siamini kama kweli Wapare ni waoga, ni kati ya wilaya zenye shule nyingi za awali na sekondari mara baada ya uhuru. Kilichowaponza ni uaminifu wao kwa wale waliowaamini.
Daniel Nzira Yona, Chediel Yohana Mgonja, mama Mziray, na sasa Anna Kilango Mallecela- wamewasaliti kwa kiwango kikubwa. Watu wa same walikuwa wakiamini kauli zao, waliwapenda wakijua ni watu wao wote wanajua shida za kwao na wana sababu za kizipigania. Bahati mbaya kila aliyepewa rungu kulinda boma alihama na rungu na kuacha wezi kuiba ng'ombe.
Walifikiri labda usomi na ujana unasaidia wakampa kijana wao David Mathayo akiwa msomi na kijana chini ya miaka 40, ikapiga tsunami ya mwisho.
Wabunge karibu wote waliotoka CCM wamekuwa kupe, wamenyonya damu zao zote wakashindwa hata kuwasaidia. Naama nakubali kwa macho ya CCM wapare ni wapuuzi, naam kwa macho ya CCM wapare ni wajinga, Naam kwa macho ya CCM wapare hawajijui. Hizi ndizo kauli ambazo unampomkirimu mtu akafanikiwa anazitoa. Ni kauli nzuri sana aliyekivulini kiztoa kwani hajui jua lina sogea.
Mwaka 2015 tutajua je kweli wapare wanajijua au la! Tutakwenda , tutawaamsha wote, tutawaelelimisha wote. Watajua kweli watasimama na kamwe hawatarudi nyuma.
CCM imetumia hali duni za maisha, ugumu wa jiografia na barabara mbovu kushinda, kuna vijiji havififkiki kirahisi sehemu za pare bila mvua ikinyesha unakata mawasiliano kabisa.
2015 ni mtu na mtu, tunajua tunasema sema tunamaanisha . Hatujawahi kuona uongozi tangia uhuru. Mwisho wa ulaghai umefika. Karibuni buku saba na lundo la kebehi.