambeba herman ili amiwahishe mafichoni………………
***********ITAENDELEA ***********
USIKOSE
 
STORY:MANUVA
MTUNZI :HERY_MILLER
SEHEMU YA #8
Rogers alipofika fukwe za kigamboni kwa mbele kidogo aliwaona jamaa zake alio kubaliana nao atakutana nao hapo, watu wale waliaanza kumfuata rogers wakitokea kwenye kipori Kidogo cha miyombo
"fanyeni fasta fasta jamaa hali yake ni mbaya kapoteza damu nyingi"roger aliwaambia wale jamaa

Bila kupoteza muda walimbeba herman na kumuingiza kwenye gari lililokuwa limeegesha mbele kidogo kutoka pale na kumuacha mmoja alienda na kuondoka na ile pikipiki ya majini na kutokomea nayo.
Mbiombio walimuwahisha kumpeleka jumba la siri ili akatolewe risasi aliyo pigwa mguuni na zainab, wakiwa njiani rogers mkono mmoja akiwa anaendesha gari mkono wa pili anaongea na simu na daktari
"dokta nipo chini ya miguu yako kuna dharura kubwa naomba uje kule kule mafichoni sahizi"
"dharura gani tena niambie ili nijue nini kinahitajika"
"bosi anavuja damu amepigwa na risasi mguuni "
"ok damu yake ni group O sio,nakuja sasa hivi"
"chondechonde ufanye haraka"alikata simu na kuendelea kuendesha gari kwa spidi kali.

Dakika arobaini na tano zilikwisha katika na tayari herman alikua juu ya kitanda akitibiwa na kufanyiwa upasuaji mdogo kwenye mguu aliopigwa risasi lakini kwa bahati nzuri risasi haikupiga kwanye mfupa ila ni vipande vidogo tu vilovyo nasa kwenye nyama za paja na kutengeneza tobo kubwa lililokata mishipa ya damu na kumsababishia kupoteza damu nyingi na kuleta maumivu makali,dokta alimuongezea damu na kumtundika drip kadhaa za maji kisha kumuosha na kumfunga majeraha, dawa za kutuliza maumivu na usingizi zilimfanya alale usingizi mzito kama pono na kuwafanya wenzake wamsubiri ili awaambie nini kilitokea na hatua gani wachukue kukabiliana na matatizo yanayo wakabili
*************************************
Vladimir kochenco na timu yake baada ya kupata chip na kukamilisha black box bila kupoteza muda walianza safari ya kurudi munich Germany lakini sasa hivi walikua na zainab Habib ambaye nae waliagizwa warudi nae.
Siku ya pili baada ya kuwasili munich Germany blackbox ilikaguliwa lakini hakukua na taarifa zaidi ya misheni ya sekenke ikionyesha kila hatua waliyopitia mpaka mwisho.
Mzee muller alipogundua hilo alijua herman bado ana umuhimu mkubwa katika harakati za uvunaji wa rasilimali zilizobakia hivyo kwa namna yeyote ile lazima arudi kwenye timu yao lasivyo watapoteza vitu vingi sana kwani hawajui atafanyanini na taarifa alizonazo.
Zainab Habib aliitwa kwa lengo moja tu,ambalo ni kupewa misheni mpya ya kurudi Tanzania na kumchunguza herman kwa njia yeyote ile na awe anatoa taarifa ya kinacho endelea, mzee muller alimwambia hiyo ndio kazi yake ya mwisho na akiikamilisha kama alivyo agizwa atarudishiwa mtoto wake aliyefichwa kusiko julikana ili yeye afanye kazi ya ushushu kwanye kampuni ya mzee muller.
Zainab Habib alikubali kwa sharti moja tu lazima ajue mwenae kama yupo hai na anapata malezi mazuri,kweli ilipigwa simu ya video na zainab aliongea na mwanae huku akimtazama kwani yapata miaka minne hajawai hata kusikia sauti yake,huku machozi ya kimtoka kwa uchungu na hasira alikubaliana na mzee muller kuchunguza herman na kuwatumia taarifa atakazo zipata.

