Salamu zangu za kufunga mwaka (2017) kwa ndugu Mwigulu Lameck Nchemba (MB)

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,242
34,903
SALAMU ZANGU ZA KUFUNGA MWAKA (2017) KWA NDUGU MWIGULU LAMECK NCHEMBA (MB), waziri wa mambo ya ndani ya nchi..,


..., nakumbuka wakati ule, Mwigulu Nchemba (akiwa waziri wa kilimo na chakula) anateuliwa kushika madaraka kama waziri wa mambo ya ndani ya nchi, na kuapishwa Juni 13, 2016, kuchukua nafasi ya Charles Kitwanga (ambaye uteuzi wake ulitenguliwa) waswahili wa sasa wanasema 'alitumbuliwa'.., Mwigulu alitoa ahadi kadhaa, naweza kuzikumbuka zote, nizikumbushe mbili tu;


(i) VITA DHIDI YA MADAWA YA KULEVYA; Mwigulu Nchemba katika mahojiano na waandishi wa habari, aliwataka wafanyabiashara haramu ya kuuza madawa ya kulevya kuacha mara moja biashara hiyo badala yake watafute shughuli halali za kujiingizia kipato., hii ni vita ambayo Mwigulu aliitangaza mwenyewe, lakini najaribu kuamini hapa kwamba, Mwigulu hii vita imemshinda kwa namna kubwa sana.., bado athari za dawa za kulevya zinaendelea kutafuna taifa kwa kasi, kundi la vijana likiwa kwenye angamizo kubwa., (labda kama kuna mengine nyuma ya pazia,) lakini katika uhalisia, bado hali ni mbaya sana!

(ii) KUKOMESHA UHALIFU DHIDI YA RAIA NA MALI ZAO; Mwigulu Nchemba pia alisema kuwa atahakikisha anasimamia Ulinzi na Usalama wa Raia na Mali zao kwa kuziba mianya inayohatarisha amani na utulivu katika nchi..., kwa kiasi kikubwa kwenye eneo hili amejitahidi.., ingawa bado uimara wa ulinzi na usalama wa raia na mali zao bado ni shida nyingine kubwa.., tumeshuhudia matukio makubwa sana ya uhalifu wa raia kuporwa, kujeruhiwa na hata kuuwawa, maeneo haswaa ya Dar es Salaam, Mwanza, Tanga, Arusha, Kagera, uhalifu wa mabenki umekithiri, uporaji wa magari umekithiri, matukio ya kutekwa kwa watu yamejitokeza, etc..,


Tuendelee.., mimi kama mtanzania, kuna masuala kadhaa ambayo nimeridhika nayo katika utumishi wako katika nafasi yako kama waziri wa mambo ya ndani, na pia kuna mambo ambayo yanapaswa kufanyiwa kazi mwaka 2017.., nitayataja;


(i) Jeshi la Polisi linahitaji kufumuliwa na kuwa chombo cha huduma kwa Raia na Mali zao yaani Police Service na siyo chombo cha kutumia nguvu dhidi ya raia yaani police force.

(ii) unapaswa sasa kusimama kuhakikisha unarejesha imani ya vyombo vilivyo chini ya Wizara yako (mambo ya ndani ya nchi) kama Polisi kurejesha uhusiano mzuri kati yao (polisi) na Raia.., uhusiano uliopo sasa siyo imara sana, umezorota!

(iii) unapaswa kujitofautisha na watangulizi wako kadhaa waliowahi kuhudumu katika wizara hiyo kama Omar Ramadhani Mapuri, Nahodha, John Nchimbi na Charles Kitwanga na wengine.., unapaswa kuwa na weledi usiopaswa kuwa na doa.. Unapaswa kuacha alama ya utumishi katika wizara hii, kuanzia 2017.,

