Sanaa na maigizo ya CHADEMA

Sanaa na maigizo ya CHADEMA

ndatama

Member
Joined
Jul 18, 2015
Posts
10
Reaction score
4
Kuelekea Uchaguzi Mkuu, nahisi waigizaji wa filamu za kibongo itabidi wapumzike kwa muda ili tutazame hizi sinema za wanasiasa.

Maigizo ya CHADEMA yanaanza pale walipomuita Lowassa in mwizi, fisadi na ni furaha ya Mungu kumzomea.

Wakaja wakamuhusisha na ACT -Wazalendo, hii ikawa zaidi haswa hadi kumpa udhamini wa ACT -Wazalendo.

Wakaja na habari Zitto kamfuata Lowassa Dodoma kumshawishi ajiunge ACT -Wazalendo, kumbe ni Mbowe na ujumbe wake waliokua Dodoma na Lowassa.

Yapo mengi sana yanayofanywa kisinema na CHADEMA haswa wakati huu wa kuelekea Uchaguzi Mkuu.

Kikubwa Leo ni yule mdhamini mkuu wa ACT -Wazalendo, anayeonekana kuwaacha aliowapa pesa na kujiunga kwa wale waliokuwa wakimtusi. Mbowe, hebu funza vijana zako nidhamu na akiba ya maneno.

Leo wanamlilia Lowassa na wameanza kuutilia shaka uwezo was Slaa. Hawa CHADEMA hii sinema wanayocheza inaudhi; ni ya kinafiki, imejaa usaliti na uasi.

Ndatama Mafuru
 
Kwenye siasa hakuna adui kwa kudumu wala rafiki wa kudumu kinachotokea hapa ni kwamba Chadema wanataka kuing'oa CCM madarakani ndio maana wanamshawishi Lowasa ajiinge kwenye hicho chma ili waweze kuiondoa CCM mdarakani hapo hakuna usanii wala maigizo bali ni Siasa
 
We sema maigizo, wakati tunazichoma kadi za chama cha zamani LIVE bila chenga. Ngoja nikafungue office mapema sana niendelee na zoezi la kugawa kadi mpya kwa wanachama wapya.
 
ndatama

Uko sahihi kabisa. This is a universal phenomenon in politics! Maigizo ni kwa wote. Maisha bora `kwa kila mtanzania yako wapi? Maigizo tu! Inapokuja kutafuta madaraka, hata mama yako/baba ya msaka madaraka/mwanasiasa and anyone closely related to the politician can be sacrificed!
 
Wanasiasa wengi wakiwa kwenye majukwaa huwa wanaongea mambo mengi sana lakini wakitoka nje ya siasa ni marafiki wakubwa so wanasiasa huwezi kwaingilia mambo yao utakuja kuabika bure.
 
Kwenye siasa hakuna adui kwa kudumu wala rafiki wa kudumu kinachotokea hapa ni kwamba Chadema wanataka kuing'oa CCM madarakani ndio maana wanamshawishi Lowasa ajiinge kwenye hicho chma ili waweze kuiondoa CCM mdarakani hapo hakuna usanii wala maigizo bali ni Siasa

uku ni kufilisika kisera, haiwezekani mtetezi wa umma leo ashirikiane na mwizi wa mali za uma tena kwa kutumia mali zilezile alizouibia uma kujenga uhalali wa akuutumikia uma. Bila hata chembe hata moja ya shaka ni wazi kuwa hapa hakuna maslahi ya uma bali maslahi binafsi ili kujaza matumbo yao. Kwa mpango huu ccm bado itaendelea kuwa chama tawala kwa kipindi kirefu sana
 
Back
Top Bottom