Dotto C. Rangimoto
JF-Expert Member
- Nov 22, 2012
- 1,985
- 1,286
SEMA AAGE NYONGA, MBIO SIMKATAZE.
View attachment 213885
Mwana wa kuku ni yai, weye wasema na nani?
Hata hivyo natumai, mlengwa kuku nadhani,
Hivyo basi sishangai, kuku kutoka fichoni,
Sema aage nyonga, mbio usimkataze.
Kuku kanituma kwako, ajua ulalamavyo,
Hivyo katoa tamko, msikie asemavyo,
Hazitaki chokochoko, anaishi atakavyo,
Sema aage nyonga, mbio usimkataze.
Kuku asema na wewe, mwana hebu msikize,
Hivi aogope mwewe, wala nini watotoze,
Wallahi hana kiwewe, huyo mwewe achomoze,
Sema aage nyonga, mbio usimkataze.
Hana titi kifuani, kuku si pundamilia,
Hana mfuko kwapani, chakula kuchukulia,
Hivi kuku afanyeni, watoto kuhudumia,
Sema aage nyonga, mbio usimkataze.
Hivi kuku hana kucha? na midomo ya kuchonga?
Mwewe amtie kucha, mdomo waweza gonga,
Kuchakura sije kacha, asimugope kipanga,
Sema aage nyonga, mbio usimkataze.
Cha mja kina hila, Zephania unajua,
Mwalea mpate kula, lengo lenu alijua,
Bora timua jalala, jua bure inaua,
Sema aage nyonga, mbio usimkataze.
Si kama anakilanga, sema na zako fikira,
Hivi akiacha tanga, pamoja na kuchakura,
Miili itajichonga, huoni hino hasara?
Sema aage nyonga, mbio usimkataze.
Kila panapo riziki, hapakosi hekaheka,
Tena mikikimikiki, ya vulio kuchanika,
Siseme haambiliki, wajibu kuhangaika,
Sema aage nyonga, mbio usimkataze.
Asemayo ni nususi, kuku yuko na hoja,
Aweke rahani rasi, kutafuta kuna haja,
Baharini wasiwasi, vipi upende kangaja?
Sema aage nyonga, mbio usimkataze.
Njano5.
0784845394/0655395394
View attachment 213885
Mwana wa kuku ni yai, weye wasema na nani?
Hata hivyo natumai, mlengwa kuku nadhani,
Hivyo basi sishangai, kuku kutoka fichoni,
Sema aage nyonga, mbio usimkataze.
Kuku kanituma kwako, ajua ulalamavyo,
Hivyo katoa tamko, msikie asemavyo,
Hazitaki chokochoko, anaishi atakavyo,
Sema aage nyonga, mbio usimkataze.
Kuku asema na wewe, mwana hebu msikize,
Hivi aogope mwewe, wala nini watotoze,
Wallahi hana kiwewe, huyo mwewe achomoze,
Sema aage nyonga, mbio usimkataze.
Hana titi kifuani, kuku si pundamilia,
Hana mfuko kwapani, chakula kuchukulia,
Hivi kuku afanyeni, watoto kuhudumia,
Sema aage nyonga, mbio usimkataze.
Hivi kuku hana kucha? na midomo ya kuchonga?
Mwewe amtie kucha, mdomo waweza gonga,
Kuchakura sije kacha, asimugope kipanga,
Sema aage nyonga, mbio usimkataze.
Cha mja kina hila, Zephania unajua,
Mwalea mpate kula, lengo lenu alijua,
Bora timua jalala, jua bure inaua,
Sema aage nyonga, mbio usimkataze.
Si kama anakilanga, sema na zako fikira,
Hivi akiacha tanga, pamoja na kuchakura,
Miili itajichonga, huoni hino hasara?
Sema aage nyonga, mbio usimkataze.
Kila panapo riziki, hapakosi hekaheka,
Tena mikikimikiki, ya vulio kuchanika,
Siseme haambiliki, wajibu kuhangaika,
Sema aage nyonga, mbio usimkataze.
Asemayo ni nususi, kuku yuko na hoja,
Aweke rahani rasi, kutafuta kuna haja,
Baharini wasiwasi, vipi upende kangaja?
Sema aage nyonga, mbio usimkataze.
Njano5.
0784845394/0655395394