Separation of power - Basic structure Doctrine

Joined
May 30, 2020
Posts
67
Reaction score
108
Leo 24/05/2021 nimesikiliza Swali la Pascal Mayalla aliloliuliza IKULU mwaka 2016 kuhusu Mihimili 3 ya serikali kwenye dhana ya separation of Powers; ' ulitoa maagizo kwa mihimili mingine kwa kutumia MAMLAKA GANI?

Katika kupitia pitia maeneo mbali mbali, nimekutana na hukumu ya Mahakama kuu ya NCHI jirani juzi ikimtaja Mkuu wao wa Mhimili mmoja uliojichimbia chini sana kuwa amekosea na amevunja katiba ya Nchi yao aliyoapa kuilinda na kuitetea kwa kuanzisha mchakato wa kuunganisha madaraja ya makabila ya nchi yao (BBI).

Kiongozi huyo ambaye alivunja katiba yao kwa kushirikiana na Kiongozi wa UPINZANI Mkongwe wa mabadiliko Africa Mashariki na Kati na kwa kuwa wametumia fedha za Umma kuendesha mkachakato kinyume cha Katiba, CAG wa Nchi hiyo ameambiwa na mahakama kuwa anaweza kukagua. Aidha, Mahakama hiyo imeenda mbali zaidi kwa kuiambia TUME yao ya uchaguzi na MiPAKA kuwa haina uhalali wa kuendesha KURA ya maoni kwa sababu mchakato ulikuwa batili na kinyume cha KATIBA "President act unconstitutionally if He seek to pre-empt the parliamentary iniated and 'popular iniatives"

Wiki 2 zilizopita tena, MAHAKAMA ya Nchi ya Mzee Mugabe nayo imetoa hukumu kali kwa Mhimili uliojichimbia chini zaidi kwa kusema kuwa Jaji Mkuu wa Nchi hiyo ya Wazalendo ameongezewa MUDA mara baada ya kustaafu kinyume cha KATIBA yao na KIAPO chake kimeisha siku alipotimiza miaka ya kustaafu kama ilivyotajwa. Mahakama hiyo iliend ambali zaidi kwa kukemea kitendo cha walinzi wa Katiba yao kushabikia au kukaa kimya wakati inavunjwa na mtu aliyeapa kuuilinda na kuitetea. Young Lawyers Association of Zimbabwe Dough Coltart as 'Defense Attornry for the Constitution and the rule of law"

Katika kuhitimisha kile ambacho kimenikumbusha Swali la Mayalla kwa aliyekuwa Mkiti wa Chama chetu kuhusu Mamlaka yake ya kutoa maagizo yanayopingana na katiba, nimejikuta natafakati mchakato wa upatikanaji wa wawakilishi 19 wa wananchi huko Mjengoni wa upande wa pili; Hivi nao si waliapishwa kulinda ,kuitetea na kuihifadhi KATIBA?

Wao wenyewe kama sane creatures with sound mind wanajisikiaje kuwepo mahali ambapo hawana uhalali wa kisiasa wala kisheria -They lack both political and legal legitimacy? Jamii yetu inawezaje kufika mahali ambapo hakuna mwenye hofu na sheria kuu ya Nchi hasa Katiba ambayo ndio NGUZO KUU ya umoja, amani na ushirikanowa Taifa letu kuanzia 1977 hadi sasa?

Hapa ndio imenifanya kumtaka Pascal Mayala kuliuliza lile swali lake na this time liulizwe kule mjengoni kama walinzi Na 1 wa KATIBA Yetu. Msomi wa kale aitwaye Kalsen Hans alisema kuwa a grund norm is the supreme to other norms in the society; when any norm does not conform to ground norm , it becomes null and void hence losses its efficacy and validity wale wawakilishi 19 wasiokuwa na chama kama groundnorm inavyotaka, wanapochangia,kemea au kushauri, wanafanya hayo kwa MAMLAKA yapi wakati wameapa kulinda KATIBA?

"Afrer all, MPs/Judges can only protect democracy if the law itself is democratic to defenders of the Constitution"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…