Samatta aanza kwa kucheza vizuri

Mkalibari

JF-Expert Member
Mar 20, 2012
659
396
Mbwana Samatta kwa sasa maisha yake ya
soka yamebadilika kwa kiasi kikubwa sana
ukilinganisha na alivyokuwa TP Mazembe pale
nchini Congo DR. Kwa sasa ameanza maisha
mapya nchini Ubeliji tangu aliposajiliwa na klabu
ya Genk.
Samatta ameeleza changamoto ambazo
amekuwa akikabiliana nazo tangu atue Genk,
jana alifanya mahojiano ya moja kwa moja
kupitia Sports Bar ya Clouds TV na kufunguka
mambo kibao ambayo kama mdau wa michezo
ni vyema ukapata kujua.

Sports Bar: Mechi ambayo ulicheza kwa mara
mara ya kwanza wakati timu yako inapata
ushindi wa goli 1-0 ugenini, ulitarajia kama
ungepangwa kwenye mechi hiyo?

Samatta: Sikujua ilikuwaje na kocha alifikiria
nini, kwasababu kabla ya hapo tulishaongea
kwamba hata nitumia kwenye mechi hiyo na
atanitumia kwenye mechi nyingine. Lakini siku
ya mwisho ambayo tulimaliza mazoezi (Ijumaa)
kabla ya mchezo wa Jumamosi aliniambia
ntakuchagua kesho twende pamoja katika hiyo
mechi.
Hauwezi kukataa kwasababu alikwambia
sitokuchagua na baadae amebadilisha, yeye
ndiyo mwalimu muhimu ni kwamba niko tayari
kwahiyo chochote kitakachotokea kwa muda
wowote nafikiri nitakuwa tayari.

Sports Bar: Kocha wako Peter Maes alikwambia
nini wakati unaingia kipindi cha pili dakika ya 73
kuchukua nafasi ya Nikolaos Karelis?

Samatta: Timu ilikuwa iko mbele kwa ushindi wa
goli 1-0 na alichoniambia ni kwamba tunahitaji
kulinda ushindi, chochote kitakachotokea
vyovyote itakavyokuwa lakini nihakikishe timu
inacheza pamoja ili tusipoteze ushindi.

Sports Bar: Baada ya mechi kumalizika ulipata
comments gani kutoka kwa mwalimu na hata
viongozi wa timu?

Samatta: Viongozi walinipa feedback ya mchezo
waliniambia nimecheza vizuri kwa muda mfupi
lakini nilionesha kwamba nilikuwa na nia ya
kujituma kwasababu muda mwingi nilikuwa
nakimbia najaribu kuisaidia timu pia rais wa timu
nilikutana naye na alinipongeza pia.

Sports Bar: Upo ugenini, ukitoka mazoezini huwa
unafanya kitu gani ambacho kinakufanya uwe
busy muda mwingi?

Samatta: Nikitoka mazoezini mara nyingi huwa
nikirudi nyumbani naabgalia TV, nacheza
PlayStation, nasikiliza music na vitu vingine vingi
ambavyo vinanifanya muda mwingi niwe busy.
Huku muda wa jua ni mchache saa 12:00 jua
linakuwa limeshazama na linachomoza kuanzia
saa 2:30 au saa 3:00 kwahiyo muda wa kulala
kwangu unakuwa ni mchache kwasababu nakua
nafanya vitu vingi.

Sports Bar: Kitu gani kwa sasa ambacho ni
changamoto kwako tangu umefika ubelgiji?

Samatta: Kwakweli kwasasa nafikiri ni ugeni,
ugeni ni changamoto kubwa kwasababu
mazingira mengi sijayazoea nahitaji kuzoea ili
vitu vingine viwe rahisi. Kingine ni hali ya hewa
kidogo bado inanipa shida lakini nikishazoea vitu
hivyo kila kitu kitakuwa sawa.

Sports Bar: Kwasasa unaishi wapi, kambini,
hotelini au umepangishiwa nyumba?

Samatta: Kwasasa mimi naishi kwenye
apartment ambayo hata sijui ni mtaa gani
kwasababu bado ni mgeni na niko pekeyangu.
Nipo hapa sijui ninaishi eneo gani. Kilasiku
wanakuja kunichukua hapa kunipeleka mazoezini
na kunirudisha.
 
Safi kijana wetu, hizo ni dalili kuwa umemkuna kocha wako, AFANYE KAZI KWA BIDII kwani bado ana safari kidogo, mwendo ni EPL. Itakuwa ni kitu cha kujivunia kwetu na hata yeye alisema angependa siku moja aende EPL kisha watanzania kila jmosi na jpili tunakuwa vibanda umiza kumuangalia akisukuma gozi kwenye kioo. Pia ningependa Samatta awe na account hapa JF tuwe tunabonga kwa kuchat nae kumpa kampani anapokuwa na muda.
 
Back
Top Bottom