Umesema hujawahi kuwa na mpenzi?
Halafu hebu jifunze kuukabili ulimwengu, acha kujiinamia ukutani. Wachumba watataka kukuona sura yako.
kila la kheri baba.
Kiukweli sijawahi kuwa katika r'ship, ila kuanzia sasa naona uzalendo unanishinda kwakweli. Kuhusu sura yangu nadhani muhusika ataiona tu pale tutakapo kutana at first time.
All the best. Ila ingekuwa vema uweke na salary range, yaani
Mshahara wangu. 700,000 - 2,000,000. N.k
Hapo pm zitakuwa mara dufu.
Hongera sana kwa kujitunza. Usijali, mahusiano hayana haraka. Kuwa muangalifu usibadili hayo masharti uliyoweka hapo manake hauwezi kumbadilisha mtu baada ya kuingia kwenye mahusiano.
By picha nilimaanisha avatar, weka iliyo more positive, na uso wenye furaha.
Kila la kheri Salim.
Mkuu kama nilivyosema hapo awali, kazi ninayofanya ni temporary bado sijapata ajira ya kudumu, na kiasi ninachopata kwa kweli hata kwa mahitaji yangu tu binafsi bado ni kidogo napia nadhani sio vema kila mtu afahamu kuwa napata kiasi gani, ila kutokana na umri nilionao sasa naona sina jinsi inabidi tu niwe na mchumba ambae Mungu akipenda tuwe kitu kimoja hapo baadae.
Hapo tu ndio umekosea sidhani kama watakuja tenaa,ushawapeperusha ndege.....
Kwa kweli hata mimi hii kazi bado sijaridhika nayo na bado nipo katika harakati za kutafuta ajira yenye maslahi ya kuridhisha kidogo. Na pia natambua, nikweli kwa wasichana wa kipindi hiki wakiona nilivyojieleza hapa ni ngumu sana kukubaliana na hii hali, lakini nimeona haina sababu ya kutokuwa mkweli katika maswala kama haya. Ni bora niseme hali halisi niliyonayo sasa ili hata atakae tokea kunipenda kwa dhati basi akubaliane na hali niliyonayo.