MANKA MUSA
JF-Expert Member
- Jul 9, 2014
- 922
- 1,094
''kama mradi wa UDA ni mradi halali, sasa ilikuwaje wabunge na madiwani wahongwe pesa ili kuuhalalisha(kukubali matumizi ya billion 5.8), unawezaje kuhonga ili upokelewe fedha zako ulizonunulia kitu halali mpaka vyombo vya habari vinaandika?''.........
· Amshangaa kupinga Rushwa lakini anabariki UFISADI UDA
· Asisitiza Rais Kapotoshwa Makusudi
· Amtaka Kujitafakari
Wakati kukiwa na taarifa kadha wa kadha mkanganyiko juu ya hatma ya Sakata la UDA kuelekea kutekelezwa kwa agizo la Rais Dkt John Pombe Magufuli la kulitaka Jiji la Dar es salaam Kukutana haraka na kupanga matumizi ya mgao wao wa shilingi bilioni 5.8 kama malipo ya mauzo ya Hisa zao asilimia 51 ambazo jiji lilikuwa linazimiliki.
Kumekuwepo na taarifa za uhakika zinazosema kwamba mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA mheshimiwa Freeman Mbowe kuunda kamati maalum ya wataalam wa chama hicho kupitia na kuhakiki mchakato mzima wa uuzwaji wa hisa hizo na ushiriki wa madiwani na wabunge wake katika kile kinachoitwa kupokea rushwa ya kati ya shilingi milioni moja mpaka tano ili kubariki uuzwaji huo.
Mmoja wa wajumbe wa baraza hilo la jiji ambaye pia ni mstahiki meya wa manispaa ya Ubungo Boniface Jacob ameonyesha masikitiko yake namna Rais Magufuli alivyopotoshwa juu ya jambo hilo na kwamba namna alivyohutubia siku ya uzinduzi wa mradi ule hakika Rais ametumika kuhalalisha moja kati ya UFISADI mkubwa kuwahi kutokea katika historia ya taifa letu.
Akizungumza na JAMVI LA HABARI mstahiki Boniface Jacob amesema kuwa haelewi na kwanini Rais Magufuli ameamua kupingana na msimamo, tabia na utambulisho wake mbele ya jamii wa kuwa mpinga Ubadhilifu na mkataa rushwa huku akitajitanabaisha kama mtetezi wa rasilimali wa Taifa.
‘’ukimsikiliza Rais Magufuli utaona namna gani ambavyo anatamani kuwa katika jumuiya ambayo haina ujanja ujanja, Rushwa , Ubadhilifu na Ufisadi wa aina yoyote, na ndio maana hakuna anayepingana naye kwenye hilo, lakini ukiangalia namna alivyo li-adress suala la UDA unaweza ukajiuliza mara mbilimbili ni Magufuli huyu huyu au mwengine’’. Alisema Mstahiki Boniface
‘’Watanzania wanaomuamini Rais Magufuli sidhani kama wanafahamu Rais wao ametumika Kubariki mradi wa Kifisadi namna hii, Rais amezungukwa na wajanja wachache waliogawana mali za masikini wa Tanzania waishio DSM, (Shirika la UDA), na sasa wanafaidi mali hizo huku waliotoka jasho kuzitafuta wakiendelea kubaki masikini’’. Aliongeza Meya Jacob
Kadharika Meya Jacob alisema kuwa haingii akilini kuwepo kwa taarifa za rushwa na kuhongwa kwa wabunge na madiwani wa vyama vyote vinavyoongoza jiji hilo ili kupitisha mradi huo na wao chadema kuchukua hatua huku chama kinachoongozwa naye Rais kikiendelea kuvuta miguu.
‘’sisi tulipozipata taarifa za kutolewa Rushwa kwa wajumbe wetu, mara moja chama kimeanzisha uchunguzi wa ndani na kamati ya wataalam imeundwa na mwenyekiti wa chama, sasa tunashindwa kuelewa mpaka sasa Rais na mwenyekiti wa CCM amechukua hatua gani’’. Aliongeza
‘’hivi nikuulize swali, kama mradi wa UDA ni mradi halali, sasa ilikuwaje wabunge na madiwani wahongwe pesa ili kuuhalalisha(kukubali matumizi ya billion 5.8), unawezaje kuhonga ili upokelewe fedha zako ulizonunulia kitu halali mpaka vyombo vya habari vinaandika?, maana yake hapo kuna walakini na siamini kama Magufuli aliyejipambanua mpiga madili dili hili halioni’’. Alisema Diwani huyo machachari wa kata ya Ubungo
Alipoulizwa juu ya thamani halisi ya shirika hilo la UDA alisema kuwa anaendelea kujumlisha mali halisi za shirika hilo na kuzitathmini na kesho atatoa taarifa kwa umma inayoonyesha mali halali za shirika hilo na thamani yake ambapo kwa kifupi anasema mali hizo ni zaidi ya mara hamsini mbele ya fedha ambazo Simon Group wamenunulia shirika hilo.