MBOKA NA NGAI
JF-Expert Member
- Jan 31, 2025
- 496
- 768
Katika hali isiyo ya kawaida,
kama Uongozi wa SADC ulivyokuwa umekubaliwa na nchi ya Rwanda, kuwarahisishia wanajeshi wa umoja huo, kuondoka mashariki mwa DRC, kupitia mipaka ya Rwanda, huku wakielekea Chato, Tanzania, jana wanajeshi hao ndipo walitakiwa waanze kuondoka.
Haikufahamika mara moja kwa nini, na hapo taarifa zikasema safari yao ingeanza leo. jambo ambalo pia halikuzaa matunda.
Baadhi ya taarifa za chini ya carpet, zinadai uzito wa mambo matatu, ambayo ni:
1. madini yaliyopo kwenye kambi za SAMIDRC, ambayo SADC ilitaka wanajeshi wake waondoke bila kupekuliwa na magari yao, jambo ambalo M23 ilishakataa; japo hata nchini Rwanda, hawawezi kuingia bila kupekuliwa.
2. Jambo la pili, ni idadi kubwa ya wanajeshi wa DRC, Wazalendo na FDLR, waliojificha kambini humo. M23, inatakiwa kuwatambua wote waliomo humo, wanajeshi wa SAMIDRC waondoke, wazalendo na FARDC itajua wapi pa kuwaweka, na FDLR ipelekwe inakotakiwa kwenda.
3. Jambo la tatu ni silaha zao, wanazotaka kuondoka nazo, huku Rwanda, ikisema zipite zilikopita wakati wa kupelekwa, kwamba hawana imani na matumizi yake njiani, na kusema wamekubali kuwapa njia watu si silaha. Mpaka sasa, wanajeshi wa SAMIDRC, wakiwa mateka wa M23, silaha na mali nyingine zote za kijeshi, si mali yao tena, bali ni mali ya M23.
Makubaliano ya awali ya kuondoka nazo, yaliitaka SADC kuondoa milipuko yote iliyowekwa uwanja wa ndege wa Goma na kuukarabati na ndo ungekutimika kuzipeleka, maana nyingine si za kuondoka kwa njia ya ardhini.
Hizi silaha, zimeiumiza kichwa serikali ya Afrika kusini kwa kiasi kikubwa.