MpangoA
JF-Expert Member
- Jul 27, 2012
- 360
- 233
Wakuu wanajamvi, Salaam
Nimetafakari sana kazi za wanasiasa hasa wa vyama vya upinzani nikaona ni jinsi gani wanavyojitoa mhanga kutetea maslahi ya wananchi. Moja ya sala yangu ni kwa hawa wanasiasa kwa majitoleo yao. Kiimani, naomba Mungu aniwezeshe japo kwa mali kuchangia jitihada hizi bila kujali itikadi kwani kazi yao ni ngumu na kubwa.
Katika mjadala huu, nawaongelea wanasiasa safi si wale wanaoingia kwa uroho, wakihama huku na huko wakihaha. Nawazungumzia wanasiasa wa kweli wanaojitoa kwa mstakabari wa wananchi na taifa kwa ujumla.
Lengo si kubeza juhudi za wanasiasa wa chama tawala, hapana, hilo tunaweza kulijadili kwenye mada nyingine, ila ni kuonyesha thamani ya siasa za upinzani katika mstakabari wa maendeleo. Na ndio maana, nchi zilizoendelea hili walishaliona zamani. Mwanasiasa mpinzani sio adui, ni mwananchi kama mwingine, kama anamalengo mazuri kwa nchi ni vizuri mchango wake ukatumika kuendesha nchi pia.
Niweke wazi kwamba mimi ni mpenzi wa siasa kwani siasa ndio maisha, lakini si mwanachama wa chama chochote. Katika sanduku la kura ninampa kila mtu kwa haki yake..Rais, Ubunge, Udiwani. Nawapenda wanasiasa wote, chama tawala na upinzani. Vigezo vyangu ni utumishi na dhamira ya kutumikia kuliko itikadi.
Katika mada hii nitatumia neno CHAMA TAWALA kumaanisha CCM kwa sasa na UPINZANI kumaanisha vyama vya upinzani. Sasa ebu tuangalie upinzani:
1.Wapinzani wamejitoa mhanga kututetea
Hii ndio sababu kuu iliyonituma kuandika mada hii. Nitawataja wanasiasa wa upinzani wachache kwa ajili ya kuelezea ninacho maanisha. Ebu tutazame wasifu wa baadhi ya viongozi ambao wana maisha mazuri kulinganisha na watanzania walio wengi. Jambo ka kusikitisha, wengi wetu tunawakebehi kwamba wamepoteza kujihusisha na siasa na hili ndilo linaloturudisha nyuma watanzania. Tunadhani kuingia kwenye siasa ni kupoteza, watu wenye nafasi zao hawataki kutumikia na wakiamua kutumikia wanaenda kwenye mteremko, CHAMA TAWALA kusikokuwa na changamoto kwao ambapo maslahi yao hayataguswa.
2.Wapinzani wameleta suruhisho mbadala na chama tawala huiga
Kila mwaka tunaona hoja za kambi ya UPINZANI, bajeti mbadala na baadhi ya mambo mazuri serikali inayachukua.
3.Upinzani umetufungua macho
Ufisadi, ubadhilifu, rushwa na kila uozo uliowahi kutokea katika nchi hii umeibuliwa na UPINZANI. Ni imani yangu wafuasi wa CHAMA TAWALA wenye mapenzi mema hutoa hata baadhi ya nyaraka za siri kwa UPINZANI ili kutuhabarisha wananchi. Ni wakati sasa hata CHAMA TAWALA kuwa na watu safi, wasio ogopa kusema ukweli. Nchi hii ni yetu sote na jukumu la kila mmoja wetu na kukemea maovu ili kufaidi tunu za nchi hii. Sio jukumu la UPINZANI tu!
4.Upinzani kimbilio la wanyonge
Moja ya kitu ambacho kinanisikitisha sana ni fikra zetu watanzania. Shukrani kwa UPINZANI imekuwa ni wakati wa shida, wakati wa raha (mavuno) hapana. Nadhani hili ni kosa kubwa sana na ndio maana hatuendelei. Kila mtu tumpe haki yake anayostahili. Mifano iko mingi ambapo tumewakumbuka upinzani kwenye shida. Si jambo la kushangaza kusikia watu wakiuliza UPINZANI ulikuwa wapi jambo lisilopendeza linapo pitishwa bila kujiuliza UPINZANI ni wangapi katika sehemu za maamuzi. Wengi wamediriki hata kutoa vitisho, 'fulani asipotatua hili ubunge awamu ijayo asahau', bila kutafakari kwamba akifanya vinginevyo kura yake atampa kinara aliyepitisha jambo hilo! Sasa hii ni akili gani? Tumeshuhudia thamani ya UPINZANI ikipanda kwa kasi ya juu kwenye masuala yanayoleta uzuni kwa wananchi na thamani hiyo ikigalagazwa pindi rupia ikipitishwa!
5.Tujifunze mazuri kutoka siasa za upinzani za nchi zilizoendelea
Hili litatufikisha mbali, UPINZANI sio uadui, sote ni wamoja na taifa moja. La muhimu ni kuangalia maslahi ya nchi zaidi. Kwa kufanya hivi, upinzani utapata wanachama bora zaidi, wenye kuleta michango na changamoto bora zaidi na nchi itaendelea.
Nawaalika tuwaombee UPINZANI wanaofanya kazi nzuri na tusiwakwamishe katika hili kwani ni kwa faida ya taifa.