Vladimir kochenco alipewa misheni ya kwenda afrika kusini kusimamia shughuli ya kusafirisha madini yaliyo tayarishwa tayari kwa matumizi ya kawaida kwenda nchi za mashariki ya mbali China , Hong Kong, na Thailand kwa wateja ambao walisha yalipia.
*************************************
Fahamu zilimrudia Herman na kuzinduka toka kwenye usingizi mzito huku akiweweseka kidogo aliangalia kwa tabu aliwaona rafiki zake ambao hakuwaona kwa muda mrefu kidogo tangu siki ile walipo vamiwa na kuporwa mali zao na kundi hatari la majasusi lililoongozwa na Vladimir kochenco, kwa uchungu machozi yalianza kumtoka na kuanza kuwaomba msamaha kwa yote yaliyo tokea
"nashindwa hata niseme nini maana siamini kama mpaka leo mpo na mimi"huku machozi yaki mtoka aliongea kwa huzuni na kuonesha kukata tamaa
"usihuzunike sana tupo pamoja mpaka kieleweke"roger alimtia moyo
"pole sana bosi tuombe mungu kila kitu kitaenda saw"big tunchiii nae alimuongezea matumaini

Alishuka kitandani na kukanyaga chini aliashangaa anaweza kitembea wakati alipigwa risasi pajani
"mhhh mbona naweza kutembea inamaana..... Mhhh mbona naanza kua na mashaka"
"mashaka na nini tena"
"mtu professional kama zainab hawezi kikosea kulenga ina maanisha alikua hataki kunidhiru"
"hiyo sio kweli maana yeye ndiye aliyenivamia nyumbani kwako wakati na chukua black box na jana alikupiga risasi "
"ni amini mimi kwa watu wa aina yake kwa uwezo wako angetaka kukuua usinge kua hai leo mimi na amini sio mtu mzuri lakin hakuwa na lengo la kutuangamiza"herman alisisitiza
Wote walimuacha hawakutaka kumpinga kutokana na hali aliyo kuwa nayo lakini hata wao walianza kuingiwa na wasiwasi kidogo maana kama ni kweli hakuna aliyeweza kupambana nao kama wangeamua kutumia nguvu zao zote kuwa sambaratisha.
Aliwasimulia kila kitu kilichotokea kuanzia siku ile pale wami hadi kifika ujerumani na kukutana na baba yake mzazi ambaye alimfanyia unyama ambao wote waliuona kwa macho yao,hasira uchungu na hisia kali ziliwaingia na machozi yalianza kuwatoka mmoja mmoja.
Alipona hivyo aliamua kukatisha mazungumzo yao kwani aliwaona candy na yurii wanaingia
"ohh i don't belive you stil alive "
"even myself i still wonder "candy alijibu huku akionyesha mshangao wa huzuni
"thank God you still alive"yurii mjibu bosi wake
Walisalimiana na kumuuliza big tunchii kama vifaa vya kuonesha vitu vilipo kwa njia ya mtandao (gps tracker) walivyo vipachika kwenye madini ya dhahabu yaliyotekwa na majasusi na kutoshewa afrika kusini
"madini yanaonekana yapo eneo lilelile kwa mr van meer na bado hayaja hamishwa kwenda eneo lingine"
"tuwe makini na kujua wanataka kuyapeleka wapi ilitujue tunayapataje au tunawaharibia vipi mipango yao"herman alimwambia big tunchii
Kila mtu aliendelea na kazi yake aliyokua anifanya ili kugundua maeneo mengine yenye utajiri huku wakipanga mikakati ya kuwaharibia mipango majasusi walio wapora n kuua baadhi ya ndugu zao walio kua nao
*************************************
Vladimir kochenco aliwasili afrika kusini tayari kuanza safari ya kusafirisha madini kuelekea mashariki ya mbali China , Hong Kong na Thailand ambako madini yalikua yanaenda kuuzwa kwa mabilonea waliolipia. Van meer na crew yake walikua wemesha pakia mizigo tayari kwa kuanza safari baada ya Vladimir kochenco kuwasili alikagua mzigo na alipo rizika na jinsi kazi ilivyo fanyika alimuaga van meer na walianza kuondoka kuelekea mashariki ya mbali na walikua wanaelekea Thailand kwa bilionea maarufu KRIT JAA.
Mtandao wa enigma ulionesha kwamba shehena ya madini ilikua inaondoka kuelekea Thailand na pia walitumiwa ujumbe wa siri uliosema kuwa madini hayo anauziwa KRIT JAA. Big tunchii alipata taarifa hizo na kuwashiriksha wenzake waliomuambia wafanye mpango wa kuwatafuta mamafya wa Thailand ambao wana bifu na krit jaa ili wawavamie siku ya kupokea mzigo unaokuja chini ya ulinzi mkali wa Vladimir kochenco na timu yake.
Herman hakuwa mzembe sana aliwasilia na kundi la mamafya hao wa Thailand linalo julokana kama VELVET likiwa chini ya uongozi wa jambazi sugu lililo kubuu Bon Bung a.k.a double B na kuvujisha siri zote za usafirishaji wa madini na thamani yake pamoja na watu wanao sindikiza mali hizo na taarifa zao zote. Pia aliakikisha anatoa taarifa kwenye vyombo vya usalama ili kama VELVET ya double B ikizidiwa nguvu basi wakose wote.

