Sera ya elimu bure jimbo la Nanyamba haitekelezeki

laurent Msembeyu

Senior Member
Oct 5, 2015
121
101
Sera ya elimu bure katika katika halmashauri mpya na change ya Nanyamba haitekelezeki kabisaaaaaa,

Sera hii katika jimbo na halmashauri hii ya Nanyamba haitekelezeki kwa sababu zifuatazo:

1. Halmashauri ni mpya haina uzoefu wowote wa kutekeleza sera za kitaifa
2. Wanainchi wake ni maskini wa kipato kwa hiyo sera inawabwetesha, wazazi wanabweteka
3.Mbunge wake Mh Abdallah Chikota kapata ubunge kimagumashi, kwa hiyo ana inferiority complex, hajiamini, hana uwezo wa kutoa ushauri serikalini kuwaambia ukweli kwamba sera haitekelezeki, na mwisho wa siku itatoa matokeo hasi ,mbunge huyu hana ubavu wa kusema haya.
4. Shule zake mfano shule ya msingi MILANGOMINNE zina mapungufu makubwa kwa hiyo zinzhitaji sana michango ya wazazi
5. Bodi zake za shule hazijapewa mafunzo yoyote ya namna ya utekelezaji wa sera hii kwa hiyo mambo mengi wanakurupuka, hawana uwezo wa kutafisiri maana halisi ya sera hii wanaelewa tofauti,tafisiri yao ni potofu kabisa matokeo yake walengwa hawatopata kile kilichokusudiwa ndani ya sera wataishia kuwa wajinga wanaoenda shule kuongeza umri tu na siyo kupata elimu bora.

USHAURI
Sera hii ingeanza kutekelezwa katika eneo dogo(pilot area) ili changamoto zake ziweze kubainishwa na kuweza kuangalia namna nzuri ya kuzitatua changamoto zitakazojitokeza. Baada kuitekeleza sera katika eneo dogo na kisha kujua matatizo katika utekelezaji na kuyatatua ndipo sera ingetekelezwa nchi nzima.

Na eneo lenyewe dogo liwe halmashauri ya Nanyamba mkoani Mtwara.
 
Back
Top Bottom