Mungu atubariki sote, karibuni kwa mjadala

- Prof. I. Lipumba (CUF) – Huyu ni mmoja miongoni mwa wasomi wachumi wazuri Tanzania na kimataifa. Amejishusha na kuingia kwenye siasa kuwatumikia wananchi. Kwa siasa zetu chafu, amedhalilishwa mara kadhaa na vyombo vya usalama. Kwa mtu wa kawaida, ingekuwa rahisi sana kusema, 'kwani shida ni nini, mimi ninaelimu yangu nzuri ngoja naachana na hizi siasa nafanya shughuli zangu'. Bado tunaona anaendelea kuwatetea wananchi. Najua anajua fika chama chake hakiwezi kumuingiza ikulu, lakini uwepo wake katika UPINZANI ni wa muhimu sana kwani amechangia uboreshaji wa mambo mengi kupitia siasa zake. Nitoe mfano kwamba, ni chama chake kilikuja na elimu bure, ufutaji wa kodi za kichwa ambapo CHAMA TAWALA kilibeza kwamba nchi utaendeshaje bila kodi lakini leo hii tunaona kodi ya kichwa imefutwa na elimu ya msingi sasa ni bure.
- Dr. W. Slaa (CHADEMA) –Msomi mzuri mwenye udaktari wa falsafa. Ni mtumishi ambaye amekuwa kiongozi wa miradi mbalimbali ya kijamii. Mfano uliowazi ni uanzishaji wa hosptali ya CCBRT ambayo watanzania wengi wa jamii zote wanafurahia huduma hii. Leo hii CCBRT kwa utendaji wake mzuri na kuwa msaada kwa wanyonge hasa kina mama na watoto, imeweza kuwavutia wafadhili wengi. Kwa kupitia CCBRT tu, Dr. Slaa angeweza kuishi maisha mazuri kuliko matukano, purukushani, na adha mbalimbali anazozipata. Lakini watanzania tunahitaji siasa zake japo hajawa Rais. Sote tu mashaida uimara wake bungeni, hoja za rushwa na ufisadi alizozisimamia kidete zimetuonyesha uozo wa viongozi wetu. Japo serikali haijatimiza wajibu wake hivyo hakuna mafanikio tuliyotarajia, lakini ni mwanzo mzuri na mapambano yanaendelea. Mwizi aliyekuwa anaiba akizani hatajulikana sasa inabidi atumie mbinu za ziada kuiba. Tunaomba walioko madarakani wawajibike na kuacha sheria kuchukua mkondo wake dhidi ya mafisadi na wala rushwa hawa.
- Mhe. F. Mbowe (CHADEMA) – Huyu ni mfanya biashara maarufu. Mali zake na biashara zake ziko wazi na hakuna kifisho. Mbali na hali nzuri aliyonayo, bado amejitoa kuwatetea wananchi. Kwa umaskini wa UPINZANI na kukosa msaada stahiki kutoka serikalini naamini anatumia hata rasilimali zake kukisaidia chama panapotokea mapungufu ya kifedha. Sioni faida ya wazi anayoipata kwenye siasa, kutoa muda wake kwenye siasa badala ya biashara zake. Lakini watanzania tunamuhitaji kwa faida yetu. Amesimamia vyema chama, ameleta dira yenye matumaini kwa wananchi. CHAMA TAWALA kimeiga mengi kutoka chama anachokisimamia!
- Dr. S. Mvungi (TLP) na Prof. M. Baregu. Hawa nawaweka pamoja kwa sababu ni wanataaluma. Dr. Mvungi ni msomi aliyebobea kwenye masuala ya sheria hasa Katiba, na Prof. Baregu ni msomi gwiji la elimu ya siasa. Hawa wamejitoa mhanga kutumia taaluma zao kukosoa maovu na mambo yasiyoenda sawa. Moja ya deni kubwa tulilonalo wasomi wa nchi hii, bila kujali itikadi zetu ni mchango wetu katika maendeleo ya nchi. Ni jinsi gani tunatumia elimu yetu kuwafumbua macho wasio na upeo. Kwa siasa za UDSM hawa wameonekana kuchanganya siasa na taaluma hivyo wameonekana ‘hawafai'. Mvungi sasa ni mhadhiri chuo kipya, University of Bagamoyo na Baregu yuko SAUT. Kwa wasomi wenzao ambao wao wanajiona wameukata, maisha yao mazuri, pesa ya utafiti inatiririka, wameamua kunyamaza hata pale akili zao za usomi zinapowafunulia kuwa mambo si sawa. Wengi wamebaki kukumbatia CHAMA TAWALA na kuendelea kutumika kuwalaghai wananchi kwa upeo wao uchwara na tafsiri uchwara za tafiti zao. Sisemi wasomi wote waende UPINZANI, la hasha!, ila waseme ukweli pale penye ukweli na watoe tafsiri sahihi za tafiti zao. Mmoja wa wasomi muumini wa CHAMA TAWALA lakini mwenye fikra za kujenga ni Dr. A. Rwaitama. Yeye anakili ni CHAMA TAWALA lakini inapofika kusema ukweli na kukosoa hasiti kufanya hivyo. Tunahitaji wasomi wa namna hii na si kuogopa kukosa fedha za utafiti endapo utasema jambo lisilopendeza machoni mwa serikali, mfano Dr. B.Banna!
- Wanasiasa wenye uhakika na maisha yao wako wengi na wengi tunawafahamu. Hawa wamenikonga zaidi na nimeweka kwa ajili ya mjadala.