dubu
JF-Expert Member
- Oct 18, 2011
- 3,500
- 3,481
Mbunge wa Ubungo,Saed Kubenea,amehojiwa na Kamati ya Haki Maadili ya Bunge kwa madai ya kusema uongo bungeni
Mbunge wa Ubungo (Chadema), Saed Kubenea amehojiwa kwenye Kamati ya Bunge, Maadili na Madaraka inayoongozwa na George Mkuchika kwa tuhuma za kulihusisha Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Waziri wake, Dk Hussein Mwinyi kwenye ugawaji wa ardhi kwa Kampuni ya Henan Guiji Industry.
Mbunge huyo amefikishwa mbele ya kamati hiyo Alhamis iliyopita ili kujibu mashtaka hayo baada ya Dk Mwinyi kulalamika wakati akihitimisha hoja ya bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2016/17.
Dk Mwinyi ameliambia Bunge wakati akihitimisha bajeti ya wizara hiyo kuwa yuko tayari kujiuzulu uwaziri iwapo Kubenea atathibitisha tuhuma hizo mbele ya Bunge.
Naibu Spika, Dk Tulia Ackson alimwagiza Kubenea kupeleka uthibitisho katika kamati hiyo ili ukachunguzwe.
Chanzo: Mwananchi