Sera za wagombea CHADEMA Serikali za Mitaa

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,991
20,312
Hizi ni sera nilizowaandalia wagombea wa mtaa wangu wa Mbutu Kigamboni, Jana tumezindua kampeni kwakutumia sers hizi,kwa jinsi wananchi walivyozipokea tunauhakika wakushinda kwa asilimia mia kabisaaaa.

Kwa makamanda wote mnaogombea serikali za mitaa, tumieni sera hizi kama zinawafaa kulingana na mahitaji ya huko mliko.
Ziboresheni ziendane na mazingira yenu.

.........................................................................................................................................
SERA ZA CHADEMA UCHAGUZI WA SERIKALI YA MTAA WA MBUTU.

Chadema tunasimamia sera zetu kama ilivyo kwenye ilani ya uchaguzi uliopita wa 2010. Na katika uchaguzi huu wa serikali ya mtaa wetu wa Mbutu, Chadema tunasimamia mambo yafuatayo.
ELIMU BURE
AFYA BURE
MAJI SAFI NA SALAMA
MIUNDOMBINU (BARABARA NA UMEME)
MENGINEYO


HATUA ZA UTEKELEZAJI

1.MAJI SAFI NA SALAMA

Chadema tumeandaa utaratibu kwakutumia raslimali watu, tutachimba visima vya maji safi na salama katika vitongoji vyote vya mtaa wetu wa Mbutu, Hili tayari rafiki zetu wahisani wameshakubali kutusaidia kuchimba visima virefu vinne na majenereta makubwa manne. Kuanzia mwezi wa kwanza tatizo la maji Mbutu ambalo ccm wamewadanganya kwa zaidi ya miaka hamsini tangu Uhuru litabaki kuwa histori.

2. ELIMU BURE (HAKUNA MICHANGO)

Ndugu zangu wanamtaa wa Mbutu, naomba mtambue kwamba Wizara ya Elimu nchini huwa inatoa ruzuku ya shilingi 25,000 kila baada ya miezi mitatu kwa kila mwanafunzi wa shule ya msingi Tanzania kwaajili ya madaftari, mitihani, twisheni na ulinzi. Lakini hela hiyo haijawahi kuwafikia watoto wetu hapa Mbutu badala yake imekuwa ikiishia mikononi mwa mafisadi wa CCM kuanzia Wilayani, Kata na ccm ya hapa mtaani.
Ndugu zangu wanamtaa wa Mbutu, leo mtakuwa mashahidi wenyewe, wazazi wetu mnachangishwa kila kukicha michango ya mitihani, twisheni, madawati nk. Sasa Chadema tumekuja na suluhisho la matatizo yenu. Kutokana na hali hii ya CCM kuendelea kuwanyonya wananchi kwakuendelea kuwachangisha wazazi michango kwaajili ya mitihani, twisheni na michango mingine, sisi Chadema tunatangaza kuwa tukiingia tu madarakani TUTAIFUTA michango hiyo mara moja.
Tutahakikisha ruzuku yote inawafikia walengwa ambao ni shule yetu ya Mbutu. Chadema tutafungua akaunti maalumu ya Benki kwaajili ya elimu Mbutu. Hivyo kama kuna ulazima wakuiboresha ruzuku, michango yote ya Mitihani, twisheni au mlinzi itatoka kwenye akaunti hiyo maalumu ya serikali ya mtaa. Michango yote italipwa na serikali ya mtaa iliyo chini ya chama chenu pendwa Chadema bila kujali itikadi za vyama, dini, rangi au kabila

3. AFYA BURE

Ndugu zangu wanamtaa wa Mbutu, naomba mtambue kwamba Wizara ya Afya nchini huwa inatoa ruzuku ya shilingi milioni tatu (3,000,000) kila baada ya miezi mitatu kwa kila kata Tanzania ikiwemo kata yetu ya Somangila kwaajili ya huduma za afya kwenye zahanati.
Pesa hii huwa anapokea Diwani wa kata husika, Lakini hela hiyo haijawahi kuwafikia hapa Mbutu badala yake imekuwa ikiishia mikononi mwa mafisadi wa CCM kuanzia Wilayani, Kata na ccm ya hapa mtaani. Kutokana na tabia ya chama cha mapinduzi ccm kuendelea kuwanyonya wananchi kwakuendelea kuwachangisha wanachi michango kwaajili ya matibabu na michango mingine,
Sisi Chadema tunatangaza kuwa tukiingia tu madarakani TUTAIFUTA michango hiyo mara moja na tutahakikisha ruzuku hiyo inafika kwenye zahanati yetu. Chadema tutafungua akaunti maalumu ya AFYA ktk Benki kwaajili ya AFYA Mbutu ili kuboresha huduma za afya Mbutu. Hivyo michango yote ya Matibabu au mlinzi itatoka kwenye akaunti hiyo maalumu ya serikali ya mtaa ikiwa ruzuku itachelewa. Michango yote italipwa na serikali ya mtaa iliyo chini ya chama chenu pendwa Chadema bila kujali itikadi za vyama, dini, rangi au kabila.

