Sasa ni Muda muafaka kwa wale wanaonunuliwa kushughulikiwa na walipwachagua

Mahweso

JF-Expert Member
Jan 10, 2014
1,098
1,501
Kama biashara ni nzuri kwanini wasigawane wanachokipata na waliowachagua? Haiwezekani tupigane wote harafu anakula mmoja,

Kabla ya kuhama tunataka warudi kuitisha Mikutano na walipwachagua na kuwaeleza walichokiona ndani ya chama anachotaka kuhama, na anakoenda, kapata nini aseme ili tufaidike wote,

Ila hii ya kujiamulia tu utafikiri kajiweka mwenyewe pale haifai.

Tuamke wananchi Hawa tunao wachagua wamegundua siasa ni Biashara, mnawachagua wawapiganie kumbe wenzenu wanapambana na Hali zao.
 
Dawa yao kipindi cha uchaguzi ni kuacha kujiandikisha na kwenda kupiga kura watawale kifalume kama mfalume Mswati wa Swaziland
 
Wafanyakazi wa mabenki mtakuwemo humu. Hao wachumia tumbo waliokuwa Madiwani na Wabunge rushwa zao walizohongwa hawawezi kuziweka ndani ya magodoro ni lazima waziweke kwenye mabenki.

Tumieni umakini mkubwa kudukua accounts zao kama kuna deposits za hivi karibuni ambazo ni kubwa mziweke humu ili kuwaanika hawa matumbili hadharani.
 
Kwa kipindi kifupi Lipumba, Maliyamungu Bashite, Le mutuz na kikundi chao cha akina Jerry muro wamevuna mapesa mengi toka Hazina pesa za walipa kodi ambao wengi si wanachama wa CCM, pesa ya walipa kodi inayotumika kwa mambo ya hovyo hovyo kisa Maliyamungu Bashite na kikundi chake wapate cha juu 10% , pesa inayotumika kuwanunua Wapinzani na pesa inayotumika kurudia uchaguzi na pesa inayotumika kuwakomoa kuwadhalilisha kuwabambikia kesi kuwapiga Risasi ni pesa nyingi sana kuliko pesa ambazo zingeweza kutumika kupeleka maendeleo jimboni na wananchi wakapendezewa na kuichagua CCM kwa kura nyingi, Maendeleo yangetosha kuvuna kura pasipo kutumia mbinu za uchakachuaji, wizi wa kura na polisiccm, cha ajabu kwa sasa pesa za walipa kodi zinaibiwa na Maliyamungu Bashite na kikundi chake kwa kisingizio cha kuzitumia kudhoofisha upinzani, huo ni Ufisadi Hatari kupata kutokea Duniani, kuchukua pesa Hazina kienyeji na kuzitumia kwa mambo ya hovyo hovyo ni ufujaji wa pesa za Umma.
 
Wafanyakazi wa mabenki mtakuwemo humu. Hao wachumia tumbo waliokuwa Madiwani na Wabunge rushwa zao walizohongwa hawawezi kuziweka ndani ya magodoro ni lazima waziweke kwenye mabenki.

Tumieni umakini mkubwa kudukua accounts zao kama kuna deposits za hivi karibuni ambazo ni kubwa mziweke humu ili kuwaanika hawa matumbili hadharani.
hii mbinu ni nzuri kwa ajili ya kuwaumbua lakini Habari za uhakika ni kwamba wengi hulipwa Cash tena kwa Dola ili kuepuka mabulungutu makubwa, Pesa zote za kuwanunua Wapinzani inatolewa na Maliyamungu Bashite ambaye huenda kuichukua kule Hazina kwa Doto katibu mkuu, mtafute Le mutuz kaa nae Bar mnunulie Bia mpe na mchepuko akishalewa atakupa Siri zote jinsi wanavyofanya kuiba pesa za Umma kwa kisingizio cha kuzitumia kudhoofisha upinzani.
 
Dawa nikuwaadhibu kikamili wale wote wanaofanya uhuni wa kuhama vyama

Ikatokea ukatolewa mfano wa adhabu kali kwa hawa washenzi....hili jambo halitafanyika tena.

Inahitajika adhabu kali, kali kwelikweli ya kukomesha usaliti huu.

Watu walikesha

Walipigwa

Waliumizwa

Wafungwa

Hawakulala
Nknk

Halafu kilarahisi tu bila mantiki wa hoja maridhawa mtu anaropoka naachia ubunge!!!!

Kwani hapo ulijeweka mwenyewe?
 
Shukrani Mkuu kwa ufafanuzi kama pesa nyingi kiasi hicho wameamua kuiweka majumbani mwao basi hawa jamaa ni majuha sana. Yule katambi aliahidiwa 50 milioni Hawa wengine inaweza kuwa hata mara nne au zaidi. Kuweka pesa nyingi kiasi hicho nyumbani ni hatari sana.

hii mbinu ni nzuri kwa ajili ya kuwaumbua lakini Habari za uhakika ni kwamba wengi hulipwa Cash tena kwa Dola ili kuepuka mabulungutu makubwa, Pesa zote za kuwanunua Wapinzani inatolewa na Maliyamungu Bashite ambaye huenda kuichukua kule Hazina kwa Doto katibu mkuu, mtafute Le mutuz kaa nae Bar mnunulie Bia mpe na mchepuko akishalewa atakupa Siri zote jinsi wanavyofanya kuiba pesa za Umma kwa kisingizio cha kuzitumia kudhoofisha upinzani.
 
1. Nahisi wanalindwa na mhimili uliojichimbia zaidi. Wamepewa kinga ya kutoshughulikiwa.
2. Sitokanyaga wala kufuatilia mkutano wowote wa kampeni na siasa.
3. Wakati wa kampeni naangalia zangu BBC, Aljazeera, CNN, CGTN, NHK, .....
4. Nafikiria hata kugomea kupiga kura.
 
Hapana mkuu utakosea kwasababu

1. Kufanya siasa ni haki yetu ya msingi kikatiba

2. Kuhudhuria mikutano ya kisiasa ni haki yetu

3. Kupiga kura, kura halali ni haki yetu

4. Kuhakikisha haki inatendeka nihaki yetu

- Kuona aliyeshinda anapewa ushindi

-Anafanya aliyoyaahidi kikakamilifu

-Haondoki kwa sabababu zozote.... Maana hakujiweka pale. Tumehenyeka kumweka aaah

-Akiondoka nihaki yetu kumwadhibu kwa njia yoyote ili kuonesha hatukubali dharau zakijingajinga...zakipumbavu... Maana sisi tumetaabika wewe unafanya mzaha!!!!

Lazima tutoke na mikakati ya kutoa adhabu kwa kila upande

Akihama wa ccm, au akiachia ngazi....ccm wahakikishe wanamshughulikia huyo mpuuzi kwa nguvu zote....na wanatoa somo ili isijirudie

Akihama wa Chadema, Cuf, Nccr nknk au akiachia ngazi....wahakikishe wanamshughulikia huyo mpuuzi kwa nguvu zote....na wanatoa somo ili isijirudie.

Watanzania tumekuwa wanyonge sana katika kusimamia haki zetu za msingi kwa maslahi ya ustawi wa Tanzania yetu.

TUAMKE
 
Back
Top Bottom