Testar
JF-Expert Member
- May 30, 2015
- 7,613
- 12,892
Schadenfreude ni hali ya kuhisi furaha/starehe pindi mtu anapoona au kusikia watu wengine wanateseka au wamepatwa na tatizo.
Hili ni tatizo la kisaikolojia lenye kuashiria chuki miongoni mwa watu kwenye jamii.
Wapo wahanga wa Schadenfreude ambao wao hufurahi zaidi pindi mabaya yanapotokea kwa wengine kuliko wakati mema yanapotokea kwao wenyewe.
SABABU ZA KUWEPO KWA SCHADENFREUDE:
1.Wivu: Kuna watu hawapendi kabisa kuona mambo mema yakitokea kwa watu wengine.
Wahanga wa wivu huumia sana pindi watu wengine wanapofanikisha mambo mema.Kama jambo baya limempata mtu aliyeonewa wivu, basi wenye wivu watafanya sherehe.
2.Chuki: Kutokana na watu kuangukia kwenye makundi mbalimbali ya kijamii kama vile dini, kabila, ushabiki wa michezo, vyama vya siasa n.k. panakuwepo na hatari ya kutokea kwa uhasama baina ya hayo makundi.Uhasama ukiwepo miongoni mwa makundi ya kijamii, wahusika wataombeana mabaya na pindi yakitokea hufurahia sana kuona wenzao wakiteseka.
3.Mtu kujihisi dhaifu: Kuna baadhi ya watu kwenye jamii ambao bila sababu za msingi wao
hujiona na kujihisi kuwa ni wadhaifu.Watu wa namna hii huamini kwenye
jamii kuna watu wenye nguvu halafu na wao walio dhaifu.Kama jambo baya
litampata mtu aliyewekwa kwenye kundi la wenye nguvu, 'wadhaifu
watafurahi na kufanya sherehe.
4.Ushindani uchwara: Kuna watu ili wao wajione ni bora, lazima pawepo na watu walio dhaifu.
Chukulia mfano wa wanafunzi, kuna baadhi ya wanafunzi wanafurahi zaidi
pindi anapo ongoza darasani kwa kupata alama 30 kuliko pindi anapokuwa
wa tatu lakini akiwa na alama 80.
NAMNA YA KUEPUKANA NA SCHADENFREUDE
JIAMINI: Kuwa na imani pamoja na matumaini kuwa wewe ni mtu bora na muhimu kwenye jamii.Tambua kwamba hapahitajiki mtu dhaifu ili wewe uonekane bora bali wewe ni mtu muhimu kwa kuwa upo.
KUWA NA UPENDO: Namna ya kuwa na upendo ni rahisi sana.Kila unapokutana na mtu assume yule mtu ni wewe au ni yule ndugu yako unayempenda sana.Kwa kufanya hivyo, utamtendea mema yule mtu na kujikuta ukimpenda na mwisho wa siku utakuwa na marafiki wengi na wema.
JIWEKEE MALENGO: Ili kuepuka ligi zisizo na umuhimu, ni bora kuishi kwa malengo badala ya kuishi kwa mashindano. Unapoishi kwa malengo, mwisho wa siku furaha yako itatokana na sii kuanguka kwa wengine bali kwa kutimia kwa malengo yako.
''HE WHO EXPERIENCES THE UNIT OF LIFE SEES HIS OWN SELF IN ALL BEINGS AND ALL BEINGS IN HIS OWN SELF AND LOOKS ON EVERYTHING WITH AN IMPARTIAL EYE''