Sekta ya fedha/uchumi ni kimbilio la makanjanja!!

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
36,155
29,677
Hii najua itawatibua wengi lakini ukweli lazima usemwe.

Nchini mwetu hii sekta ya fedha au uchumi ni sekta iliyoonekana kuwa kimbilio la wasio na uwezo mkubwa kielimu kama inavyotokea sasa kwenye sekta ya elimu.

Sekta ya fedha ilichukua form four au form six failures ambao wengi walienda kujiendeleza IFM,CBE na IAA.

Nikijaribu kufanya sample ya waliokuwa watupu darasani wengi wao waliibukia kwenye uhasibu na ugavi...kama unabisha ulizia wale uliosoma nao na waliokuwa vilaza au wavivu au watoro watakwambia wako wapi kama sio TRA,TPA,BOT,NMB,ACB n.k.

Tumelazimisha na Tunaendelea kulazimishia wasio kuwa na uwezo kuingia kwenye fani zinazohitaji weledi na matokeo yake ni mkwamo tu....hata aje rais malaika bado kuna kazi ngumu sana ya kurekebisha sekta kama hii ya fedha....yaani kila ukisample utajikuta unapata garasa tu...!

Ni sekta hii hii ya fedha/uchumi inayoshuhudia watu wakijipatia mavyeti meengi mara sijui CPA mara NBAA n.k yaani in three or four years mtu ameshakuwa na vyeti vitano na zaidi wakati form four au form six alitoka kama kilaza!!

Leo nimeona nioongelee sekta hii ya uchumi na fedha kwanza kwani ni muhimu kwa maendeleo.

IT IS A BLUE MONDAY!!
 
Leo nakuunga mkono jingalao. Elimu ya bongo ni nzuri tu ila wabongo wengi sana wanasoma TU wapate vyeti na sio kuelimika. Badala wasome wapate vyeti na kuelimika.

Siyo tu sekta ya fedha na uchumi hata mawazir na hata wakubwa wa nchi Elimu zao hata kama ni kbwa lakini wamefikia huko kiujanja janja
 
Naona muendelezo wa wapinzani kutaka vilaza wabebwe
 
Hakika hiyo sector imebeba vilaza wengi sana,
Ndio mana tunashindwa kupiga hatua, kuna mapoyoyo mengi sana yamejificha huko,
Mtu tangu chini alikuwa ni mtu wa zero tu,unakuja kushangaa eti nae anafanya kazi kwenye sector kiungo muhimu kwenye nchi,
Na upuuzi wa kubebana nao unachangia sana hilo tatizo,
Na mbaya zaidi serikali ya CCM imelikalia kimya hilo tatizo
 
Hakika hiyo sector imebeba vilaza wengi sana,
Ndio mana tunashindwa kupiga hatua, kuna mapoyoyo mengi sana yamejificha huko,
Mtu tangu chini alikuwa ni mtu wa zero tu,unakuja kushangaa eti nae anafanya kazi kwenye sector kiungo muhimu kwenye nchi,
Na upuuzi wa kubebana nao unachangia sana hilo tatizo,
Na mbaya zaidi serikali ya CCM imelikalia kimya hilo tatizo
Upo sahihi kabisa...
 
Back
Top Bottom