Serengeti: Tumekosa mtetezi, hatuna mbunge.

don-oba

JF-Expert Member
Dec 8, 2011
1,387
677
Kwa muda mrefu sasa jimbo la Serengeti ni kama vile halina mbunge. Pamoja na kuwa na rasilimali nyingi za kitalii watu wa Serengeti bado wapo kwenye ufukara mkubwa. Dr Kebwe akiwa anachangia muswada wa sheria ya fedha leo hii ameshindwa kuchangia na kuonesha jinsi wananchi wa Serengeti wananufaika ktk pato la utalii. Vijiji kama NATTA, ISENYE, MOTUKERI, NYAKITONO, BURUNGA, IKOMA nk hawawezi kulima tena kutokana na tembo kuvamia mashamba yao. Hoteli kubwa kama V.I.P ambayo wageni wanalala kwa USD 1500 per day imeshindwa hata kujenga miumdo mbinu ya maji kandokando ya vijiji vinavyoizunguka. Kebwe amekuwa mbunge wa Dar es salaam tangu tumemchagua hajawahi kanyaga NATTA na maeneo mengi jimboni kwake. 2015 kwaheri Dr Kebwe, tulifanya makosa kukuchagua sasa tunajuta!.
 
Back
Top Bottom