Sauti ya wengi, ni Sauti ya Mungu

Sauti ya wengi, ni Sauti ya Mungu

Mwanawakati

Member
Joined
Sep 6, 2014
Posts
10
Reaction score
12
Miezi kadhaa iliyo pita, kulikuwepo minong'ono na mijadala mingi mitaani na mitandaoni ilio kua ikikosoa/ ikishauri na kushinikiza nembo ya mwenge iliowekwa daraja la Tanzanite iondolewe na kuwekwe alama ya Dini la Tanzanite!.

Mheshimiwa Rais wetu, Mama Samia Suluhu Hassan alipozindua daraja hilo Machi 24 2022, kwa vile ni mnyenyekevu na msikivu, alipokua akihutubia aliagiza nembo hiyo ya Mwenge iondolewe na iwekwe nembo ya jiwe la Tanzanite!. Leo yapata miezi miwili na siku kadhaa agizo halijatekelezwa!.Tatizo ni bajeti? Hapana. Na Je, hamutii maagizo yake? Au mpaka mpatiwe hofu?

Mtakubaliana nami kua maoni ya Wananchi tulio wengi tunasema uwepo wa nembo hiyo hapo darajani haustahili. Ukweli ni kwamba, alama ya Mwenge ina Uwakilishi wa kutosha tayari kupitia alama nyingi mbalimbali. Mifano: Mwenge upo kwenye nembo ya Taifa( Bibi na Bwana), Upo kwenye nembo ya Jeshi la Ulinzi la Tanzania, Upo pia kwenye nembo ya Jeshi la Zima Moto na Jeshi la Magereza, Mwenge upo tena katika nembo ya Benki kuu... Tuna mbio za Mwenge, n.k Kwaivo itoshe kusema tunauthamini Mwenge na kuheshimu tunu zake.

Sambamba na hayo; Tanzanite ni Dini pekee linalopatikana Tanzania peke yake. Kwa maana hii, tunastahili kulinadi dini hili kisawasawa pia na kulipatia hadhi za kipekee kupitia Alama mbali mbali za utambulisho wa Taifa letu. Ni dhahiri imependeza kuona jengo la stesheni kuu ya treni ya kisasa limejengwa kwa umbo la Tanzanite!Hongera serikali yetu, na kwa kua daraja letu hilo sifa yake ni refu kuliko yote Afrika ya mashariki, hakika ni kivutio kingine cha taifa hili! Kwa mantiki hii ndugu Viongozi wetu, tunawaomba kwa mara nyingine wekeni nembo ya Tanzanite ili liongeze Mvuto na maana zaidi.

Wakuu, Mwisho nimalizie kwa kusema, utekelezaji wenu ndo utaamua daraja linaakisi 'Tanzanite Bridge ama Mwengenite Bridge'.

#Natanguliza shukurani
#Mwanawakati
#Mwananchi
IMG_20220604_052601.jpg
 
Back
Top Bottom