Sakata la Korosho,nini kifanyike?-Mjadala.

Sakata la Korosho,nini kifanyike?-Mjadala.

mkimagii

Member
Joined
Oct 16, 2013
Posts
34
Reaction score
58
“Mkataba huo ulifikishwa kwenye ofisi ya mwanasheria mkuu, umepitiwa,tumeridhika,mkata huu imekidhi hatua zote za kisheria na ushahidi wote ulio takiwa kufanyika”. Haya ni maneno ya Waziri Prof. Kabudi wakati akitia sign mkataba na kampuni ya Indo power ya Kenya kununua korosho kwa Tshs 4,180,000/= kwa tani.Wakati huo bei ya Korosho kwenye soko la dunia imeendelea kushuka kwa 10.1% kipindi cha 2018/2019,kupelekea korosho ghafi kuuzwa kwa wastani wa Tshs 3,174,000/= kwa tani.

Mnamo mwezi wa tano,mkataba kati ya Indo power na Serikali ulishitishwa kutokana na mnunuzi kushindwa kukizi vigezo vya mkataba. Kwa sasa Serikali imeingia mkataba mwingine na kampuni sita kununua hizo korosho. Ukweli ni kwamba kama Taifa tutapata hasara huu msimu,maana korosho zimeshakaa sana karibia kuaribika(expired).Bila shaka,kama wanunuzi watanunua,basi watanunua kwa bei ya hasara. Kama tunavyo jua,kitu kinacho karibia kuaribika kawaida kinauzwa kwa bei ya kutupa au ya chini sana.

Tukubali kwamba tumekula hasara huu msimu,hii ni hali ya kawaida kwenye ulimwengu wa biashara. Kuzuia makosa kama haya kujirudia,nini kifanyike kwa msimu ujao?

1.Raisi anasema korosho zikaagwe, zibanguliwe na kuuzwa.Hii nadhani ni ngumu kuwezekana maana hatuna viwanda vyakuweza kubanguwa korosho kwa ujazo mkubwa.Na kama tukifanikiwa kuzibanguwa,korosho zitakuwa nyingi sokoni ambapo itapelekea bei kushuka sana karibia na bei ya bure.Pili sidhani kama kutakuwa na walaji wa kutosha kuweza kumaliza hizo tani za ujazo ndani ya miezi sita kabla ya korosho kuaribika. Hivyo,kama tukijaribu hii njia tutapata hasara.
Lakini,hii njia inaweza kufanikiwa kama tukiamua au kufanikiwa kujenga kiwanda kikubwa cha ubanguzi wa korosho na kuhifadhi.Ingawa itaitaji mitambo ya kisasa yenye gharama bila shaka faida itakuwa ni kubwa.

2.Korosho sio zao jipya,hivyo kutakuwa na wanunuzi wa kudumu.Tujaribu kufanya mazungumzo nao ili kuweza kupata bei nzuri ambayo inakaribia bei ya soko.Mazungumzo haya ni vyema yafanywe miezi michache au hata mwaka kabla ya mavuno. Mwisho,kwenye mikataba tunatakiwa pia kuhakikisha kuna kuwa na “guarantee” ya malipo na jinsi hasara itavyo
fidiwa kama mkataba ukishitishwa. Fidia ya mkataba kuvunjwa lazima iwe na uwalisia(reasonable)na uwezo mkubwa wa kupunza idadi ya wanunuzi kuvunja mikataba hovyo.

3. Kama hatuta pata mnunuzi wa kueleweka,basi tunaweza kutengeza pool ya wanunuzi.Ndani ya hiyo pool tukawapa vipande(share) za kununua korosho.Hii itatusaidia kupunguza risk ya hasara ya korosho kutuaribikia au kuuzwa kwa bei ya kutupwa kutokana na wanunuzi kuvunja mikataba.

Nini unadhani kifanyike kukuza zao la korosho?
 
Hakuna namna tumeishaingizwa mkenge na jiwe.siku ile akikagua magari ya deraya alijisifu sana kuwa ana jeshi ana Mungu ana pesa ya kununua korosho zote kwa masaa machache,nini kifanyike kwanza ajitokeze hadharani aombe radhi watanzania wote kwa hasara na mateso aliowasababishia halafu tutathmini hasara yote ikiwa pamoja na kukosa fedha za kigeni pia kwa kushindwa kuziuza ina maana kuna pahali fedha zilichotwa so atueleze tutazifidia vipi.
 
Wagawiwe hizo korosho wanaume wa dar(esp. Kinondoni) maana utafiti umeonyesha 24% inaonekana wana matatizo ya nguvu za..
 
Naipenda nchi yangu,natamani nishiriki hata kwa mchango wa mawazo ili kisukuma mbele maendeleo ya nchi yangu,,,,nadhani rais anapewa taarifa ambazo si halisi kwny field na ndyo kinachotuponza kama taifa,kwenye dunia ya leo ya kibepari ambayo imeshuhudia kuanguka na kushindwa kwa ujamaa,mfumo unaoletwa kwenye mazao mengi ya biashara hata kwenye mikataba mingine itafeli sana kama kutakuwa na mazngra ya kutaka kulidisturb soko huria (universal market),mfano kwenye pamba kulikuwa na wanunuzi permanent (alliance, villian,olam,nsagali,ndegesela,gaki, nk),serikali kuingia kuwa mtu kati kwa kigezo cha ushirika itaendelea kuwaumiza watu wake,na hasara itaendelea kupatikana,nadhani serikali ingetengeneza sera na kubaki kukusaya mapato halaf biashara ikabaki kuwa kati ya mkulima na mnunuzi,kama nje ya ushirika (vyama vya msingi) walikulima waliibiwa kwann walikuwa na fraha na waliifrahia misimu kulikoni ilivyo sasa?
 
wanunuzi walikuwepo shida ilikuja/inakuja pale raisi anapofikiria kwamba yeye anaakili nyingi kuliko wote kumbe lah.ifumo ilikuwepo na ipo . alipaswa kufanya intervention lakini sio kununua... hakika huyu ameharibu sana uchumi wetu
 
IMG_1124.JPG


Kiumbe kama hiki kwa sasa China wanakifanyaje.
 
Korosho biashara kichaa sahivi.

Aliesababisha haya yote awajibishwe.
 
Korosho wahusika wote wawajibishwe Kwa kuhujumu uchumi wa watu wa kusini wamecheza Na maisha yao,wahukumiwe Kwa kunyimwa kura za ndio,Na mahakamani waburuzwe
 
Back
Top Bottom