Mbase1970
JF-Expert Member
- Jun 11, 2015
- 6,054
- 4,601
Siasa za Tanzania ni kama comedy maana hakuishi matukio kila kukicha. Mzee wetu mpendwa tuliyempatia jina la tingatinga alipoiona ikulu mahali ambapo hakuwahi kuota kama siku moja yeye na Mama Jesca wataingia hapo akaja na mikwara mingi sana. Wengine tulikua tunamtetea na sababu kubwa ya kumtetea ilikua ni CV yake ya miaka 20 ya uwaziri wake. Kumbe hatukujua lengo kubwa lilikua nini?
Likaja tatizo la majipu, kila mtu akawa mtetezi wake. wengine waligundua mapema hasa kwa usemi ule usemao mchicha hauwezi kuzaa mbuyu lakini wengi wetu tulihamahasika na kuona tumempata mkombozi. Majipu yalienda sambamba na ziara za kustukiza, maarufu ni ile ya Muhimbili. Wapiga chapuo tulimpigia chapuo kubwa kwasisi tulio nje ya nchi tulihakikisha kuwa tunawaonyesha waafrika wenzetu matukio yote ili waione Tanzania mpya. La hasha tuliingizwa mkenge.
Wakati mcheza zumari wa CCM akiendelea na gombe sugu lake huko kwa wenzao tuliowakataa wakawa wanakuja na ya kwao. UKUTA, KATA FUNUA, KUFUNGA MIDOMO, KUVAA NGUO ZA MSIBA ali mradi tu na wao waonekane wapo.
Tuliokua na imani naye tulianza kustuka pale tu ukurupukaji ulipoonza. Sijawahi kuona ama kusoma mahali popote pale ambapo kuna demokrasia ya kweli watu wanazuiliwa kufanya mikutano ya siasa. Nimeishi ughaibuni kwa zaidi ya miongo miwili lakini sijaona vijembe vya kijinga kama vya wanasiasa wetu wa Tanzania. Lakini uzuri moja wanabishana kwa Kiswahili hivyo siyo aibu kubwa sana maana hakuna anayewaelewa na wanaowaelewa nao ni kama sisi kwa maana ya Wakenya, Waganda, Warundi.
Mtukufu mkuu alipomaliza mafuta katika lori lake akalikabidhi kwa baadhi ya wasaidizi wake, lakini kijiti kilimfikia mtoto mpenzi. Kwanza akampandisha cheo, lakini inaonekana alipoanza jitihada za vyeti bandia akagundua kuwa na mteule wake mpendwa naye yumo. Ninachoweza kukisema ni kwamba ama mteule alimtonya mzee wake kuwa apunguze kasi ya vyeti bandia ama mtukufu aligundua mwenyewe. Baada ya kugundua inaonekana akampatia mbinu ya kuweka kitanzi tujifunge wenyewe.
KITANZI TUJIFUNGE WENYEWE:
Hapa ni njia moja weka vuguvugu litakaloungwa mkono halafu machafu yote yakija tutakuwa tumeshapata kisingizio. Vita ya madawa ya kulevya
Hainijii akilini rais wa nchi anasimama mbele ya wawakilishi wa dunia kutetea uhuni uliofanywa na mteule wake kwa kisingizio cha kuwa hakuna aliyemchukulia fomu. Kwani kuwa rais ni sawa na kuomba kazi kwa Dewji ama Bakhresa kwamba ukifaulu interview basi kazi umepata??? Kura je? ulipigiwa na watoto wako, baba yako na mama yako?
Ni lini hawa viongozi wetu watajua kuwa hizo kazi walizokuwa nazo waajili wao ni sisi wananchi???
Mwisho narudia nukuu ya Askofu mkuu wa jimbo la dar es salaam alilolitoa kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 1995. Alisema " CCM na viongozi wote mliopewa dhamana na watanzania, niwakumbushe kitu kimoja kuwa Hittler hakuipindua serikali ya Ujerumani bali alichaguliwa na wananchi wa Ujerumani kidemokrasia kwasababu walichoka na mambo yaliyokuwa yanaendelea kwa wakati huo. Sasa na ninyi msitufanye tuje tuchague kichaa aje kuwa Hitler wa pili."
NA MIMI NASEMA MAGUFULI WATANZANIA WALIKUPATIA HIYO NAFASI SABABU WALIKUAMINI LAKINI INAONEKANA UMEJISAHAU NA UNAONA ULITUMIA NGUVU ZAKO KUAJILIWA. JIULIZE WENZAKO KINA BLAISE COMPAORE, YAYA JAMMEH KILITOKEA NINI? JIFUNZE NA MATUKIO YALIYOTOKEA DUNIA NZIMA KUANZIA URUSI MWAKA 1917. Wananchi wanyonge maji yakifika shingoni ni vigumu sana kuwabadili. Siombei tufike huko.
Me say, Tujadili kwa manufaa ya taifa letu tukufu la Tanzania tusijiingize katika itikadi na tuache matusi maana hayatusaidii. Nipo huru kukosolewa kwa mada na siyo kwa matusi. Kwa hii mada unaruhusiwa kutaja majina lakini si vizuri kuwatukana watajwa.