4. MIUNDOMBINU (BARABARA NA UMEME)

Ndugu zangu wanamtaa wa Mbutu, naomba mtambue kwamba jukumu la miundombinu na huduma nyingine za kijaimii ni la serikali yoyote iliyopo madarakani. Wizara ya TAMISEMI nchini huwa inatoa ruzuku ya shilingi milioni tatu (3,000,000) kila baada ya miezi mitatu kwa kila kata Tanzania ikiwemo kata yetu ya Somangila kwaajili ya huduma za Barabara katika mitaa. Naomba muelewe Pesa hii huwa anapokea Diwani wa kata husika, Lakini hela hiyo haijawahi kuwafikia hapa Mbutu badala yake imekuwa ikiishia mikononi mwa mafisadi wa CCM kuanzia Wilayani, Kata na ccm ya hapa mtaani. Chadema tunawaahidi kuwa tukiingia madarakani tutahakikisha ruzuku hiyo inafika hapa na kulima barabara zote za mitaa na kuweka changarawe/moram ndani ya mwezi mmoja tangu tuingie bila kujali dilni au kabila.
Pia tutahakikisha umeme unafika Mbutu hasa kwenye zahanati yetu na kwa wananchi wote. Chadema tunajivunia kwakuwa kupitia kamanda wetu YERICKO NYERERE, tayari tumeshawajengea daraja lenye thamani ya milioni kumi na sita (16,000,000=/) watu wa kitongoji cha Mbarajange waliokuwa wametelekezwa ccm tangu nchi ipate UHURU na sasa wanavuka mto vizuri hata mvua inyeshe namna gani. Mpaka ccm wanapitia kwenye daraja hilohilo kwenda mbarajange kuomba kura.

5.AJIRA

Chadema tunatambua tatizo la ajira ambalo limesababishwa na sera mbovu za ccm, hivyo Chadema Mbutu tunakuja na mwarobaini halisi. Hamuwezi kujikwamua bila kuwa na umoja thabiti, Chadema tutawaunganisha kila aina ya kazi katika makundi yake, mfano wavuvi, wafugaji, wagonga kokoto, wakulima nk. Tumewandalia taasisi za mikopo ambapo serikali ya mtaa itakuwa mdhamini. Pia tumewaandalia masoko ya bidhaa zenu.

MENGINEYO.

TUNAWAOMBA KURA ZENU NDUGU WANAMTAA ILI TUTEKELEZE AHADI ZETU ZA KUWATUMIKIA.
 
Yericko nakupongeza sana, ngoja tuzichukue na kuziboresha kulingana na maeneo ya kwetu.
 
hakika chadema ni mkombozi , wakati sera ya upande wa pili ni kuhakikisha maeneo yote ya wazi yanauzwa kwa wachina , nyinyi mmeamua kuboresha elimu , miundo mbinu na afya ! Asanteni sana .
 
kwa angalizo tu kwa wadau na wapenda mabadiliko mkumbuke kwamba pamoja na yeriko kutumwagia sera hizi ni vizuri mkajua kwamba kila eneo au mtaa au kijiji kina matatizo yake tofauti kwa hiyo nitashangaa kama kila mtu hapa atakopi kama zilivyo ainishwa halafu anazipeleka kwenye eneo ambalo hizo sela hazifiti hata kidogo.
 
Ongeza nyingine apo.HAKUNA MICHANGO YOYOTE KWENYE OFISI ITAYO ONGOZWA NA CHADEMA.Hawa magamba wanatutoaga upepo sana pale unapo enda kwa ofisi ya s.mtaa.Mfano una shida na mhuri wa ofisi ili ukusaidie kuomba mkopo majamaa lazima yakuchomoe.
 
Ongeza nyingine apo.HAKUNA MICHANGO YOYOTE KWENYE OFISI ITAYO ONGOZWA NA CHADEMA.Hawa magamba wanatutoaga upepo sana pale unapo enda kwa ofisi ya s.mtaa.Mfano una shida na mhuri wa ofisi ili ukusaidie kuomba mkopo majamaa lazima yakuchomoe.

hiyo kitu kwa serikali ya cdm ni mwiko .
 
Kuwa na mahusiano ya wazi na wawekezaji,ili kuchangia maendeleo ya mtaa na sio kuchangishwa kwa ajili ya vikao vya chama tu.

Kuweka utaratibu unao eleweka wa uzowaji wa taka na usafi kwa ujumla.


Kuitisha vikao kwa mujibu wa sheria na kusoma mapato na matumizi



Kuwapa wananchi nafasi ya kuibua kero zao na maendeleo yao
 
Kuwa na mahusiano ya wazi na wawekezaji,ili kuchangia maendeleo ya mtaa na sio kuchangishwa kwa ajili ya vikao vya chama tu.

Kuweka utaratibu unao eleweka wa uzowaji wa taka na usafi kwa ujumla.


Kuitisha vikao kwa mujibu wa sheria na kusoma mapato na matumizi



Kuwapa wananchi nafasi ya kuibua kero zao na maendeleo yao

Naaaam naaaaam mkuu pamoja sana!
 
kuwa na mahusiano ya wazi na wawekezaji,ili kuchangia maendeleo ya mtaa na sio kuchangishwa kwa ajili ya vikao vya chama tu.

Kuweka utaratibu unao eleweka wa uzowaji wa taka na usafi kwa ujumla.


Kuitisha vikao kwa mujibu wa sheria na kusoma mapato na matumizi



kuwapa wananchi nafasi ya kuibua kero zao na maendeleo yao

tunakushukuru sana
 
bila kusahau kukomesha wale MCHWA WANAOTAFUNA MAENEO YA WAZI , WALE WANAOSHIRIKIANA NA MADIWANI KATIKA KUMEZA ARDHI YA UMMA .
 
Back
Top Bottom