Serekali ziangalieni hizi MFIs na Financial Services company kuhusu Mikopo

Mnyonge wa Wanyonge

New Member
Feb 8, 2017
3
0
Naiomba Serekali kuziangalia kwa jicho la karibu sana hizi kampuni zinazotoa huduma za kifedha.Hii mikopo ya DHarura wanayotoa imekuwa Mwiba na Imewaumiza watanzania walio wengi.
Kwanza kumekuwa na Tabia ya Watanzania wengi wasio na Makampuni ,hawalipi Kodi bado nao wanakopesha tena kwa riba kubwa.Hii sio sahihi kabisa,kama Unataka kufanya biashara hiyo, fuata taratibu husika, lipa Kodi,fungua Ofisi ili na wewe uweze kuchangia katika pato la Taifa na kufuata taratibu za Mamlaka Sahihi.
Pili haya Makampuni yanayotoa mikopo ya Dharura,nani anaziangalia,Maana Riba 30% kwa mwezi, 25% kwa mwezi.Yani kwa Mwaka ni 360% au 300% bado kila mwezi ukichelewa kulipa una interest kwenye riba ya 3% au 5%.
Watanzania walio wengi wameingia huko,wameshindwa kulipa na mali zao walizochuma kwa miaka mingi zinachukuliwa ndani ya miezi michache.Tunaomba Wizara husika iliangalie hili,wao wanakopa kwenye Mabenki kwa riba ndogo 24 kwa Mwaka au 21% kwa mwaka na kuwakopesha wenzao kiasi kikubwa namna hii.
Tunapenda wakopeshe watu lakini kwa Riba iliyo ya haki na usawa.wanapata Super normal Profit huku waliokopa wakirudi kwenye lindi la umasikini.Wanafanya Biashara halali lakini tunaomba mamlaka husika ziwasimanie na kupanga riba stahiki ya juu na ya chini katika eneo hili.
Leo watanzania wengi wamekuwa watumwa katka maeneo yao kwa ajili mikopo hii hailipiki.
kwa Mfano.Ukikopa 1,000,000 utalipa gharama za mkopo kwanza,utarudisha 1,300,000/= kwa mwezi, ukishindwa mwezi ujao utatakiwa kulipa 1,600,000/= plus 3 0r 5% ya laki 300,000 .
Watanzania wanataka Mikopo lakini mikopo Rafiki itakayowainua kutoka sehemu moja kwenda nyingine,Hili lisipoangaliwa vizuri watanzania wanaumia,wanadaiwa na wengi wamekimbia hata makazi yao.Walikopa kwa nia njema na matumizi sahihi walio wengi ila kiuhalisia mkopo riba ni kubwa na kulipa inakuwa ngumu mno
Mamlaka tusaidiane kuwe na fair ground ili tuweze kuinuka kiuchumi na kuishi kwa amani katika nchi yetu,Mungu ibariki Tanzania,Mungu .
 
Kwan mkiendaga kukopa hamuelezwi jins malipo yanavyotakiwa? Mpka ukubali kuchukua mkopo wao ina maana unakubaliana na masharti yao
 
Kwan mkiendaga kukopa hamuelezwi jins malipo yanavyotakiwa? Mpka ukubali kuchukua mkopo wao ina maana unakubaliana na masharti yao
Watu wanakopa huko maana altenartive ni chache,Mabenki mengi sasa yanapokea deposit n kukopesha kidogo au hawakopeshi kabisa .Hapa tunatetea Watanzania wenzetu, Shida haina mwenyewe,Wizara ya fedha Ihakikishe inaregulate makampuni haya,Leo Mabenki yangekuwa hayako chini ya Benki kuu na hakuna wakuwafuatilia,Riba zingekuwa juu,Charges pia,Wasipozibitiwa ni shida kwa Taifa na jamii pia
 
Iringa microfinance, wapo jengo la imucu iringa,hawa hutoza riba 50% na hawalipi kodi,mamlaka husika hebu fuatilieni hawa watu ili walipe kodi na wafuate taratibu za ukopeshaji.
 
Afadhari mkope huko mlizoea kwetu ati ndugu yangu niazime laki kadhaa baada ya wiki nitarudisha... Nyambafu hadi miaka inaisha mnageuka Adui wakati ni rafiki au ndugu... Hiyo ndio kiboko mtie akili ya kuibia watu jasho... Siku hizi mtu akiniomba mkopo jibu ni live Sina. Akikomaa nikopee kwa mtu namtukana kimya kimya and then namuambia bank na taasisi zipo
 
Back
Top Bottom