Vyombo vya habari mbali mbali leo vimeripoti taarifa ya polisi kuwashikilia watuhumiwa watatu wa uvamizi wa mkutano wa mwenyekiti wa CUf wilaya ya kinondoni ambao watu mbali mbali wakiwemo waandishi walijeruhiwa na mali kuharibiwa.
Nilibaki kinywa wazi pale Polisi kupitia kamanda Siro kueleza kuwa hakuna aliye juu ya sheria na kuonya kwamba ikiwa kuna kikundi cha watu hakiridhiki na jambo fulani basi waende mahakamani na SIO KUFANYA JINAI. NILISHANGAA SANA LAKINI NIKAJIULIZA HAWA POLISI WETU KWELI WALAU WANA KUMBUKUMBU?
Kwamba hizi vurugu za watu wa Lipumba na jinai hiyo iliyopelekea kuwashikilia hao watu watatu imeanza juzi jumamosi tarehe 22 Aprili, 2017 tu ? Wamesahau kuwa Lipumba na genge lake walivamia pale Blue Pearl hotel ubungo , walijeruhi na kuharibu mali na hakushikwa yoyote wamesahau ? wamesahau kuwa hata wale watuhumiwa walioshikwa na kupelekwa polisi magomeni waliachwa kwa mizengwe ?
Polisi wamesahau kuwa genge hili la lipumba lilifanya jaribio la kumteka Mkurugenzi wa Fedha wa CUF ndugu Bashange na kufanya vurugu mahakamani kwa kumzuiya mwenyekiti wa bodi ya wadhamini kule kisutu ? Pilisi wamesahau kuwa kuna jinai hapa ilitokea ya watu kuchomwa visu wamesahau hawa ?
Hivi ni vioja vya wazi lakini ni taswira halisi ya serikali iliyopo. Ikiwa kuna kiongozi anadiriki kuvamia kwenye kituo cha habari amelindwa na polisi kushindwa walau kumuhoji unategemea nini? Kibaya zaidi ngazi ya kiuongozi iliyo juu ya mtuhumiwa uhalifu ilipochukuwa hatua za kiuongozi zilizo chini ya mamlaka yake kutaqka kulishughulikia tatizo wote tunajuwa nini kilimtokea Ndugu Nape.
Mambo ni mengi leo sikusudii kuyataja yote hapa, Lakini ni wazi hiki kioja cha polisi na sakata la CUF linaakisi mambo yalivyo katika awamu hii ya uongozi.
Ndugu zetu Poilisi HADI LINI MTASIMAMA KULINDA HESHIMA YENU ?
Kishada.