Samsung Note9 upgrade

teac kapex

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2011
Posts
470
Reaction score
137
Wadau naomba kujua kama naweza kui update simu tajwa toka android os 9 to os 10, kama inawezekana nichukue hatua zipi kufanikisha zoezi zima.

Natanguliza shukrani.
 
Nikwamba hujui kabisa au njia inayojulikana imefail.

Kwani hata kuletewa notification ya update hujapewa?
 
Ki ukweli sijui ndio maana nikaja kuomba msaada huku, na sms ya ku update sijapata, msaada inahitajika namiss vitu vingi version 10
 
Ki ukweli sijui ndio maana nikaja kuomba msaada huku, na sms ya ku update sijapata, msaada inahitajika namiss vitu vingi version 10
Naamini Jf wataalamu wa kitu hii wapo naomba msaada wenu tafadhali
 
Hapo zamani nilikuwa nasikia kwamba hizi simu za samsung unaweza kui update version ya android hadi kufikia version mpya iliyopo kwa wakati huo lakini nimejaribu kusaka msaada humu hakuna aliyejitokeza kunisaidia, kama kuna mwenye anajua msaada unahitajiaka tafadhali
 
nenda setting kisha system update acha isearch halafu tuma hapa ujumbe inaokupa.
 
Naelewa shauku uliyonayo ya kupandisha toleo la software yako mkuu.

Sina hakika kama Samsung watapandisha Note 9 kwenda Android 10 ama 11. Nilisikia kuna tetesi hizo za kupandisha Note 9 na S9 kwenda matoleo mapya ya Android.

Ushauri. Jichange ununue kuanzia Note 10 ama S10 ambazo sasa hivi ziko kwenye 600k hadi 800k upate kitu roho yako inapenda ambazo zinaweza kwenda hadi Android 13.

Ama kama unaweza zaidi subiri Note 21 mwezi wa 8. Jichange zaidi uje uvute huo mzigo.
 
Mmmh hela yenyewe hii ya manati sitegemei mwaka gani nitanunua. Ok asante kwa ushauri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…