Hili uliloongea halina ukweli wowote kwani wao walikuwa name haki ya kuandika katiba bila hata kuwashirikisha watangamyika kwakua haiwahusu ila wao wazanzibari wanahaki zote kushiriki mchakato wa katiba unao endelea sasa ili kutetea maslahi ya Zanzibar ndani muungano kwakua hii ni katiba ya JMT, subiri mkianza kutengeneza katiba ya Tanganyika uone kama watakuja kuwaingilia ndo uanze kusema hayo uliyosema hapo juu. Sisi watanganyika ndo watu wa ajabu kabisa maana tunajifunika koti la muungano huku tukidhani kuwa tunaonekana, muungano ni wa nchi mbili zenye historia tofauti, hivyo tunatakiwa kukubaliana ama tuzike nchi zetu na historia zake na tuwe na nchi moja yenye historia moja au tuendelee name historia zetu na nchi zetu huku tukiutambua muungano na sio kama tunavyodanganyana, nchi moja inatambulika kama nchi name nyingine eti haipo, huu ni utapeli was wazi kabisa ambao unafanywa na wanasiasa, mimi si shabiki wa chama chochote ila ukweli ndio huo. Usiwalaumu wazanzibar badala yake walaumu wabunge waliotupilia mbali rasimu iliyoletwa na timu ya wazalendo