Ndugu watanzania mfumo wa siasa za vyama vingi ni mfumo wenye lengo la kuleta ushindani katika siasa ili wananchi washindane katika kutafuta mawazo ya kutatua changamoto za jamii na kuleta mawazo hayo kwa wananchi ili wachague yale wanayoyaona bora kwa wakati huo.
ni kwa bahati mbaya sana watanzania kwa ujumla sisi bado ni wachanga sana katika siasa kwa maana ni rahisi sana kwa mtoto mdogo kupata tatizo leo baadae akipata suluhisho kesho asahau tatizo la jana kama lipo.
Utu uzima ni ukomavu wa kifikra ambao unamfanya mtu akikumbana na changamoto mara moja anajifunza muhimu kutokana na changamoto hiyo
1. ni changamoto gani inayomkabili
2. changamoto hiyop imesababishwa na nini?
3. ni njia gani za kuepuka au kukabiliana na changamoto hiyo.
ukifuatilia tumepitia wapi katika siasa zetu tangu tumepata uhuru unaweza kuona kuna mifumo ya siasa tuliyoipitia ambayo tunaenda tunairudia rudia. Kurudia rudia mifumo hii bila kujifunza kupitia tuliyoyapitia huko nyuma ili hayo yasijirudie tena ndio sababu ya kusema kwa mtizamo wangu watanzania sisi bado wachanga sana.
mfano
miaka ya 60 mpaka 70 tulikuwa na mfumo wa vyama vingi Tanzania na mwaka 1977 tuliachana rasmi na mfumo wa vyama vingi tukaingia kwenye mfumo wa chama kimoja.
Tujiulize hivi kuna mtanzania anajiuliza ni kwa nini tulitoka katika mfumo wa vyama vingi na kuingia katika mfumo wa chama kimoja?
Binafsi sio mwana historia lakini kwa historia ndogo niliyofundishwa kuanzia shule za msingi sioni popote inapozungumzwa sababu bali elimu yetu ya historia na siasa zimejikita katika kunukuu tarehe, majina ya wahusika na mahali tukiona lilipotukia. hakuna kinachozungumzia nini kilikuwa kinaendelea, kilileta changamoto gani na suluhisho kwa wakati huo ilionekana ni nini na je baada ya kufuata hilo lililoonekana suluhisho kwa wakati huo nini kilifuata, je tulitatua moja kwa moja au tulitatua tatizo moja na kuzalisha mengine au ilikuwaje?
binafsi nimeamua kujikita katika mambo yaliyokuwepo enzi hizo na kutafuta chochote kinachoweza kunipa dondoo.
Niliporejea katika ahadi za mwana TANU nimekutana na ahadi ya 8. inayosema "Nitasema kweli daima fitina kwangu ni mwiko"
Je ahadi hii inaweza kutuonyesha kitu gani enzi hizo?
mfumo wa vyama vingi unalenga kuleta ushindani katika siasa, watu washindane kutafuta mawazo bora ya kusaidia jamii lakini katika siasa huku kuna vyeo na mali hivyo kuperekea wananchi kuanza kutumia mbinu zozote kujipatia mali au vyeo. Inaonekana wananchi walikuwa wako tayari kuzungumza uongo kwenye siasa ili wachaguliwe, wanasiasa walikuwa wako tayari kuwatengenezea wananchi wenzao fitina ili wao wasichaguliwe.
ni wazi inaonekana siasa zilikuwa zikipoteza mwelekeo kwa watu kugombania vyeo na mali badala ya kushindanisha hoja.
katika kukabiliana na hili walianza na ahadi za mwana Tanu ili kuwadhibiti wananchama wa chama cha Tanu wasijiingize katika biashara hiyo.
Ni jambo ililowazi kuwa ahadi za wanachama wa chama kimoja zisingeweza kudhibiti mfumo wa siasa wa nchi nzima hivyo waliona enzi hizo mfumo wa vyama vingi hauleti ushindani unaoweza kuwaletea wananchi maendeleo bali malumbano, udanganyifu, kufitiana ambavyo badala ya kuchochea maendeleo vilidumaza.
