Sakata la mgomo wa madaktari kuna shinikizo la kisiasa-wasomi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sakata la mgomo wa madaktari kuna shinikizo la kisiasa-wasomi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwanajamii, Mar 6, 2012.

 1. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #1
  Mar 6, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Wasomi mbalimbali wamesema sakata la mgogoro wa Madaktari na serikali linachochewa wanasiasa kutokana na misimamo ya wanasiasa hao walioitoa kwa nyakati tofauti huku wasomi hao wakinena kama ifuatavyo:

  1. Uhai haupimwi na kitu chochote, Utaratibu wa Madaktari kugoma umepigwa marufuku katika nchi nyingi duniani-Dk.BENSON BANA
  2. Ni tabia mbaya kuona kada moja inajiona ni bora kuliko nyingine-Dk. Bana
  3. ANANILEA NKYA kusema kitendo cha Mawaziri wa Afya kushindwa kujiuzulu ni maajabu ni dhahiri suala hili limejaa siasa-SALIM SAID
  4. Haki bila nidhamu, wajibu ni sawa na wazimu-Salim Said
  5. Kuna njama za kuidhoofisha Serikali kupitia taaluma ya Udaktari-JOSEPH LUGHA
  6. Kumpa Rais siku kwa ajili ya kutaka kufanikisha mambo yao ni kinyume na utamaduni wa Watanzania-BANA

  Tutafakari
   
 2. R

  RMA JF-Expert Member

  #2
  Mar 6, 2012
  Joined: Oct 10, 2010
  Messages: 409
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapa huna hoja yoyote ya maana! Hizi ni propaganda tu za utawala feki wa ccm kutaka kuwahadaa wananchi kwamba chama fulani cha upinzani ndicho chanzo cha mgomo wa madaktari. Kumbuka madaktari wanagoma kwa sababu tu ya kudai maslahi yao. Sasa hii chuki unayotaka kuipandikiza hapa umeitoa wapi?

   
 3. Emmani

  Emmani JF-Expert Member

  #3
  Mar 6, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 525
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Bana tulishamzoea Pro CCM, yeye kwake chongo ya CCM ni kengeza!
   
 4. myhem

  myhem JF-Expert Member

  #4
  Mar 6, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  naona umeamua kukusanya maoni ya BANA.sijui ulitetegemea aseme nini zaidi ya hayo aliyosema.
   
 5. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #5
  Mar 6, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  mh! Kila mtu akidai haki yake ni mkono wa mwanasiasa
   
 6. N

  Njaare JF-Expert Member

  #6
  Mar 6, 2012
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 1,075
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Wakati wa ndiyo mzee umekwisha. Sasa hivi ni wakati wa uwazi na ukweli. Hatuwezi kumsubiri miaka mitano ipite ndo tumwadhibu. Sasa hivi adhabu ni hapo hapo kama wanavyofanyiwa vibaka. Hatukubali achezee roho zetu. Mchezo wa serikali na madaktari ni mauti kwetu. Lazima aliyeanzisha huo mchezo na anayependa uendelee alazimishwe kuuacha.

  Hawa wanaojiita wasomi ni wavivu tu wa kufikiri na huwa wanaviamini visababu uchwara vya CCM. Ni nani asiyejua kuwa hakuna mwanasiasa anayetibiwa hata kufanya check up hapa nchini. Ni nani asiyejua sababu yao kutokutibiwa hapa. Je, Tanzania tuna raia wa 1st class na 3rd class? unafikiri hawatibiwi hapa kwa sababu wanapenda au ni kwa sababu wanajua kuwa hospitali zetu hawazipi fungu la kutosha hivyo hazina vifaa vya kutosha.
   
 7. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #7
  Mar 6, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Yupi asiye na hoja? mleta huu uzi au waliosema?
   
 8. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #8
  Mar 6, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Do you really think that it can work?
   
 9. Emmani

  Emmani JF-Expert Member

  #9
  Mar 6, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 525
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hivi mkuu unaweza kweli kutumia muda wako kum-quote Dk. Bana!!!!!
   
 10. M

  Mpanzi JF-Expert Member

  #10
  Mar 6, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 767
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Bana ni msomi ambae hajaelimika!
   
 11. mamaWILLE

  mamaWILLE Senior Member

  #11
  Mar 6, 2012
  Joined: Jul 27, 2011
  Messages: 152
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Bana mlopokaji hana lolote zaid yakujipendekeza tu.
   
 12. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #12
  Mar 6, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Huyu ni mmoja kati ya watu waliouza utu na usomi wao kwa sababu ya kuneemesha matumbo yao; hawana weledi wala uzalendo wa kuwafikiria na kuwatetea mama ,baba, dada na kaka zao ambao wanateseka kwasababu ya ubinafsi na ufisadi wa viongozi wa ccm!
   
 13. Lasikoki

  Lasikoki JF-Expert Member

  #13
  Mar 6, 2012
  Joined: Jan 10, 2010
  Messages: 642
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Of all the people, BANA is hopeless. Anatumia elimu yake ya vyeti kuwahadaa watanzania. Maana msomi kweli kweli ni yule anayetumia usomi wake kusema ukweli na kushauri, siyo huyu proCCM BANA
   
 14. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #14
  Mar 6, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,709
  Trophy Points: 280
  Ulitegemea Ban aseme nini?
   
 15. D

  DOMA JF-Expert Member

  #15
  Mar 6, 2012
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 946
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Kumbe bana khaa
   
 16. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #16
  Mar 6, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  unatosha kuwa na akili ya ziada kuwa hapa JF ,,,,,,THREAD IMEJAA UKWELI MTUPU
   
 17. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #17
  Mar 6, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Bana anaropoka = chadema wanaropoka = Freemason Mbowe
   
 18. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #18
  Mar 6, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  yani wewe ni zaidi ya ki.az.i
   
 19. O

  Omulangi JF-Expert Member

  #19
  Mar 6, 2012
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 1,026
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Nafikiri kuna ukweli kuwa wanasiasa wanatumika kuchochea mgomo wa madaktari. Mhe Pinda amedhihirisha wazi kuwa siasa kwake ni muhimu kuliko maridhiano. Mbona alishakubali kukaa na madaktari na muafaka ukawepo wakarudi kazini?

  Hakuna aliyemwuliza zile kauli zake za mwanzo ilikuwaje?

  • Alikataa kusubiri siku moja akutane na ma dr j3 akidai anashughuli muhimu zaidi za bunge! kumbe kikao cha bunge kilikuwa muhimu kuliko uhai wa watu.Na mbona aliacha tena bunge na kuja kukutana na ma dr.
  • Alituhaidi watakaogoma wamejifuta kazi. Hakutujulisha baadaye ni wangapi walijifuta kazi.
  • Alisema Ameandaa ma dr toka jeshini wala hakuna litakalo haribika? Hivi kweli ma dr wa Jw walikuja kuwa mbadala pale Muhimbili na kwingineko.
  • Ni kweli wanasiasa wanaingiza siasa katika kila jambo, na hata katika mgomo wa madaktari.
   
 20. B

  Benaire JF-Expert Member

  #20
  Mar 6, 2012
  Joined: Dec 13, 2011
  Messages: 1,947
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Unajua hapa ndio tunapoudhalilisha usomi wa Tanzania...msomi hapaswi kujustify hisia zake kuwa ndio sababu ya tatizo fulani...msomi hujipa muda kufanya tafiti kisha kugundua sababu za tatizo na jinsi ya kulitatua!
   
Loading...