VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,136
- 17,871
Nimefuatilia kwa kina sakata la kusimamishwa kwa Wabunge wa Upinzani kuhudhuria vikao vya Bunge huko Dodoma. Hiyo imefuatia uchunguzi juu ya vurugu zilizotokea Bungeni mnamo tarehe 27 Januari mwaka huu. Uchunguzi ulifanywa na Kamati ya Maadili ya Bunge chini ya Mbunge George Mkuchika,Kapteni Mstaafu.
Wabunge Tundu Lissu,Zitto Kabwe,John Heche,Halima Mdee na Ester Bulaya wanahusika na sakata hilo. Nilipopitia Taarifa ya kina ya Kamati ya Maadili,maazimio na taarifa ya Bunge nimeona mapungufu/makandokando haya:
Kwanza,adhabu iliyotolewa kwa Wabunge hao imezidi kiwango cha kisheria. Kwa mujibu wa Kanuni ya 74 ya Kanuni za Bunge,adhabu kubwa kabisa ni kusimamishwa kwa vikao ishirini.
Pili,Kamati ya Maadili,badala ya kushauri kama inavyopaswa na Kanuni za Bunge,ikatoa adhabu ya onyo kwa Wabunge wote wa upinzani. Kamati hii haina mamlaka ya kutoa adhabu kama onyo na kadhalika.
Tatu,kosa walilotenda Wabunge hao halikeri kiasi cha kuwapa adhabu kali hivyo. Kuoneshwa Bunge live ni kilio cha kitaifa.
Nne,Wabunge wote walioadhibiwa ni wa upinzani. Sintofahamu ya Januari 27 ilijumuisha Wabunge wa CCM. Kuwaadhibu wapinzani tu ni kuchora picha mbaya kibunge na kidemokrasia.
Tano,Kamati ya Maadili,kwenye Taarifa yake ililenga na hakika iliadhibu badala ya kulishauri Bunge. Kamati ilipoka mamlaka ya Bunge kuadhibu.
Kwa hali ilivyo,mbele ni giza!
Mzee Tupatupa wa 'Ulevini' Lumumba,Dar es Salaam