Mwaka 1977 tukaingia mfumo wa chama kimoja
wakati tumeingia mfumo wa chama kimoja tuliamini kwa kuwa tumekabiliana na "kusema uongo pamoja na fitina hivyo sasa wananchi watajikita katika kujiletea maendelea bila vikwazo "deceptions"
Kumbe La hasha! baada ya kuondoka adui fitina na uongo akajitokeza adui mwingine ambaye alikuwa ni ni "umimi"
hapa wanasiasa walijiona kama wao ndio alpha na omega, walijitambua kuwa wananchi hawa mbadla hivyo wafanye vibaya au vizuri sio kigezo cha wao kuondolewa au kubakizwa kwa maana hawashindani na mtu. Maamuzi ya siasa katika kipindi hiki yalilenga maslahi ya watu wachache waliokuwa kwenye siasa au wenye ushawishi na sio kutazama jinsi ya kumuinua mwananchi mnnyonge.
Mwaka 1993 tukarejea mfumo wa vyama vingi
Kutokana na yale tuliyoyapitia katika mfumo wa chama kimoja tuliona mfumo wa vyama vingi hauepukiki. miaka ya 90 tukarudi kwenye mfumo wa vyama vingi.
Jambo moja mbalo hatukufanya likionyesha kwamba sisi tu wachanga katika siasa ni kutotumia uzoefu wetu wa mfumo wa siasa za vyama vingi katika miaka ya 60 na 70 kutunga kanuni zitakazotusaidia kuelekeza wanasiasa wetu wajikite katika kutafuta mawazo bora ya kusaidia wananchi kutatua changamoto na matokeo yake ni kuanza kuonyesha dalili za kutaka kurejea kwenye "uongo na fitina za miaka ya 60 na 70" katika kugombea madaraka na mali.
Msimamo Wetu kama chama cha upinzani
1. Ni jukumu la serikali kuchambua historia yetu tulikopitia na kuwafundisha watoto wetu historia sahihi yenye mafunzo waliyoyapitia katika maisha yao, na sio mfumo wa sasa wa kukalili tarehe, majina, mahali bila kufahamu undani wa historia yetu, tulikuwa na changamoto gani huko nyuma, tulitumia njia gani kuzitatua, na je baada ya kufanya maamuzi tuliyofanya tulifanikiwa kwa kiwango gani au tulikumbana na yapi tena.
2. Mfumo wa vyama vingi ndio mfumo pekee unaoweza kuwadhibiti wanasiasa wetu kuwatumikia wananchi hivyo kwa kiongozi yeyote anayependa maendeleo endelevu ataweka mazingira ya kustawisha mfumo wa vyama vingi ili mfumo huu utengeneze wanasiasa makini katika nchi yetu katika vyama vyote vya siasa. Tujifunze kupitia kwa mwalimu Nyerere, aliipenda sana nchi yetu, alichukia sana dhuluma, rushwa n.k. mwalimu Nyere alipenda sana maendeleo ya nchi yetu lakini alipotoka madarakani na kuwaachia wengine sina imani kama aliowaacha walitenda kama yeye alivyotaka.
ni kwa bahati mbaya sana mwalimu Nyerere wakati anaondoka madarakani aliacha ameweka mfumo wa chama kimoja ambao hata wananchi wenyewe hawakuwa na mbadala wa kusema labda tunaona mnatoka kwenye misingi aliyotujengea mwalimu. Ni watu walewale, wanafanya maamuzi wenyewe hata mkienda kwenye uchaguzi wanachaguana wenyewe na hamna namna.
3. Upinzani sio kupinga kila kitu kinachofanywa na serikali, hii ni tafsiri potofu ya watu wasioelimika! Upinzani ni kuwa na njia mbadala ya kutatua changamoto za wananchi ambazo yapo maeneo njia hizi na za watawala zinaweza kukutana, yapo maeneo njia hizi zinaweza kutofautishwa na speed kuwa nyote mnapitia njia moja lakini hawa speed yao ni yakasi zaidi na hawa kwa spidi yao watabuluzwa nyuma tu, lakini pia yapo maeneo kila mmoja anaweza kupita njia yake. Kikubwa mwisho wa siku ni nyote mnatakiwa kukutana katika sehemu moja ambayo ni kuona jamii ya watanzania wakipiga hatua kutoka hali ya maisha ya chini kwenda juu kadiri mda unavyopita.
Sera zetu kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu 2020
1. kwanza kabisa wapinzani tunapenda kuipongeza serikali ya awamu ya 5 kwa utendaji waliouonyesha tangu wameingia madarakani katika nyanja ya uchumi kwa kutizama matokeo. wamebadili utendaji wa watumishi katika serikali na sekita binafsi.
