Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,410
Mama mmoja Mgesi Juma (20) mkazi wa kijiji cha Kazi, kata ya Manchira wilayani Serengeti ambaye amejifungua watoto wawili,mmoja amefariki kutokana na kilichodaiwa kuwa ni uzembe wa Mganga wa zahanati ya kijiji Rwamchanga aliyefahamika kwa jina la Miriam Martin.
wakizungumza na waandishi wa habari waliofika kijijini hapo kwa ajili ya kufuatilia tukio hilo,mwenyekiti wa kijiji hicho,Samwel Fransic pamoja na mkunga wa kijiji hicho,Christina John wanaelezea tukio hilo.
Akizungumza tuhuma za mganga huyo Mkurugenzi wa Halmashauri wa wilaya hiyo,Naomi Nko amesema tayari ofisi yake imeshapokea malalamiko ya mganga huyo na tayari ameshamchukulia hatua ya awali ya kumsimamisha kazi wakati akisubiri taratibu nyingine za kisheria .
Akiongea kwa njia ya simu kuhusiana na tukio hilo Kamanda wa Polisi mkoa wa Mara ,Ramadhani Ngh’azi amesema jeshi hilo linamshikilia mganga huyo kwa uchunguzi zaidi ili kubaini kama kweli alizembea na kusababisha kifo cha mtoto huyo na endapo itabainika atafikishwa mahakamani ili kujibu tuhuma zinazomkabili.
Hata hivyo baadhi ya wananchi wa kijiji hicho wamewaeleza waandishi wa habari kuwa mganga huyo alikuwa ameshakataliwa kijijini hapo na tayari walikuwa wameshakaa mkutano wa kumkataa kutokana na vitendo vyake vya kutozingatia maadili ya kazi yake