(iv) kuna kesi kadhaa za watanzania ambazo zimekufa kifo cha MENDE, kuna zingine zimekosa nguvu kutokana na sababu kadhaa, tunaomba kwa uwezo na nafasi yako uzifufue na kuziweka kwenye mandhari nzuri.., mfano, kesi ya mauaji ya Alphonce Mawazo, kesi ya mauaji ya Daud Mwangosi (hii unaweza kufuata hatua zote katika taarifa ya tume ya Jaji Maneto)

(v) Rushwa, hili pia ni janga kubwa sana linaloendelea kulichafua jeshi letu la polisi.., kumekuwepo na tuhuma jadidi za askari wetu, hususani askari wa usalama barabarani, kupokea na kuomba rushwa kutokana na makosa kadhaa wa kadhaa, imefikia nyakati (hii tamathali inayoitwa pesa ya ku'brush viatu, iondoke kabisa katika macho yetu watanzania), ni kero na aibu kubwa..,

(vi) vituo vya polisi kusogea karibu na makazi ya raia, kazi na jukumu la kwanza la polisi ni kulinda na kuhakikisha raia na mali zao, wako katika usalama usiotiliwa shaka.., hivyo, Mwigulu kama waziri, nakuomba tena, hakikisha vijiji ambavyo vinastahili kupata vituo vya polisi, vinapata, hii itasaidia sana jamii hizo, kuna sehemu kata kina watu zaidi ya watu 25,000 na hakuna kituo cha polisi.., mfano kata ya Simbo, halmashauri ya Wilaya ya Kigoma.., sogeza huduma za polisi kwa raia..,

.., na mengine mengi kama kuboresha makazi ya askari wetu, kupandisha vyeo vya utumishi na madaraja na pia mabadiliko ya mishahara kwa askari, pia kuboresha Maslahi ya Askari Wetu wa kada zote, wapate fursa ya kwenda masomoni..,

Kwa kumalizia.., ukiwa wewe ni mmoja kati ya wale vijana zao la CCM ambao wanajipambanua kama ni Wazalendo na wenye weledi.., basi tunapenda kuona suala la ``LUGUMI" likipata kushikiwa bango.., wewe ukiongoza jahazi hilo.., maana hadi sasa limefunikwa kimyaaa, na hakuna ambaye anasema tena kuhusu sakata hilo.., naweza kuamini kwako, kwa sababu, uliweza kusimama kinyume na wenzako katika sakata la ESCROW, hivyo, simama kwenye hii 'chaos' ya LUGUMI..,

Yapo mengi.., niiishie hapo kwa leo.., nipate fursa ya kufikisha ujumbe wangu kwa kiongozi mwingine ambaye anastahili kukosolewa, kusifiwa na hata kupewa ushauri na mimi (Mwananchi wa kawaida)


MWISHO; Mwigulu, ulisema na wote tunaelewa kwamba Ben-Rabiu Wa Saanane ni rafiki yako.., tangu 18-11-2016, alitoweka katika mazingira yenye utata mwingi sana.., ni mwezi wa pili sasa unakwenda kukatika.., wewe kama waziri wa mambo ya ndani ya nchi, waziri kijana, naamini unaweza kusaidia kijana mwenzetu huyu akapatikana akiwa salama ili taifa liendelee kumtumia kwa namna chanya zaidi.., tunaendelea na kampeni yetu ya [HASHTAG]#BringBackOurBen[/HASHTAG] pia [HASHTAG]#BringBackBenAlive[/HASHTAG] itakoma pale tutakapoona haipaswi kuendelea nayo!



Mwananchi wa kawaida,
Martin Maranja Masese (MMM)
 
Mkuu pole sana bado unamtegemea Mwigulu?

Toka yeye na JPM wakae kimia issue ya Lugumu.

LUGUMI alifunga vifaa vya utambuzi kwenye vitu vya Polisi 14 tu, kwa Gharama ya zaidi ya Tzs Bilioni 200.

Mwigulu kimia na Awamu ya Tano Kimiaa. Busness as usual

[HASHTAG]#BringBackBenAlive[/HASHTAG]
 
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ni nzito sana.Mwigulu nae ni miongoni mwa watu muhimu wanaohitaji kuombewa.
 
Back
Top Bottom