Serikali ya awamu ya tano imedhibiti upotevu wa fedha za umma ambazo zilikuwa zikitapanywa ovyo na waliokuwa wakipewa dhamana.
serikali imetekeleza miradi mingi ya maendeleo ambayo huko nyuma haikuwezekana kutokana na nidhani ya fedha na watumishi wenyewe
Lakini katika hili la utendaji wa serikali ya awamu ya 5 shukrani za pikee ziende kwenye mfumo wa vyama vingi. Watanzania bila kuwa na mfumo wa vyama vingi ni wazi tusingepata serikali hii tunayoiona leo. mambo yangekuwa yaleyale ya watu wachache kupeana madaraka, kiongozi akifanya kosa badala ya kutumbuliwa inaundwa tume inayokuja kumsafisha, ili uwe kiongozi ni lazima ujuane na wakubwa n.k
mambo yaliyokuwa yakitendeka huko nyuma wananchi waliona na baada ya kuingia mfumo wa vyama vingi wananchi walionyesha kukerwa na ndio ikapelekea mifumo ya zamani kuvunjika na watu wenye kuwapenda wananchi na waliko tayari kuwatumikia wananchi kwa sifa zao ndio wakaonekana ndio njia pekee ya kubaki wakiaminiwa na wananchi hivyo watanzania wote tuuenzi mfumo wa vyama vingi kwani unaweza kuwa mbadala wa kumdhibiti yeyote anayeweza kutaka kuturudisha katika sera tulizoachana nazo
Kuenzi mfumo wa vyama vingi ni kwa watu wenye sifa kujitokeza katika vyama vyote na wananchi walinganishe sifa za wagombea na sio kupiga kura kwa kutazama mtu anatoka chama gani
2. mbali na kuipongeza serikali kutenda vizuri katika maswala ya uchumi bado sisi tunaona kuna maeneo mengi ambayo yanahitaji kurekebishwa ili kuyaenzi kwanza yanayofanywa leo lakini kufanya na mengine mengi kwa wakati huo. Haya wanayofanya watawala leo ndiyo hayo sisi tuliyapigia kelele siku nyingi na yanapofanyika sisi tunafarijika lakini kwa uchache mkitupa nafasi tunalenga kufanya zaidi ya haya kwa mfano
a) Wawakilishi wetu bungeni.
sisi wapinzani haturidhiki na mfumo wa sasa wa uwakilishi bungeni. Mtu anachaguliwa na wananchi kuwa mwakilishi wao, yuko dar es salaam anafanya biashara zake, ukifika mda wa bunge anatoka kwenye biashara zake anakwenda bungeni kuchangia mawazo yake na tunamlipa fedha nyingi tu. Hivi hawa wanafanya kazi gani hasa?
Wananchi mkitupa kura tupata wawakilishi wa kutosha kufanya maamuzi bungeni tunalenga kubadilisha sheria ili mbunge awe ni mfanyakzi katika ofisi ya mbunge iliyoko jimboni kwake. Mwananchi anapokutana na changamoto, iwe kukosa huduma ofisi ya umma, iwe kunyanyaswa, iwe ni changamoto ambazo serikali inatakiwa kushughulikia basi anaenda kuipeleka kwa mbunge. Lakini pia mbunge huyu akae afuatilie utedaji wa serikali katika jimbo lake, kama ni miradi ya maendeleo afuatilie na kusimamia, kama ni watumishi wa umma afuatilie, kama ni matumizi ya fedha za serikali afuatilie.
mtizamo wetu wa uendeshaji wa bunge kwa sasa tunaona ni kama "debate" tulizokuwa tukifanya mashuleni kuwa watu mnakusanyika kila mmoja ana weza kuamua kuchangia kwa kusapoti mada au kupinga mada. Sisi tunasema wabunge wanatakiwa kuwa watendaji, mbunge alipwe mshahara kuwa mtendaji na tunaamini tutaweza kuleta mabadiliko makubwa kama tutakuwa na wabunge watendaji ambao wanalipwa kufuatilia changamoto za wananchi na kuwasemea wananchi
b) makazi
Sisi tunaamini msingi wa kwanza wa maendeleo ni utaratibu bora wa makazi
miaka ya 70 mwalimu nyerere alidhamiria kuweka mpangilio mzuri wa makazi mpaka vijijini ili awahudumie. Leo hii mpaka miji inakosa udhibiti. Waziri mwenye dhamana anahangaika na kutatua migogoro ya hati, walionyanganyana mashamba n.k.
Sisi tunaamini tatizo kubwa la makazi ni uholela na uholela huu unasababisha maisha ya watanzania kuwa magumu sana wakati rasilimali zilizopo zingeweza kuwahudumia wakapata maisha ya juu kulinganisha na ya sasa.
