Naomba nianze kuelezea mifano ya hizi propaganda katika makundi mawili:
1. Rais - Kila mmoja wetu anajua katika katiba yetu rais amepewa madaraka makubwa sana ya kimaamuzi na kiutendaji. Haiingii akili kuona mtu huyu huyu tuliyemwezesha akilalamika juu ya udini, ukabila, rushwa na mengine mengi. Kwanini asitumie mamlaka aliyopewa kikatiba kushughulikia haya matatizo?Anapolalamika sisi tusio na meno/makali tufanyeje?. Inabidi ifike mahali watanzania wenzangu tuseme sasa yatosha na tuwaumbue hawa watu kwa hoja. Tunataka vitendo na siyo kulalama.
2. Chama Tawala - Tumeona viongozi wa ngazi za juu kwenye chama chenye dola wakilalama kwenye mikutano ya siasa na mingine juu wa kuwepo kwa chama/kundi la watu wanaopanga mauaji, wanaochochea udini, ukabila na mambo mengine mabaya. Kama watanzania wamewaamini au mlifanikiwa kuiba kura na leo mmeshika dola kwanini mnashindwa kuwashughulikia hawa watu kwa mujibu wa sheria hadi mnalialia kwenye mikutano, social medias, n.k? Hivi mnafikiri sisi watanzania hatujua kupembua na kuchambua mambo?Hizi propaganda hazitufai kwa miaka hii na karne hii. Tunataka vitendo na siyo propaganda chafu na outdated
Mimi nadiriki kusema hizi propaganda ndiyo zinachochea ukabila, udini, chuki, rushwa na mambo mengine mabaya. Kimsingi hizi propaganda ni kansa ambayo inaendelea kulitafuna taifa hili na kibaya zaidi zinapaliliwa na viongozi tuliowaamini na kuwapa dola.
Naomba nimwombe Mdogo wangu Mwigulu na Nnauye waje hapa wajibu hii hoja kiyakinifu na siyo kwa jumla jumla kama tulivyowazoea maana hawa wawili wako kwenye kundi na2 hapo juu
Asante
Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums