Wasomi mbalimbali wamesema sakata la mgogoro wa Madaktari na serikali linachochewa wanasiasa kutokana na misimamo ya wanasiasa hao walioitoa kwa nyakati tofauti huku wasomi hao wakinena kama ifuatavyo:
1. Uhai haupimwi na kitu chochote, Utaratibu wa Madaktari kugoma umepigwa marufuku katika nchi nyingi duniani-Dk.BENSON BANA
2. Ni tabia mbaya kuona kada moja inajiona ni bora kuliko nyingine-Dk. Bana
3. ANANILEA NKYA kusema kitendo cha Mawaziri wa Afya kushindwa kujiuzulu ni maajabu ni dhahiri suala hili limejaa siasa-SALIM SAID
4. Haki bila nidhamu, wajibu ni sawa na wazimu-Salim Said
5. Kuna njama za kuidhoofisha Serikali kupitia taaluma ya Udaktari-JOSEPH LUGHA
6. Kumpa Rais siku kwa ajili ya kutaka kufanikisha mambo yao ni kinyume na utamaduni wa Watanzania-BANA
Tutafakari
Hivi huyu anaejiita dr Bana ni kweli anaelimu ya kuweza kuitwa dr au ni mwanasiasa, kwani mie simwelewi. Kama serikali aithamini kada ya udaktari kwa vile viongozi wanatibiwa nje. Na kudharau huduma za hospitali zetu kwanini madaktari wasigome kwa maslai ya wananchi. Ukiangalia wanasababu za msingi ni kweli hospitali zetu ni duni na hazina vifaa,ukilinganisha na maofisi za kuanzia kwa wakuu wa wilaya mpaka mawaziri na rais mwenyewe. Hebu tizama fenicha zilizopo katika hizo ofisi na utizame bechi tu za kukalia wagonjwa wanaosubiri huduma au utizame ofisi ya daktari utashangaa. Huyu anayejiita dr Bana angalie picha zilizopigwa katika hospitali inayoitwa ya taifa tanzania(Muhimbili) wakati wa mgomo wa kwanza, vifaa vilivyoko vilivyochaa. Bana achane na siasa za mwaka 47 kuwa rais asiulizwe kitu au kumwambia eti sio utamaduni wa mtanzania. Kwasasa ni wakati wa vitendo rais akikosea anawajibishwa sio wakati wa rais kuwa ikulu kustarehe. Sasa huyu Bana anasema madaktari wanadai madai yao, ukifuatilia madai ya madaktari yanahusu watanzania wote wala sio kwa ajili yao tu. Madaktari wametoa madai yao tangu mwezi uliopita na wakakubaliana serikali haijatekeleza halafu leo hii Bana anatamka maneno ambayo hata mwanafunzi wa darasa la saba hawezi sema. Kwanza vifo vilivyotokea wakati wa mgomo wa kwanza ni tosha kwa waziri wa afya kujiuzulu. Lakini mpaka sasa hajajiuzulu na rais nae wala hajamwajibisha sasa hapa Bana anawalaumu madaktari kwa lipi kama sio huyo rafiki yake rais anaemtetea kashindwa kazi. Kwanza nawashangaa sana wandishi wanaomfuata huyu Bana ili kupata mawazo yake. Hafai hana mawazo ya kuendeleza nchi yeye anamawazo ya kuonewa huruma ili apewe cheo. Kwa upande wangu niko nanyi madaktari endeleeni kudai haki zenu na haki kwa watanzania. Waziri mkuu anasema kuwa waziri wa afya ni mgeni katika wizara na ameyakuta matatizo, huyu waziri kakaa mwaka mzima ameshindwa kuyatatua matatizo aliyoyakuta inamaana uwezo wake ni mdogo. Hivyo waziri mkuu anataka kutuaminisha kuwa tumwachie huyu waziri akae kwa miaka mitano ndio atatatua matatizo ya wizara ya afya. Waziri mkuu nae uwezo wake mdogo ukiangalia kwa makini ni yaleyale ya kulindana sio kufanya kazi. Tizama kwa wenzetu unaweza kuchaguliwa leo kuwa waziri baada ya mwezi moja inatokea matatizo katika wizara yako wa kwanza kuwajibika ni wewe wala haijalishi umekaa muda gani. Inachotakiwa ni utendaji wako wa kazi kuwa kiongozi sio starehe. Bana achana na mawazo ya enzi hizo za mwaka 47 tuko 2012Wasomi mbalimbali wamesema sakata la mgogoro wa Madaktari na serikali linachochewa wanasiasa kutokana na misimamo ya wanasiasa hao walioitoa kwa nyakati tofauti huku wasomi hao wakinena kama ifuatavyo:
1. Uhai haupimwi na kitu chochote, Utaratibu wa Madaktari kugoma umepigwa marufuku katika nchi nyingi duniani-
Dk.BENSON BANA
2. Ni tabia mbaya kuona kada moja inajiona ni bora kuliko nyingine-Dk. Bana
3. ANANILEA NKYA kusema kitendo cha Mawaziri wa Afya kushindwa kujiuzulu ni maajabu ni dhahiri suala hili limejaa siasa-SALIM SAID
4. Haki bila nidhamu, wajibu ni sawa na wazimu-Salim Said
5. Kuna njama za kuidhoofisha Serikali kupitia taaluma ya Udaktari-JOSEPH LUGHA
6. Kumpa Rais siku kwa ajili ya kutaka kufanikisha mambo yao ni kinyume na utamaduni wa Watanzania-BANA
Tutafakari