Sisi tunasema waziri wetu wa ardhi na makazi tutamwambia tunataka mpango wa miaka 15 ambao utahakikisha
1. hakuna nyumba ya tope katikati ya mji wowote
2. Miaka 20 ikipita ya utekelezaji hakuna nyumba mjini itakayokuwa haina access ya barabara
3. miaka 20 ikipita mwananchi asitembee zaidi ya mita 500 bila kufikia public transport
4. miaka 20 ya utekelezaji ikiisha, mwananchi asitembee kilomita zaidi ya 1 kufuata shule, soko, hospitali
5. miaka 20 ikipita mwanachi asikatize kiwanja cha wazi kwenda nyumbani kwake, hapa tunalenga kutokomeza watu kununua ardhi kuweka ili bei zikipanda wauze huku wakati wameweka wananchi wa maeneo hayo wanapata adha kubwa kimaisha. Nunua kiwanja unapotaka kujenga na jenga.
6. Tunataka plani za kubadilisha miji tuliyonayo kwa sasa na sio mipango ya kukopa benki ya dunia mabilioni kuanzisha miji mingine. Planning kwenye miji yetu hii iliyovurugika. Wape watu ndani ya miaka kadhaa wanatakiwa nyumba zao ziwe zimefananaje ili wajipange na kuanza kubadilisha taratibu. wale watakaopitiwa na public services ambazo hazipo katika maeneo haya tuko tayari kuanzisha kodi ya kurekebisha miji yetu
7. watu wa vijijini nao tunalenga wawe na makazi yaliyokaa pamoja kama centers ili wapate huduma kwa urahisi kwa pamoja. Huduma za kijamii zikifikishwa kwenye center ni rahisi wote kuishi maisha bora huku wakienda maeneo ya nje na makazi yao kulima.
Usafi wa mazingira
Tutafuta mipango ya sasa ya kufunga biashara kila jumamosi, sijui alihamisi eti ili kufanya usafi. Usafi kwetu sisi itakuwa sehemu ya maisha ya watu. Sheria za usafi zita ainisha kila mwananchi anawajibika kufanya usafi mpaka wapi?
Haiwezekani mtu anaishi siku zote anatupa uchafu kwenye mtaro uliko mbele ya nyumba yake alafu ikifika alihamisi eti tunamwambia afunge biashara na kusafisha mtaro huo. Mbaya zaidi ni kwa yule anayeishi maisha ya usafi maana kama mtaro wako uko msafi na mazingira yote ni masafi ukafungua biashara wewe unakuwa criminal kuliko anayetupa uchafu kwenye mtaro na siku ya alihamisi akafunga biashara kusafisha mtaro, Hizi nisheria kipofu.
sisi kupitia halmashauri tutaanzisha kampeni za miji ya kijani. halmashauri zote zitawawezesha vijana na wanawake kuzalisha miti, maua, ukoka kwa gharama nafuu kupitia mikopo ya makundi haya. Hamlashari hizi zitatoa michoro ya bustani na idadi pamoja na aina ya miti kwa kila mtaa ili kuwepo na uniformity ki mitaa.
Jukumu la mwananchi itakuwa ni kuchukua vifaa kutoka vijana wa halmashauri bure, mtapewa ushauri, kazi yao ni kupanda na kuhudumia. Serikali itakuwa na wakaguzi wa kukagua utekelezaji na si swala la kufunga shughuli zako. kama unaona unaweza kuweka mtu akufanyie sawa, kama unafanya mwenye sawa, kwa mda gani ni jukumu lako bali mkaguzi wa serikali akipita akute mazingira yako yako katika hali iliyotolewa mwongozo
Ajira
Sisi tunaamini mfumo wa sasa wa ajira unatakiwa kubadilika lakini kwa kifupi tutaanzisha utaratibu kwa kila idara, kila kazi tunataka kuona generations tofauti ambazo zitazalisha ajira nyingi zaidi kwa watu wetu na kutengeneza vizazi vinavyorithishana maarifa.
katika ajira yoyote tutaweka utaribu wa kuona
1. Exoperienced personel working with
2. Juniors
haiwezekani unafika sehemu leo unakuta mtu amekwisha staafu amepewa ajira tena analipwa mshahara huku graduate yuko mtaani miaka 3 hana hata pa kujitolea. Au unakuta graduate anafanya kazi hana mtu anayemuongoza ili ajue haraka kuwa hapa tunatakiwa kufanya hivi.
Ni lazima kila mwenye uzoefu afanye kazi na mtu asiye na uzoefu sio chin i ya mmoja ili kile alichokikusanya miaka yake yote ya uzoefu akiache kwa hawa siku hawezi kufanya kazi.