hekimanyingi
JF-Expert Member
- Jul 12, 2013
- 679
- 573
Nasikitika kusema sekretarieti ya ajira imekuwa ni janga la wasaka ajira. Nilikuwa siamini nilipokuwa nikiambiwa na sasa nimekubali kuwa hawa jamaa ni genge tena genge la watu wanaofanya kazi kindugu, kwa rushwa na kwa kujuana. Watoto wa maskini wanapewa kazi za TGS D zile zenye mishahara mirefu wanapewa wanaowajuwa wao. Leo hii sishangai kuona watoto wa maskini wanapangiwa sitimbi yaani mbali na mjini wa vigogo wanawekwa pale magogoni. Yaani inasikitisha sana. Mliibia watu kazi za PPRA mmeiba kazi za AG na sasa juzi mmeiba kazi za GPSA na nyingine nyingi tu, najua keshokutwa mnapanga kugawana kazi za TANROADS Mungu atawalaani. Kama kweli nyie wema mngekuwa mnarudisha karatasi au kutoa nafasi ya mtu kukata rufaa kama msingeumbuka. Nashauri serikali iunde chombo cha kuwasimamia hawa jamaa au kama kipo ujue kimekufa. Pale Chuo cha uhasibu Arusha (IAA) waliita watu kwaajili ya usahili mwezi januari cha kushangaza walikuwa na vijana wao waliosoma pale tayari walikuwa intern na ndiyo waliwapa kazi na wengine watoto wa waalimu wa pale mpaka majina tunayo tukanyamaza sasa mnataka kufanya kama idara za serikali ni mali yenu. Hamna huruma na watoto wa maskini wanaotoka Bukoba, Ukerewe, Rorya, Musoma, Kigoma na Songea? wanaharibu hela mnakuja kuwaonea. Inaudhi sana.