Serekali yetu inasikitisha sana

nahavache

JF-Expert Member
Apr 3, 2009
871
246
Tuliambiwa na serekali yetu kuwa ni sikivu, lakini madakitari wamegoma serekali inatoa vitisho. Ni kweli JK ambaye alituthibitishia kuwa serekali yake ni sikivu hatambui habari ya huu mgomo?

Siamini. Pinda, unataka uwapeleke madakitari kazini wakiwa na kwenye low mood kwa kuwalazimisha? Pinda, Spika wanapotofautiana na ikulu kuhusu posho za wabunge, ina mana raisi hakuwasiliana na wenzake kuhusu posho?

Kama kweli JK hajaidhinisha nyongeza ya posho ambazo tayari Spika amesema kuwa zishaanza kulipwa, basi hawa jamaa hawawasiliani. Ukikumbuka suala la Jairo, suala la Richmond, na mengine mengi ambayo wakuu wanatoa matamko yanayotofautiana, Jeshi la polisi lina ushahidi wa ugonjwa wa Mwakyembe lakini Waziri mwenye dhamana ya mambo ya ndani hajui, hii serikali inasikitisha.

Kila mtu pale anafanya lake. Waondoke haraka kwa sababu nina wasiwasi watatuachia hata viti vilivyochakaa. Hawako pamoja, wanadhalilishana tu. hakuna uongozi
 
Wabunge wamenza kozi ya udaktari wa mtindo wa maji mafupi. wakitoka Bungeni Mahospitalini. Ila mimi sitaenda huko.
 
Back
Top Bottom