*==AIBU KWAKO GODBLESS LEMA==*
_Na_ _Mwananchi wa_ _Moshi_ .
Nimeshangaa sana kumsikia Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema akidai maafisa usalama wanazuia shughuli ya kuaga mwili wa Marehemu Philemon Ndesamburo.
Huyu jamaa ameendeleza ugonjwa wake wa kukosa hoja za kisiasa na kuwahudumia wananchi waliomchagua na badala yake sasa anageuza misiba ndio mahali pa kufanyia siasa. Lema anataka kupanda mbegu mbaya kwa watanzania. Hivi Lema umefikia kutafuta kiki za kisiasa kwenye misiba?
Labda tuwekane sawa.
Kilichofanywa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Moshi ambayo inaongozwa na CHADEMA ni uungwana Mtupu.
Kwamba uwanja wa Mashujaa ni mdogo na hauwezi kuhimili idadi kubwa ya watu wanaotaka kushiriki kuuaga mwili wa Mzee wetu Ndesamburo. Mkurugenzi ameshauri kwa tena yenye lugha ya upole na unyenyekevu kuwa utumike uwanja wa Majengo ambao ni mkubwa na upo jirani na nyumbani kwa Marehemu.
Na kwa taarifa yako Ndg. Lema Serikali inaposema hivyo inazingatia mambo mengi. Kuna kuepusha msongamano wa watu na magari, kurahisisha mambo ya usalama endapo jambo lolote likitokea na pia kulipa heshima tukio lenyewe hasa ikizingatiwa Marehemu Mzee Ndesamburo alikuwa mtu wa watu.
Nashangaa huyu Mbunge ambaye kama kawaida yake ya kukurupuka na kutoa hoja vioja anakuja na kutoa maneno ambayo hata wana CHADEMA wenzake wanashangaa.
Yaani sasa hivi Lema amekuwa mjuaji wa kila kitu.
Na nimemsikia mahali anamtaja hadi Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Bw. Mrisho Gambo, yaani kamshindwa Arusha sasa kaona aje abangaize kumshanbulia akiwa Moshi. Anamsema Kaimu Mkuu wa Mkoa Bw. Gambo ambaye hata Kilimanjaro hajafika.
Maamuzi haya yamefanywa na uongozi wa Wilaya kwa kushirikiana na Halmashauri. Na kama wafiwa ama CHADEMA hawaridhiki walikuwa wanaweza kuwasiliana na Mkuu wa Mkoa kabla ya Bw. Lema kukimbilia kwenye mitandao ya kijamii na kutafuta Kiki. Ndg. Lema chukua faida legacy ya Mzee Ndesamburo ndio muhimu kuliko kutaka kifo chake kikujenge kisiasa Kaka.
Ukijenga tabia hiyo utajikuta unamuombea kila mtu muhimu ndani ya CHADEMA afe ili upate nafasi ya kupata kiki ya kisiasa. Ulifanya hivyo kwa watoto wetu 32, walimu 2 na Dereva wa Lucy Vincent School waliopoteza maisha ajalini, ukidai umenyiwa nafasi ya kuongea msibani na leo unarudia kwa Mzee Ndesamburo? Nilidhani umejifunza kumbe Daaaa!!!! Hii ni Aibu kubwa. Tuache tumzike Mzee wetu Ndesamburo kwa Amani, mwache Mzee Ndesamburo alale mahali pema, mwache Mzee Ndesamburo azikwe na maombi ya Watanzania wote usilete ubaguzi, acha Watanzania wote wamlilie Baba yao.
Siasa zako tafuta pa kuzifanyia sio hapa aisee!!!!
Na kwa taarifa yako hata Mwenyekiti wako Freeman Mbowe anakushangaa. Ndio maana ulipojifanya kuamuru Makomandoo wa CHADEMA wapambane kuhakikisha shughuli inafanyikia uwanja wa Mashujaa Mbowe amekupinga na kuagiza maandalizi yakafanyike uwanja wa Majengo.
Kaka tunamzika Mzee wetu aliyefanya siasa za kistaarabu nawe fanya siasa za kistaarabu. Ubabe wako hauna maana. Unazidi kuwa kituko kila kukicha.
Wacha mimi niendelee kumlilia na kumuombea Mzee wangu Ndesamburo.
C&P