Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,346
- 26,138
Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania Mbwana Samatta ameiongoza TP Mazembe kuishinda Maghreb Tetouan ya Morocco kwa mabao 5-0 jijini Lubumbashi,DRC na kutinga nusu fainali ya Klabu Bingwa Afrika.
Samatta alifunga mabao matatu na kuwazima kabisa Wamoroko hao waliokuwa wakilingana nao kwa alama kabla ya mchezo huo wa jana. Samatta alikuwa mwiba mchungu kwenye mchezo huo uliokuwa wa kasi na ufundi.
Sasa TP Mazembe itakutana na El Merreikh ya Sudan kwenye nusu fainali.