Mzee muller alijua wazi kua kazi haita kua rahisi hivyo alichukua tahadhari mapema ya kuweka wapelelezi katika maeneo tofauti tofauti ili herman na kundi lake wakitaka kufanya lolote awe amesha jua kabla lakini walifanya kosa kubwa sana kwamba wali wadharau kuwa hawawezi kuingia kwenye mtandao wao kama hawana black box kumbe ile chip waliobadilishiwa ilokua inahamisha taarifa zote na kuzipeleka kwa big tunchii ambeye alikua anazibadilisha au kuwapa taarifa za uongo.
Mzee muller alisha lipwa nusu pesa na Krit jaa na nusu iliyobaki alikua anaisubiria itaingia baada ya muda mfupi ujao.
Meli kubwa iliyokua na bendera ya afrika kusini ilingia ndani ya bandari ya Bangkok Thailand chini ya ulinzi mkali wa kampuni binafsi ya ulinzi ikiongozwa na Vladimir kochenco taratibu kontena la lililo jaa dhahabu lilishushwa na kupakiwa kwenye lorry kubwa tayari kusafirshwa kwenda kwa krit jaa mwenye mali yake mzigo ilipimwa na kuonekana ni uleule walio kubaliana ndipo alipikamilisha malipo kwa mzee muller.
Lorry lililobeba mzigo lilipo toka tu nje ya eneo la bandari lilipigwa kombora zito na kontena likaanguka pembeni ndipo kundi la double B walipouteka mzigo na kutokomea nao kusiko julikana na kwenye vyombo vya habari kutangazwa kuwa mzigo wa magendo unao semekana kuwa ni silaha za nyuklia umeingizwa nchini Thailand na wahusika wanatafutwa na vyombo vya usalama.
Mzee muller aliona mchezo mzima kwa njia ya setilaiti na kumuambia Vladimir kochenco na timu yake waondoke na mzigo uliobaki na Waendelee na safari iliyo baki ya Hong Kong na China, lakini kichwani alijiuliza nani aliyevujisha siri maana asingetumia akili kidogo tu angekosa vyote madini na pesa.Wazo likamjia kua lazima herman atakuwa na uwezo wa kupata taarifa zao kwa kutumia ile black box aliyo warudishia.

Maneno ya vitisho na hasira yalimtoka krit jaa akimtaka mzee muller amrudishie pesa zake lakini alikataa, ndipo herman alipo ongea ma Jaa na kumueleza jinsi alivyoibiwa na mzee muller na kumwambia bado kuna mizigo mingine ipo kwenye meli inapelekwa China na Hong Kong kwa hiyo kama yupo tayari waungane na kuwatafuta majasusi watako uteka huo mzigo hukohuko baharini.
Baada ya double B kukamilisha zoezi alipewa malipo yake na Herman alichukua kilichobaki na kumpa dili jipya la kuiteka meli yenye madini baharini ikielekea china.
Tayari majasusi walikua wamesha patikana walikodisha nyangumi ya kivita(submarine) na kuanza kuifukuzia meli iliyokua katikati ya bahari ili waiteke na kupora madini chini ya uongozi wa kamanda double B ambaye alikua anafanya kazi akishirikiana na herman ambaye alikua Tanzania anatibu majeraha aliyoyapata toka kwa baba yake mzazi na huku upande wa pili tajiri krit jaa alitoa pesa kidogo kwa ajili ya kuhakikisha mambo yanaenda sawa kila kundi lilikua na malengo na sababu zake.
Nyangumi (submarine) ilikua tayari ipo kwenye usawa kwa kuishambulia meli iliyo beba madini ikiwa chini ya usimamizi wa Vladimir kochenco.

UNAJUA NINI KILITOKEA HAPO KATIKATI YA BAHARI
************ITAENDELEA ***********
USIKOSE
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom