Habari..
Ningependa kuwataarifu wazazi wenzangu kama mimi kuhusu tatizo kubwa linalowapata wazazi wa awamu ya kwanza(first timers) kuhusu swala la uzazi katika hatua yote ya kujifungua mpaka malezi.
Mwenza wangu alibarikiwa kupata ujauzito na tuliamua ni vyema kupata huduma nzuri kwaajili ya afya ya Mwanetu katika Hospitali ya Muhimbili (Clinic Private Sessions). Nikimaanisha tulienda kwa kulipia na sio huduma za bure.
Tulibarikiwa na Mwanetu Mwaka 2016 ila kwa bahati mbaya alizaliwa kwa Vacuum (Vacuum Extraction) ikisemekana mtoto alinyongwa na kitovu chake, hivyo ilisababisha mtoto kutokuzaliwa vizuri nikimaanisha kuchelewa kulia na kuvuta hewa, kunywa maji (Amniotic Fluid) hivyo aliwekewa kipumulio (Oxygen) kwa mda wa siku 11.
Hivi sasa mwanetu ana miezi 10 ila alishindwa kufanya matendo yale ambayo mtoto wa kawaida mwenye miezi hiyo mfano kukaa, kupiga makofi, n.k ikisemekana mtoto wetu alipata athari kwenye ubongo kwa kukosa hewa na pia matumizi ya Vacuum, ila tunamshkuru Mungu anaendelea vizuri ila bado tuliamua kutathmini zaidi juu ya hilo swala tangu tuivyogundua wenyewe kwamba angekua na matatizo hayo akiwa na miezi 7.
Huduma zinazotolewa na Hospitali zetu Hapa nchini zimeathiri Wazazi wengi mno na ushahidi ni utembelee Hospitali ya CCBRT Tanzania unagundua kua madaktari na manesi wanakua wazembe katika dakika za mwisho haswa mtoto akiwa anazaliwa na hata kabla nikimaanisha maandalizi ya Mama na Mtoto kabla hawajaingizwa Wodini.Hivyo hufanya Wazazi wengi kupitia mateso ya kupata watoto waliopooza au kutotengamaa viungo na vibaya zaidi vifo vya watoto wengi sana haswa kama wazazi hawana Uwezo wa kuwapeleka watoto wao wakapate huduma bora zaidi ili kurekebisha makosa yaliofanyika.
Hivyo Ningependa kutaarifu wazazi wengine wapya au walio na uzoefu kuwa na uangalizi na umakini wa huduma zitolewazo na Madaktari na Manesi wetu kwasababu wao ndo hubeba afya za watoto wetu katika swala la Kuzalisha na Matibabu.
Hivyo ukijua kua mtoto wako hakulia wakati alizaliwa au kuchelewa kulia tafadhali tafuta msaada wa Daktari mzuri mapema.
NB: Please ignore my Swahili but my Goal was to reach a multiutde of people to raise awareness. Thank you