Safi Rais Magufuli kumtoa Kitwanga, lakini kauli ya Lema imenipa maono tofauti na kuniogopesha

Pro Magufuli Wa 47

Senior Member
Mar 5, 2016
188
58
Mbunge wa Arusha Mjini (Godbles Lema) alinukuliwa akisema
'Sisi tunazielewa Siasa za Bunge, am telling you, am telling u my brother Lugumi is nothing in this parliament wanakutafuta wewe Kitwanga wanasema wewe ndo kiherehere mkubwa kwa Rais utakuja kuniambia'
Je Bunge letu lipo salama?
Sentensi ya Lema inaonyesha kuwa ni kama kawaida Wabunge kutumika kuunda zengwe kwa Viongozi wa serikali ili waondolewe kwa maslahi ya watu kadhaa iwe Wazuri ama Wabaya.
Kitwanga alikuwa anawindwa mostly na drug kingpin na waarifu wengine wengi waliobanwa kimaslahi mfano kupitia Takukuru au jeshi la polisi na hivyo kumuundia zengwe atolewe.
Kitwanga alichokosea ni kung'ang'ania Cheo, alipaswa akae pembeni kupisha uchunguzi badala ya kukomaa.
Stress za Lugumi, Mauaji ya Mwanza zimemfanya apige viroba.
Yote heri, kama wanahisi wamepona, Dr Magufuli atawa-spprize atakuja na kiboko zaidi ya Kitwanga, hivyo waharifu wajipange.
 
Neno moja tu la lema wanakutafauta wewe kitwanga tayari kwa maneno yake wamempata kama ushindi wameshinda bila kujali sababu iwe ulevi au lugumu au urafiki wake na raisi tayari hayupo alipokua
Nini malengo ya huko mbele ndo muda wa kutafakari
 
Kama ni cha pombe mnajua nyie ila Hongera sana lema hata wafiche ukweli wako

Na hata kama watanzania hawajaona bas sisi tuliokusikia hongera sana
 
Atapata chaka lingine la kutafuna mhogo mbona kenya machief wakiacha pombe na kuomba radhi wanarejesha heshima!
 
Wa Tanzania sijui lini tutaacha ukweli uwe ukweli na tuache kuishi kwa kuvuziana. Sasa unaambiwa kafutwa kazi sababu kaenda kazini akiwa amelewa, unaacha kulichukulia hivyo unaanza Ku create kichwani kwako unavyotaka wewe, unataka kutuambia hakuna Tatizo kuingia bungeni ukiwa umelewa? Au hakupaswa kutimuliwa kwa kuingia huku kalewa?

Usiishi kwa mazoea mkuu, kaingia kalewa kafutwa kazi, baaaaaasi! Acha kujenga mahesabu meeeeeeeeengi kichwani, utajipunguzia muda wako wa kuishi.

Kama ishu Ni Lugumi au urafiki na namba moja au ulevi mwisho wa siku Kitwanga kaonekana hafai katenguliwa, hili ndio kubwa, imetosha! Usitake kutuaminisha Kuwa JPM katumwa na wauza unga ili amtoe Kitwanga sababu alikuwa anawabana, a big NO! Sitakuamini kamwe.

Nimemaliza
 
Mbona anaonekana ndio sauti yake ya kawaida au issue ya lugumi ndio imechangia

Mawaziria Na wabunge kuingia wakiwa wamelewa ni Jambo la kawaida, ila jamaa yeye alizidisha akawa anajibu maswali anavyojisikia.

Ndio Maana hata Masha amekiri wazi kuwa alikuwa anagida Ndovu kabla ya kutinga Bungeni kujibu maswali ila yeye hajawai shitukiwa.
 
Tho
Hu huo ni mche
Huo ni mchezo uliochezwa ili kitwanga asihojiwe juu ya keso ya lugumi. Msiishi kama hamna akili. Akitenguliwa nafasi yake wapinzani mta muhoji nani? Lema shitukeni mkihamka mmeliwaaaa. Ilipangwa na imetokea.
think twice lini ilitokea amekuja kalewaaa?
 
Mi sijamuelewa huyu lema, ana maana hata lugumi ni mpango tu wa kumng'oa kitwanga katika uwaziri. Kama ndivyo mbona hata yeye aliikomalia lugumi ili jamaa ang'oke. Kama ndivyo je naye ametumika???
 
Back
Top Bottom